Nafasi za kazi Halmashauri ya Wilaya ya Iramba

Jamii Opportunities

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
4,405
1,382
NAFASI ZA KAZI MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRAMBA ANAKARIBISHA MAOMBI YA KAZI KWA WANANCHI

MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III NAFASI 8


Sifa za mwombaji.
Mwenye elimu ya kidato cha nne (IV) au sita aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo. Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii na Sanyansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

Kazi na majukumu
  • Afisa masuuli na mtendaji Mkuu wa Serikali za Kijiji​
  • Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa Utawala bora katika Kijiji.​
  • Katibu wa Mikutano na kamati za Halmashauri ya Kijiji  Kutafsiri na kusimamia sera, Sheria na taratibu.​
  • Kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na kuongeza uzalishaji mali.​
  • Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya Kitaalam katika Kijiji​
  • Kusimamia kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji.​
  • Mwenyekiti wa Kikao cha wataalamu waliopo katika Kijiji​
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi​
  • Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji.​
  • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.​
MAELEKEZO
  1. Waombaji wote wawe raia wa Tanzania ambao hawazidi umri zaidi ya miaka 45 na hawapungui umri wa miaka 18,
  2. Waombaji wote lazima waambatanishe wasifu binafsi (CV) zenye mawasiliano ya uhakika, anuani, barua pepe na namba za simu.
  3. Waombaji wote waombe kwa kufuata masharti ya TANGAZO LA KAZI,
  4. Waombaji lazima waambatanishe nakala za vyeti vifuatavyo:-
    • Astashahada/Cheti cha Utaalamu kulingana na sifa za nafasi husika
    • Cheti cha mtihani wa kidao cha nne au sita,
    • Cheti cha kuzaliwa.
    • Picha moja ya Passport size
  5. Hati ya matokeo ya kidato cha nne (Result slip) haitafanyiwa kazi.
  6. “Transcript” ambayo haikuambatanishwa na cheti haitafanyiwa kazi.
  7. Kuwasilisha vyeti vya kughushi na maelezo mengine itasababisha kuchukuliwa hatua za kisheria.
  8. Watumishi wa Umma walioajiriwa wapitishe maombi yao kwa waajiri wao
  9. Waombaji ambao walistaafu kazi kwa sababu yoyote ile hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi.
  10. Waombaji waonyeshe wadhamini wawili na mawasiliano yao, anuani na namba za simu.
  11. Waombaji wenye vyeti vya kidato cha nne na cheti cha Taaluma ambavyo vimepatikana nje ya nchi wahakikishe vimehakikiwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Baraza la Elimu ya ufundi la Taifa (NACTE).
  12. Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au kiingereza.
  13. Kwa waombaji wenye vyeti vya ngazi ya NTA level 4 Basic Technician Certificate” (NTA Level 4) maombi yao hayatafanyiwa kazi. Kwasasa cheti kinachopokelewa ni “Technician Certificate” (NTA level 5) na kuendelea
  14. Watakaochaguliwa kufanya usaili watajulishwa tarehe ya usaili kupitia tovuti ya Halmashauri – www.irambadc.go.tz na kwenye mbao za matangazo za Halmashauri
  15. Watakaoitwa kwenye usaili watajigharamia wenyewe.

Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 17/09/2020 saa 9:30 Alasiri, baada ya tarehe hiyo kupita maombi hayatapokelewa.
Tangazo hili pia linapatikana kwenye tovuti ya Halmashauri na Sekretarieti ya Ajira.
Barua zote zitumwe kwa :-

Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Iramba,
S.L.P. 155,
KIOMBOI/IRAMBA.


Simu Na. 026 2532253
Fax Na. 026 2532253
E – mail: ded.irambadc@singida.go.tz

Linno P. Mwageni

MKURUGENZI MTENDAJI WILAYA
 
Hizi kazi za halmashauri hasa hizi za watendaji nyingi huwa ni geresha tu, makada tayari washazichukua zamani sana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom