Nafasi za kazi kampuni ya kuzuia ujangili (kwa waliopitia jkt tu)

D Metakelfin

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
2,873
2,000
GRUMETI FUND TRUST.
TANGAZO LA KAZI
Grumeti Fund Trust inatangaza nafasi za kazi zifuatazo;
Askari wa wanyamapori
Majukumu ya Askari wa wanyapori:
Majukumu ya msingi kwa Askari wa wanyapori ni kufanya kazi kwa kushirikiana na wadau wa Serikali wa
Grumeti Fund kuhakikisha usalama kwenye eneo la hifadhi la Grumeti-Ikorongo. Askari wa wanyapori wana
wajibu wa kuhahakikisha kuwepo kwa maadili kwenye eneo la hifadhi la Serengeti, hii inajumuisha
kuhakikisha kunakuwepo na mazingira ya usalama wa wanyamapori na kwa uoto wa asili. Askari wa
wanyapori wana wajibu wa kuzuia vitendo vyovyote vilivyo kinyume na sheria na vilevile kuzuia vitendo
vyovyote vya ujangili ndani ya eneo la hifadhi. Watakuwa chini ya utawala na watawajibika kutoa taarifa ya
vitendo vyovyote vilivyo kinyume na sheria kwa utawala wa Grumeti Fund na kwa wadau wa Serikali.
Tarehe ya tangazo 05 /01/2020
Nafasi za kazi Askari wa wanyamapori
Idara husika Kuzuia Ujangili
Kituo cha kazi Wilaya ya Serengeti, Mkoa wa Mara, Tanzania
Msimamizi wa kazi Mkuu wa Idara ya Kuzuia Ujangili (Anti-Poaching Manager)

Ufafanuzi wa majukumu:
 Kushiriki kwenye mafunzo ya majuma sita (6) ya uteuzi
 Kufanya doria kwenye eneo la hifadhi kwa jitihada za kuhakikisha kuwa liko salama kwa wanyamapori
 Kuzuia vitendo vyovyote Vilivyo kinyume na sheria kwenye eneo husika la hifadhi kwa mfano ujangili,
uchungaji mifugo usioruhusiwa, ukataji wa miti na utengenezaji wa mkaa na kutembea maeneo ya hifadhi,
 Kusaidia kuwakamata majangili kwenye eneo la hifadhi
 Kutoa taarifa zozote za ujangili au za matendo yoyote yaliyo kinyume na sheria ambayo yatajulikana
 Kusaidia usalama wa maisha ya watu, mazao na mifugo iliyoko karibu na eneo la hifadhi inayoweza kuvamiwa
na wanyamapori
 Kuwa tayari kufanya kazi muda wowote mchana au usiku
 Kufanya kazi zozote za idara kama zitakavyoelekezwa na utawala
Sifa za waombaji
1. Angalau aliyehitimu na mwenye cheti cha elimu ya kidato cha nne
2. Angalau mhitimu wa ngazi ya Stashahada kwenye usimamizi wa wanyamapori (Wildlife Management)
3. Aliyehitimu mafunzo kamili ya jeshi la kujenga Taifa (JKT) ya kuanzia miezi sita (6). Wenye Mafunzo ya
miezi mitatu hawataruhusiwa.
4. Mwenye uwezo wa kuwasiliana vizuri kwa Kiingereza na Kiswahili kwenye kuandika na kuzungumza
5. Mwenye uwezo wa kuandaa taarifa ya kazi vizuri na inayoeleweka vema.
6. Muombaji awe na umri wa miaka 23 mpaka 35
7. Muombaji ni lazima awe na moyo wa kuwapenda wanyamapori

Vigezo vya uteuzi
1. Waombaji wa nafasi hizi za kazi ni lazima wawe wakakamavu, wenye afya njema ya mwili na ya akili
2. Waombaji wote wa nafasi hizi ni lazima wawe tayari kupimwa afya, upimwaji huu utafanywa na wataalamu
wa afya wa kampuni
3. Waombaji wote wa nafasi hizi na ambao wataitwa kwa ajili ya usaili ni lazima wawe tayari kushiriki kwenye
mafunzo ya muda wa majuma sita (6) ya ukakamavu na kuchunguzwa tabia zao. Mafunzo haya ya muda
mfupi ni ya mchujo na hayatoi kibali cha kuajiriwa.
4. Waombaji wote watakaoitwa kwenye usaili watapaswa kujigharamia gharama za usafiri. Malazi na chakula
vitatolewa kituoni bila gharama yoyote.
Jinsi ya kutuma maombi yako:
Ikiwa unapenda kuomba nafasi hizi za kazi na umekidhi vigezo kama vilivyoainishwa hapo juu basi fuata masharti
yafuatayo;
1. Andika barua ya maombi ya kazi na uambatishe taarifa zako binafsi zinazoeleweka vyema (CV), cheti cha
kuzaliwa, pamoja na vyeti vya kuhitimu taaluma yako. Taarifa zako binafsi (CV) ni lazima zioneshe mahali
unakoishi kwa sasa, namba zako za simu zinazopatikana pamoja na anuani na namba za simu za watu angalau
watatu (3) wanaokufahamu vizuri na wanaoaminika ambao watakudhamini.
2. Waombaji wote waliohitimu mafunzo ya kujenga taifa (JKT) ni lazima waambatishe barua ya utambulisho
kutoka JKT pamoja na cheti cha kuhitimu mafunzo hayo.
3. Vyeti vyote vitakavyowasilishwa vitafanyiwa uchunguzi wa hali ya juu, muombaji atakayewasilisha cheti cha
uongo au atakayetoa taarifa za uongo ataondolewa mara moja na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
4. Maombi yote yatumwe kwa Mkuu wa Idara ya Rasilimali watu; ama kwa anuani ya barua elekroniki (email)
ambayo ni: jobapplications@grumeti.singita.com au kwa njia ya Posta kwenda kwa
Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu
Grumeti Reserves Ltd
S.L.P. 65
Mugumu, Mara, Tanzania.
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI NI TAREHE 18/01/2020, SAA 11.00 JIONI.
Grumeti Fund Trust haina ubaguzi wa aina yoyote kwenye kutoa ajira.
 
sulai

Member
Jan 11, 2017
61
125
ina maana sisi tuliopitia mafunzo ya mgambo hatuna nafasi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom