Nafasi za kazi JWTZ zatangazwa

BILGERT

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
4,951
2,000
Ni kweli mkuu, Maaana hapo mgulani watu itakuwa zaidi ya maelfu, chukulia wahitimu Tangu 2014- 2017 kwa Kada tofauti, utaisha lini huo usaili na tutatumia garama gani? Maana itakuwa zaidi ya wiki sasa, sasa sisi walalahoi situtakosa na nauli ya kuludia kabisa.
Watajaa hao madaktari bingwa ama?
 

the galaxy a

Senior Member
Mar 25, 2017
183
250
Hivi nataka kuuliza swali kwa wale ambao hawajasomea medical records ila wamesomea mambo record management je wanaweza kuomba kazi/hapo jeshini?
Hapo kwenye cheti chako mwanzoni ongezea medical iwe inasomeka medical records management watakuchukua
 

BUROFELO

Member
Oct 1, 2013
40
125
-Specialists
-Medical Doctors
-Clinical Officers
-Ass clinical Officers nk

Tar 17/12/2018 kuripoti Mgulani. View attachment 961764

======

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini Madaktari wa Binadamu na fani nyingine za Tiba.
Nafasi hizo zinatolewa ili kuongeza idadi ya wataalamu wa tiba watakaotoa huduma za afya katika Hospitali zetu, vituo vya afya na Zahanati kulingana na mahitaji ya sasa na siku zijazo.

Watakao andikishwa Jeshini ni wale wenye taaluma zifatazo:-

a. Daktari Bingwa wa Meno – Dental Surgeon

b. Daktari Bingwa – Specialist Neurasurgeon

c. Mkemia (Chemisist)

d. Mteknolojia Msaidizi (Maabara) – Assistant Laboratory Technician.

e. Tabibu msaidizi – Assistant Clinical officer.

f. Katibu wa Hospitali –

g. Msaidizi wa kumbukumbu. – Medical Records (Certificate)

h. Daktari – Medical Doctors.

j. Afisa Muuguzi – Registered Nursing Officer.

k. Fundi sanifu vifaa tiba – Bio Medical Engineer.

l. Tabibu – Clinical Assistant (Certificate).

m. Mteknolojia msaidizi – Laboratory Assistant (Certificate)

n. Mfamasia – Pharmacist (Degree)

o. Mtoa tiba kwa vitendo – Physiotherapist (Diploma)

p. Afisa Muuguzi msaidizi – Assistant Nursing officer

Sifa za kuandikishwa Jeshini ni zifuatazo:-

a. Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.

b. Awe na umri kati ya miaka 18 hadi 28 isipokuwa specialist

c. Awe na afya njema ya mwili na akili timamu.

d. Awe mwenye tabia njema na nidhamu nzuri

e. Awe hajawahi kupatikana na hatia ya makosa ya jinai Mahakamani na kufungwa jela.

f. Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate), vyeti vya shule (Academic & School Leaving Certificates) na vyeti vya Chuo (Transcript & Academic Certificates).

g. Kama ni Daktari awe amemaliza mafunzo kwa vitendo (Internship) na kutunukiwa vyeti pamoja na kusajiliwa na Bodi.

h. Awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo.

Wenye sifa tajwa na kuhitaji kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania waripoti katika Kambi yaJenerali Abdallah Twalipo, Mgulani Dar es Salaam tarehe 17, Desemba, 2018 kuanzia saa 1.00 Asubuhi kwa usaili.

Waombaji wafike na vyeti halisi (Original Certificates) vya kuzaliwa na masomo pia wajitegemee kwa usafiri, chakula na malazi.

Aidha, watakaochaguliwa na kuandikishwa Jeshini watapatiwa mafunzo mbalimbali ya Jeshi na yatakayo waendeleza katika taaluma zao. Wakiwa Jeshini majukumu watakayopatiwa ni yale yatakayowapa changamoto na fursa nzuri za kutumia taaluma zao.

JIUNGE NA JWTZ UJIFUNZE MENGI, UONE MENGI NA UFAIDI MENGI
Vipi waliopata kwenda na kufanya usaili walishaitwa ??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom