Nafasi za kazi-jeshi la polisi tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nafasi za kazi-jeshi la polisi tanzania

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by mwankuga, Jan 7, 2011.

 1. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Ajira
  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  JESHI LA POLISI TANZANIA


  TANGAZO LA AJIRA

  Jeshi la Polisi Tanzania linatangaza nafasi za ajira ya kazi ya Polisi kwa waombaji wenye sifa kama ifuatavyo:-

  SIFA /VIGEZO VYA JUMLA:
  (a) Muombaji awe Mtanzania kwa kuzaliwa.
  (b) Awe na afya njema iliyothibitishwa na Daktari wa Serikali.
  (c) Awe hajaoa/kuolewa
  (d) Awe na tabia njema na asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
  (e) Awe tayari kufanya kazi mahali popote ndani na nje ya
  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  A. Kwa waombaji wenye elimu ya kidato cha nne:
  - Awe amemaliza kidato cha nne kati ya mwaka 2008 na 2010
  na kufaulu angalau kwa kiwango cha daraja la nne, Pointi 28.
  - Awe na umri kati ya miaka 18 na 25.

  B. Kwa waombaji wenye elimu ya kidato cha sita:
  - Awe amemaliza Kidato cha sita kati ya
  mwaka 2008 na 2009 na kufaulu.
  - Awe na umri kati ya miaka 18 na 25.

  Waombaji wa kundi A na B wenye sifa zilizoainishwa hapo
  juu wanatakiwa kupeleka maombi yao kwa njia ya barua
  kwa Wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) katika Wilaya wanazoishi.

  C.Kwa waombaji wenye ujuzi/utaalamu.

  (1) Mafundi Pikipiki (nafasi 23).

  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu waombaji wawe na:-
  (a) Elimu ya Kidato cha IV/VI pamoja na Cheti cha Trade
  Test grade I - III kilichotolewa na VETA au na chuo
  kingine kinachotambuliwa na VETA.
  (b) Umri usiozidi miaka 25.
  (c) Waombaji wawe wamefanya kazi kwa vitendo walau
  kwa muda usiopungua mwaka mmoja.

  Waombaji watume maombi yao kwa:
  Mkuu wa Kikosi cha Matengenezo ya Magari,
  S.L.P. 9141,
  DARES SALAAM.

  (2) Wataalamu wa Afya:

  (a)(i) Maafisa Tabibu (nafasi 10).
  (ii) Tabibu meno – Dent Therapists’ (nafasi 2).
  (iii) Mtaalamu wa dawa ya usingizi Anaesthesia (nafasi 1).
  (iv) Maafisa Uuguzi – (nafasi 4).
  (v) Wafamasia wasaidizi – (nafasi 5).

  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu waombaji wawe na:-
  (a) Elimu ya Stashahada katika fani hizo.
  (b) Umri usiozidi miaka 25.

  (b) (i) Fundi Sanifu maabara – Lab Tech. (nafasi 5)
  (ii) Wauguzi – Enrolled Nurses (nafasi 2)
  (iii) Wauguzi Wasaidizi/Wahudumu wa Afya (nafasi 8)

  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu waombaji wawe na:
  (a) Elimu ya Kidato cha IV pamoja na Vyeti katika fani
  hizo na uzoefu katika huduma za Hospitali.
  (b) Umri usiozidi miaka 25.

  Waombaji watume maombi yao kwa:
  Mkuu wa Polisi,
  Kikosi cha Afya,
  S.L.P 9791,
  DAR ES SALAAM.

  (3) Wataalam wa muziki (Brass Band/Jazz Band) (nafasi 28).

  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu waombaji
  wawe na:-
  (a) Elimu ya Kidato cha IV/VI
  (b) Umri usiozidi miaka 25.
  (c) Vyeti vya kufaulu katika fani ya muziki vilivyotolewa na vyuo
  vya sanaa vinavyotambuliwa na Baraza la Sanaa laTaifa (BASATA)

  Waombaji watume maombi yao kwa:
  Mkuu wa Polisi,
  Kikosi cha Bendi,
  S.L.P.63194,
  DAR ES SALAAM.

  (4) Mafundi Ushonaji:- (nafasi 27)

  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu, waombaji
  wawe na:
  (a) Elimu ya kidato cha IV pamoja na cheti cha ujuzi katika fani hiyo kutoka VETA au Vyuo vinavyotambuliwa na VETA.
  (b) Umri usiozidi miaka 25.
  (c) Uzoefu wa angalau mwaka mmoja katika fani hiyo.

  Waombaji watume maombi yao kwa:
  Mkuu wa Kikosi,
  Ghala Kuu la Polisi
  S.L.P 2228,
  DAR ES SALAAM.
  (5) Wanamaji:
  (i) Manahodha (nafasi 5).
  (ii) Mafundi Meli (nafasi 5).

  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu waombaji
  wawe na:
  (a) Elimu ya kidato cha IV/VI
  (b) Stashahada ya fani hizo kutoka Chuo cha Wanamaji (DMI).
  (c) Umri usiozidi miaka 25.

  (iii) Wazamiaji: (nafasi 10)
  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu waombaji
  wawe na:
  (a) Elimu ya Kidato cha IV.
  (b) Uzoefu katika fani hiyo.
  (c) Umri usiozidi miaka 25.

  (iv) Mafundi Rangi za Meli (nafasi 10)
  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu waombaji
  wawe na:
  (a) Elimu ya Kidato cha IV.
  (b) Cheti kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na VETA.
  (c) Umri usiozidi miaka 25.

  Waombaji watume maombi yao kwa:
  Mkuu wa Polisi,
  Kikosi cha Wanamaji,
  S.L.P, 3010,
  DAR ES SALAAM.

  (6) Wataalam wa masuala ya Jamii (Social Workers- nafasi 150).
  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu waombaji
  wawe na:
  (a).Elimu ya Kidato cha IV na kuendelea.
  (b).Stashahada/Vyeti kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa
  na Serikali katika fani za:
  - Maendeleo ya Jamii (Community Development)
  -Kazi za Jamii (Social works)
  -Sayansi ya Jamii (Social Science/Sociology).
  (c) Umri usiozidi miaka 25.

  Waombaji watume maombi yao kwa:
  Inspekta Jenerali wa Polisi,
  Makao Makuu ya Polisi,
  S.L.P 9141,
  DAR ES SALAAM.

  (7) Waombaji Wenye Elimu ya Vyuo Vikuu/Vyuo vya elimu ya juu katika fani za:-
  (i) Sosholojia (nafasi 20).
  (ii) Menejimenti ya raslimali watu (nafasi 20)
  (iii) Sheria (nafasi 15)
  (iv)Washauri nasihi (Counsellors) (nafasi 25)
  (v)Utawala katika utumishi wa Umma (Public Admin). (nafasi 20)
  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu waombaji
  wawe na:-
  (a) Shahada/Stashahada ya juu katika fani hizo.
  (b) Umri usiozidi miaka 27.

  Waombaji watume maombi yao kwa:
  Inspekta Jenerali wa Polisi,
  Makao Makuu ya Polisi,
  S.L.P 9141
  DAR ES SALAAM.


  NB:Jinsi ya Kuomba:
  (1) Kila mwombaji anatakiwa aandike barua na kuambatanisha vivuli vya vyeti vyake vya kuhitimu shule (Leaving Certificates) vyeti vya kufaulu (Academic Certificates), cheti cha kuzaliwa
  (Birth Certificate), na picha tatu za passport size za rangi.
  Hati ya kiapo (affidavit) haitakubaliwa.
  (2) Kila mwombaji anatakiwa awe na wadhamini wawili wanaomfahamu vyema na awaorodheshe majina yao, anuani na mahusiano yao na mwombaji.
  (3)Maombi yawasilishwe kuanzia tarehe 27 Desemba, 2010 kwa anuani zilizoorodheshwa hapo juu.

  Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15 Februari, 2011.
  (N.I. MASHAYO – DCP)
  Kny: INSPEKTA JENERALI WA POLISI
   
 2. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Polisi wanaua watu?!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  No wonder reasoning capacity ya polisi wote hata Said Mwema mwenyewe ni sifuri,
  siku hizi point 28 hata kuchukuliwa chuo cha ualimu ni hatihati, kwa police bado ni hot qualification???
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,482
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Mbona ya MWEMA na ANDENDENYE hazijatangazwa?
   
 5. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Sifa nyingine uwe tayari kuipigania ccm mahali popote utakapokuwa katika jamhurin ya muungano wa TZ
   
 6. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  police wanauwa hakuna haja ya kuapply
   
 7. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Duh, nashukuru sana,yaweza kuwa suluhisho la tatizo langu sugu la kazi....wish me well my friends!nikabadili mwelekeo huko..........LOL
   
 8. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Duh,naomba anayejua aniambie hivi hapa lugha inayotumika kwenye maombi na Cv ni kiswahili au kiingereza??nisijeharibu tokea mwanzo?
   
 9. T

  Think Tank JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 234
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pointi 28!!Sifa mojawapo.....!Ok wacha vijana wapate ajira ya kuzuia mabadiliko,wakati wameshindwa kulinda raia na mali zao kama majukumu ya kazi yao inavyoanishwa.Polisi acheni kufanya kazi kama maroboti that is my ushauri to you guys.U can take it or leave it.
   
 10. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Most of CV zinakuwa kwa kizungu
   
Loading...