Nafasi za Kazi Gardaworld Security Tanzania

View attachment 808369

Kampuni ya ulinzi ya KK Security Tanzania Ltd. Yenye ofisi yake Capripoint mbele kidogo na Kamanga Fery Mwanza na ofisi kuu Mikocheni B Dar es Salaam, Inatangaza nafasi ya kazi Ya ulinzi.

VIGEZO
  1. Elimu: Kidato cha nne na kuendelea.
  2. Uwezo wa kusoma, kuandika na kuongea kiingereza.
  3. Umri wa miaka 23 - 42
  4. Urefu futi 5.7 na kuendelea (kwa wanaume)
  5. Afya njema
  6. Asiwe na makosa yeoyote ya jinai
  7. Awe tayari Kazi Mkoa wowote wa Tanzania.
HATUA
  • Mwombaji Afike na barua ya maombi ya kazi iliyoandikwa kwa mkono na mwombaji kwa kiingereza
  • Nakala za vyeti na vyeti halisi, cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo.
  • Barua ya utambulisho kutoka kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa.
  • Barua za wadhamini wawili (zipiigwe muhuri kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa juu ya picha na Wasiwe walinzi au wanafunzi).
  • Mdhamini awe na kitambulisho halali.
  • Mwombaji awe na picha 5 za pasipoti zilizopigwa hivi karibuni
  • Mwombaji awe tayari kwa mahojiano na usaili.

Usaili utafanyika kuanzia Tarehe 16 July , Ofisini kwetu Capripoint Mwanza kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni.

Epuka matapeli, Hakuna rushwa ni vigezo tu vinazingatiwa.

Broo nataka kumsendi mdogo wangu juma tatu aje vigezo vyote anavyo but naomba unieleweshe hapo je, anaweza kuja na barua ya wadhamini walioko nje ya mwanza au mpaka apate wadhamini wote kutoka hapo hapo mwanza? Maana yeye si mkazi Wa mwanza
 
well, kama atafaulu usaili wadhamini watahitajika kufika ofisini kwaajili ya kusign documents mbali mbali hivyo nadhani ni nafuu Zaidi kama utapata wadhamini wanaomwamini, maeneo ya karibu.
 
Shukrani ngoja tuanze utaratibu
 
Nyie watu waongo sana! Mnakumba mlikuwa na site north Mara good mine (Nyamongo)!? Mlikuwa mnawatesa sana Vijana wenu mpka sasa kampuni yenu imegawanyika, na baadhi ya top leaders wanaanzisha kampuni nyingine ya ulinzi! Walinz wa kampuni mama (mgodi) walikuwa wanaliowa 90+ lakini walinzi wenu mlikuwa mnawapa laki na sabini! Mpuuzi gani mtakayempata? Nyie n watanzania, acheni kuwatumikia makuburu kiasi hicho!
 
Kati ya kampuni za kinyonyaji na kinyanyasaji KK wanaongoza mshahara kiduchu halafu maboss wanawanyanyasa sana wafanyakazi,rushwa ya ngono imeshamiri sana kwenye kampuni hii hasa mwanza
 
well, kama atafaulu usaili wadhamini watahitajika kufika ofisini kwaajili ya kusign documents mbali mbali hivyo nadhani ni nafuu Zaidi kama utapata wadhamini wanaomwamini, maeneo ya karibu.
Mkuu vvm umefunga pm yako? Kila nikijaribu kukutumia ujumbe inashindikana.
 
UPDATE
INTAKE MPYA IMEANZA KUPOKELEWA MWISHO TAREHE 24 AUGUST 2018
 
Acha kuharibu akili za vijana wenzako kwa ujira mdogo.
Health insurance ya aina gani mnaitoa nyie kama sio ile ya one healthy centre/hospital only ambayo hata mkulima mdogo huweza kujilipia.
Nimefanya kazi G4s najua upuuzi wa kampuni hizi. Kk nako kuna marafiki zangu waliwahi kufanya pia.
Ni full utumwa.
 
Makampuni kama G4S NA KK SECURITY yamejaa wezi mshahara wa laki mbili na nusu hapo haujaumwa siku zote upo job bado hujaombwa rushwa na wakaguzi mteja analipa milion mlinz unapewa laki majizi sana haya
Sasa wao watapate faida. hayo magari yaliyoandikwa Rapid Response yatapata wapi mafuta .
 
View attachment 808369

UPDATE NAFASI MPYA TAREHE 15 MPAKA 24 - AUGUST-2018

Kampuni ya ulinzi ya KK Security Tanzania Ltd. Yenye ofisi yake Capripoint mbele kidogo na Kamanga Fery Mwanza na ofisi kuu Mikocheni B Dar es Salaam, Inatangaza nafasi ya kazi Ya ulinzi.

VIGEZO
  1. Elimu: Kidato cha nne na kuendelea.
  2. Uwezo wa kusoma, kuandika na kuongea kiingereza.
  3. Umri wa miaka 23 - 42
  4. Urefu futi 5.7 na kuendelea (kwa wanaume)
  5. Afya njema
  6. Asiwe na makosa yeoyote ya jinai
  7. Awe tayari Kazi Mkoa wowote wa Tanzania.
HATUA
  • Mwombaji Afike na barua ya maombi ya kazi iliyoandikwa kwa mkono na mwombaji kwa kiingereza
  • Nakala za vyeti na vyeti halisi, cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo.
  • Barua ya utambulisho kutoka kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa.
  • Barua za wadhamini wawili (zipiigwe muhuri kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa juu ya picha na Wasiwe walinzi au wanafunzi).
  • Mdhamini awe na kitambulisho halali.
  • Mwombaji awe na picha 5 za pasipoti zilizopigwa hivi karibuni
  • Mwombaji awe tayari kwa mahojiano na usaili.

Usaili utafanyika kuanzia Tarehe 16 July , Ofisini kwetu Capripoint Mwanza kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni.

Epuka matapeli, Hakuna rushwa ni vigezo tu vinazingatiwa.

UPDATE:

INTAKE MPYA IMEANZA RASMI LEO (15-AUGUST-2018) MPAKA 24-AUGUST-2018
WAOMBAJI WENYE VIGEZO WANAKARIBISHWA

KUMBUKA, TARATIBU ZOTE NI BURE HIVYO EPUKA MATAPELI.
Mkuu endelea kutupa update kama zikitoka nafasi za kazi kuna watu kibao bado wanahitaji huku mtaani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom