Habarini wanajamvi
Niko kwenye ndoa ni mwaka wa nane sasa, mume wangu ni mature person wa miaka 35, ila kuna tabia moja anayonikera nayo mno ya kutumia muda wote baada ya kazi kwenye mitandao ya kijamii ifuatayo whatsup, facebook, youtube na JF anajisahau humo
Sio asubuhi sio usiku wa manane yupo tu na kabla hajakolea kwenye tabia hii alikuwa na mchepuko tabia ya wakati huo ikawa ni safari nyingi za kikazi nikamfuma akaahidi kuacha lakini ndo kabadilika sasa yuko bize kwenye mitandao.
Najisikia mpweke kweli kwa kuwa nakosa attention yake kabisa au sijui ndo nimeshindwa kufill pengo la mchepuko na mitandao imeweza, nimemueleza kwa upole mara kwa mara naona hana mpango wa kubadili msimamo na kibaya nikichat nae mimi hajibu hata hiyo text, naombeni ushauri wadau.