Nafasi za Kazi 25 JamiiForums - mwisho wa kutuma maombi ni Julai 27, 2019

Kudo,

Kazi zetu lugha za msingi ni mbili (Kiswahili na Kiingereza). Tumekuwa tukiajiri watendaji bila kujalisha Kiingereza chao ni fasaha, na imekuwa ikiwapa shida katika uwasilishaji wa kazi zao inapotakiwa iwe kwa Kiingereza. Hilo limepelekea, wale ambao wanajua kuwasaidia hivyo kumaanisha mtu mwingine anamfanyia kazi. It is NOT productive.

Hivyo kujua Kiingereza ni moja ya Hitaji mhimu maana tunafanya maandiko na research nyingi tukishirikiana na nchi jirani na za kimataifa. Kiswahili pekee haitoshi.

Muombaji akisoma akashindwa kuelewa tangazo tokana na lugha, tunashauri asiombe. Aache tu.
Nnachotaka kuwashauri ni jamobo moja,

SASA HIVI JF INAPIGWA VITA NA WATAWALA, kuweni makini mnapoajiri maana mtaishia kuajiri mashushushu JF ikafa!!

Narudia tena kuweni makini!!
 
Hizi kazi lazima mtu akae ofisini au anaweza fanyia mahali popote alipo? Maana sijaona hili swali likijibiwa
 
Kudo,

Kazi zetu lugha za msingi ni mbili (Kiswahili na Kiingereza). Tumekuwa tukiajiri watendaji bila kujalisha Kiingereza chao ni fasaha, na imekuwa ikiwapa shida katika uwasilishaji wa kazi zao inapotakiwa iwe kwa Kiingereza. Hilo limepelekea, wale ambao wanajua kuwasaidia hivyo kumaanisha mtu mwingine anamfanyia kazi. It is NOT productive.

Hivyo kujua Kiingereza ni moja ya Hitaji mhimu maana tunafanya maandiko na research nyingi tukishirikiana na nchi jirani na za kimataifa. Kiswahili pekee haitoshi.

Muombaji akisoma akashindwa kuelewa tangazo tokana na lugha, tunashauri asiombe. Aache tu.
Ni kazi inayohitaji mtu akae ofisin au anaweza fanyia mahali popote alipo?
 
Hakunaga nafasi ya Ban Engineer?iwekeni jamani nimesomea kupiga watu Ban hukoo Bangladeshi.
 
Habari zenu humu ndani, naomba msaada kwa anaejua tuition fees kwa course za Masters hasa ya MBA pale Open University of Tanzania mana nmehangaika kugooglr nmeshindwa.
 
Ni bora haya matangazo mkayweka kwenye forums za UK ama USA, kisha mkaajiri wazungu.

Lakini ni upotofu, matangazo yote kutumia lugha ya kigeni, wakati wanaosoma hayo matangazo si wote wanaojua hiyo lugha.

Vipi kama kuna mtu anandugu yake, ila yeye haijui lugha iliotumika, huoni atashindwa kumpa taarifa ya tangazo la kazi?

Kibaya zaidi, mnaandika kinge, usaili mnatumia kiswahili, ofisini wanabonga kiswahili.

Mwenye sifa za kuajiriwa akisoma kiswahili, hawezi shindwa fanya kazi.
Kwa nini kwa Kiswahili mkuu.Mimi naamini kufanya kazi JF kunahitaji Kingereza.Kama wewe ni kati ya wale wanaosema Kiingereza sio muhimu jikalie pembeni wakwetu.Siunajua JF zipo forums za Kimombo.
 
Kama unahusudu kingereza, na umejibu kiswahili, na bado hujanielewa nilivyonadika, sasa kuna umuhimu gani wa kutumia kingereza na kukihusudu wakati lugha Mama yako huilewi?

Mkuu, ni kweli hujaelewa nilichoandika? Au hujaelewa lengo la komenti yangu?

Nikusaidie basi.....

Lengo la komenti yangu ni kwa wale wasiojua kingereza na wanao ndugu, au watoto wao wenye kuhitaji ajira na wanasifa zinazohitajika.

Kwa kingereza, ina maana vijana wale ambao hawajafanikiwa kusoma tangazo hili, watakuwa wamekosa kujaribu bahati zao.

Sasa kushindwa kunielewa kwa kiswahili, hicho kingereza ndo utaelewa?
 
Mm.
 
Ajira zimekaa kibaguz sana kwa sisi tusiojua kizungu
Hakuna ubaguzi wowote ulitaka waajiri wasiojua kiingereza ilihali majukum yao yanahusisha kusoma na kuelewa post zilizoandikwa kiingereza?
hakuna kazi isiyo na vigezo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom