SoC01 Nafasi za biashara zipo nyingi lakini tumeshindwa kufungua macho na kuziona

Stories of Change - 2021 Competition

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,587
215,182
Katika mawazo ya biashara ya kufanya, weka mawazo yako katika kutoa huduma katika jamii inayokuzunguka. Mawazo yako yakijikita hapa ni rahisi kugundua kitu kinachohitajika sana katika jamii yako. Fikiria jinsi utakavyozalisha kwa wingi bidhaa ile itakavyo okoa maisha au usumbufu katika jamii.

Mfano mdogo ni soko la vitafunwa, wengi wanawaza kitafunwa kikubwa ni mikate. Bakery za mikate zipo karibu kila mkoa. Lakini mtaani watu wananunua pia chapati, maandazi, sambusa, vitumbua nk.

Bakhresa ameweza kufungua bakery ya vitafunwa lakini bado hajakidhi hata soko la Dar peke yake. Bado kuna watu wengi wanaishi kwa kupika na kuuza vitafunwa mtaani. Unaweza kufungua bakery ya chapati na vitumbua, kwa kwa kutumia mashine ukazalisha vitumbua na chapati kwa wingi na kwauzia wachuuzi zikiwa zimegandishwa.Wachuuzi wataokoa muda wa kuandaa wakinunua kutoka kwako.

Chapati ilikandwa inaweza kuhifadhiwa kabla haijachomwa. Na hata ikikaa mwaka mmoja kwenye freezer inapochomwa inakua na ladha bora. Vitumbua vinahifadhiwa kwenye baridi na kutokewa masaa 12 kabla ya kumfikia mteja.

Ukijitangaza na wafanya biashara wakijua kuwa katika kila chapati anayonunia kwako anawezawkutengeneza shikingi mia au miambili bila adha ya kununua unga, mafuta na muda wa kuandaa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom