Carnivora
JF-Expert Member
- Jan 26, 2018
- 3,651
- 5,987
Habari wakuu
Katika jamii zetu za Kitanzania ni jambo la kawaida kusikia bint anapotaka kuolewa wajomba wake lazima wahusike kwa namna moja ama nyingine. Sote tunafahamu wajomba ni kaka wa mama wa mtoto anayetaka kuolewa hivyo kama ndugu wa karibu wana haki ya kujulishwa kinachoendelea. Kila jamii ina taratibu zake, hivyo uzito wa mambo hayo pia hutofautiana toka jamii moja ama nyingine. Kuna jamii nyingine mpaka wajomba nao wanahusika kupanga mahari.
Hali huwa mbaya zaidi kwa baadhi ya jamii ikiwa wajomba wataona hawajatendewa haki kwa namna moja ama nyingine. Wanaweza kupinga ama kususia mahari/harusi kabisa ya mtoto wa dada yao. Hivi mjomba ana nafasi gani katika bint anayeolewa wakati huyo mtoto si wa ukoo wao? Ni mtoto wa ukoo mwingine kazaliwa kwa dada yao. As long as dada yao ( mama wa bint) yupo, na hata kama hayuko hai wao kwanini wanaulazima watie neno ama kudai fungu la mahari? Wana haki gani? Unakuta hata hawajahusika kwa namna yoyote ile katika malezi ya huyo mwolewaji.
Ni mila tu za kizamani au ni utaratibu upi? Mi sielewi. Ifike mahali tuache kuishi kwa mazoea....wajomba, wajomba eeeh wana mamlaka gani? Kwanini wasiwe baba wadogo/wakubwa, mashangazi ambao wanaweza kusema mtoto wa kaka yao (ukoo wao)?
Yaani mimi Mgunya nimeoa mchaga tukazaa bint. Siku posa imekuja wachaga wanasimama dede kwenye posa....hivi huyu mtoto ni wa kwao? Si wanasema mtu akiolewa anahamia huko kwa mumewe....sasa nyinyi wajomba mnadai nini huku?
Katika dini ya Kiislam, mwenye mamlaka ya kuozesha ama kukataa kuozesha ni baba(kama yupo hai) wa bint. Mjomba hana haki yoyote na wala hausiki kukubali posa wala kuwakubalia waleta posa na kuwafungisha ndoa. Akatae, akubali, aridhike/asiridhike habatilishi uhalali wa ndoa kwa namna yoyote ile. Kwa maana nyingine mjomba ni mtu wa kupewa taarifa tu kuwa mpwa wako anaolewa.
Je, haya mambo ya wajomba kwa upande wa jamii yako yakoje na yapi maelekezo ya dini?
Kama sina elimu nipewe. Msinikashifu.