Nafasi za ajira

baba afrika

Member
Dec 11, 2015
86
125
J& k company limited.
YAH:USAJILI WA MWANZO WA WANAKAMPUNI PAMOJA NA UTAMBULISHO WA KAMPUNI.
Mambo vipi wadau.kichwa cha habari hapo juu chausika.dhumuni ya andiko hili ni kuitambulisha kampuni mpya ya j&k company limited pamoja na kufanya usajili wa awali wa wadau wa kampuni hiyo.andiko hili litagawanyika ktk sehemu kadhaa kama utambulisho pamoja na historia ya kampuni,malengo ya kampuni,usajili wa wanachama wa mwanzo wa kampuni na maelezo juu ya miradi itakayofanywa na kampuni.
1.HISTORIA YA KAMPUNI.
Kampuni hii itaitwa j& k company limited.JK ni code au neno la siri ambalo hutumika na watawala au watu wengi wenye mafanikio duniani hususan ni Afrika ya mashariki.mfano julius kambarage,jommo Kenyatta,joseph kusaga,john kenedy,jakaya kikwete na wengine wengi ambao nikitaka kuwataja basi nafasi haitotosha.so j&k haina maana yoyote bali ni code ya great people duniani so nimeamua kuiita ivyo ili kusadifu vission na mission za kampuni.kampuni hii imeanzishwa na Joseph leonard haule( gotta) na inatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi wa nane mwaka huu.
2.MALENGO YA KAMPUNI.
kampuni hii itajiusisha na mambo ya mitandao kwa asilimia 80 na mambo yasiyo ya kimtandao kwa asilimia 20.kampuni itakuwa ni moja ila yenye kufanya shughuli tofauti tofauti huku msingi mkuu ukiwa ni ubunifu,smart work,innovation,transparency,utekelezaji na maelewano.
Kampuni itaanza project( miradi) 3 kwa kuanzia huku mradi wa 1 na 2 ndo itakayopewa kipaumbele wakati mradi wa tatu hautaguswa kabisa mbaka wakati muafaka utakapofika.
MRADI WA 1.
mradi wa kwanza utakuwa ni kubadili tasnia ya burudani,habari na utalii Tanzania kwa kuintroduce vitu ambavyo havijawai kufanyika katika tasnia izo au kuviboresha vilivyopo katika namna ambayo ni very convicing( yenye ushawishi wa hali ya juu). katika kufanikisha mradi huo wa kwanza itatakiwa itengenezwe mtandao wa kijamii ( social network) ambao utaweza kufanya hayo mambo yote kwa pamoja na kuhakikisha Mtandao huo mpya utaua mitandao maarufu kama facebook na instagram ili kufanikisha malengo ya kampuni kwani matumizi ya mitandao hiyo ya fb na instagram itatishia uhai wa mradi wetu wa kwanza.mbaka muda huu tayari zishapatikana mbinu zitakazotumika kuua mitandao iyo ya fb na instagram but mbinu izo bado ni siri ya wataalamu wa kampuni hii na wadau watakao fanikiwa kusajiliwa watazipata katika kikao cha kwanza cha kampuni.so kukamilika kwa mradi wa kwanza ndo kutafungua njia ya kuanzishwa kwa mradi wa pili ambao hapa sitouzungumzia hadi kwenye kikao cha kwanza cha kampuni.
Jinsi gani tutaweza kubadili tasnia izo tajwa hapo juu kwa kutumia mtandao wa kijamii nayo itaelezwa katika kikao cha kwanza mana hapa najaribu tu kufupisha ili watu wapate idea ya kampuni hii.
MEMBER WA KAMPUNI.
Kimsingi kampuni hii itadili na watu wa rika tofauti tofauti ila asilimia 99 itakuwa ni vijana.kampuni inaamini katika uwezo wa vijana katika ubunifu,utendakazi na maelewano na ndo sababu kampuni hii imeamua kuwa na MEMBER vijawa as much as it can.sifa za kujiunga ni utayari wa mtu kutumia muda wake,akili yake Na nguvu zake ili kufanikisa malengo ya kampuni hii.ubunifu na utekelezaji ndo utakuwa uti wa mgongo wa kampuni hii so kama unaona unaweza kufanya hayo basi unakaribishwa katika kampuni hii( familia hii)
MAZINGIRA YA UFANYAJI WA KAZI.
since kampuni itadeal na vijana kwa sana basi kampuni hii itafuata rabita ya mfanyakazi husika ambayo mtu husika ataitoa ili kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji kazi.ufanyaji kazi hautaathiri shughuli nyingine za mfanyakazi unless kama kuna hali ya dharura.kwa kusema ivo ninamaa ya kuwa watu wataweza kufanya kazi bila hata ya kuja ofisini na mambo yakaenda.
Natumaini nimejitaidi kufupisha kadri nilivoweza bila kuwachanganya watu.
Nategemea maswali sasa.karibunii
By Joseph haule ( gota)
The master plan and game changer aka ceo of this company.
0625 58 21 09
 
Jul 19, 2016
25
45
Great idea bro...nilishawah kufkiria mapungufu mengi tuliyonayo katika sekta hizo hususan ya utalii..

since tumegraduate advance level mwaka jana,hatukua na broad idea rather than creation of NGO'S ambyo itadili na utalii hususan kutangaza rasilimali tulizo nazo.tulihis kama ndo njia sahihi sababu hatukua na idea wala fund ya kufanya tunachotaka..futherwhile tukashindwa kufikia malengo na mpango ukafa

Still kile kitu kiko moyon kuus utalii...nw niko bachelor of taxation fst year,

Kama una base nzuri bro mapunguf yalioko katika utangazaji wa rasilimali zetu+utajiri tulionao unaweza tumia fursa

nimejarbu kufatilia,kila siku utaskia tanzania ndo nchi pekeee duniani yenye....but we r reluctant to reach wherw we deserve

Dont give up najiona ulipo na unapotaka kufika baada ya 2yrz
 

kabon14

JF-Expert Member
Jun 14, 2016
1,226
2,000
Fungua group whatsapp kwa semina zaid,maana umefpisha maelezo kna vtu vng vya kuuliza
 

0909Hekima

JF-Expert Member
Feb 23, 2013
229
225
Umebase wapi zaidi!? Yaani upo mkoa gani kwa sasa?

Unahitaji watu wa aina gani?

Elimu yao, utaalamu wao na mengine yanayoendana na uhitajio wa hizo kazi achilia mbali ujana!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom