Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
Chenge na Uspika
Suala la Bwana Andrew Chenge kugombea uspika limezua mjadala maeneo mbalimbali kama ilivyokuwa wakati kashfa ya radar ilipowekwa adharani (na kashfa nyingine zilizoibuka) na vile vile mijadala mbalimbali inayohusiana na kesi yake ya kuendesha gari lwa uzembe na bila kuwa na bima halali!
Hivyo si jambo geni kusikia mjadala unaomuhusu Bwana Chenge. Swali la kujiuliza kwanini ajadiliwe?
Kwa wengine hakuna sababu ya Bwana Chenge kujadiliwa. Ni haki yake ya kikatiba kugombea nafasi ya uspika! ni msomi na ni kiongozi! pia sheria iko hivi 'innocent until proven guilty na siyo 'guilty until proven innocent'.
Kwa wengine lazima ajadiliwe kwa sababu hafai! ana kesi mahakamani, hajawahi kutoa maelezo ya kuridhisha kuhusu kuhusika kwake kwenye kashfa ya radar na mikataba mingine ambayo imeisabishia serikali na nchi yetu hasara kubwa. Kama kiongozi mwenye nia ya kuongoza ni lazima angetoa maelezo kuhusu hayo yote kabla hajafikiria kuomba ridhaa ya kuongoza chombo muhimu kama bunge!!
kwangu mimi huyu Bwana Chenge lazima ajadiliwe. Lazima wadau wapate nafasi ya kutoa ma-dukuduku yao waliyonayo moyoni. Si sahihi kuruhusu hii hali iendelee ya baadhi ya viongozi kutokuwa na chembe ya aibu wala woga wa mawazo ya watu!
Hata kama yeye ni safi na hana makosa watanzania wana haki ya kujua hivyo kabla hajathubutu kugombea nafasi yoyote ya uongozi! Busara ni yeye kukaa pembeni na kuruhusu ukweli ujulikane kabla ya kurudi kwa wananchi kuomba uongozi! hii imeonekana huko Kenya kwa waziri wa mambo ya nje na katibu wake kujiuzulu siku za karibuni.
Kwa kukaa pembeni haimaanishie wewe ni mkosaji ila inaonyesha heshima uliyonayo kwa taratibu na maadili ya kiungozi. Inathibitisha uwezo na busara zako kama kiongozi!
Kwa jeuri ya kuamua kuogombea kwa kisingizio ni 'haki ya kikatiba' na 'innocent until proven guilty' ni wazi busara na heshima ya Bwana Chenge ni vitu vya kuhojiwa! Ni mtu wa aina gani huyu? Hana aibu! hana soni! hana haya!
Kwani angekaa pembeni na kujisafisha angepoteza nini? au kwa sababu hata raisi wa nchi hajasema lolote na ameendelea kukaa kimya basi anaweza kufanya na kuamua chochote? auu kwa sababu raisi alimnyanyua mkono wakati wa kampeni ameafikia mahali ameona anastahili kuwa spika na kuliongoza bunge!
Ni wapi tunakoelekea au tunakopelekwa? Kwa njia nyingine naamini inaweza kuwa ni a 'blessing in disguise' haya yote yanatokea! Mungu ameamua kutuonyesha njia za kujikwamua kutoka kwenye uongozi mbovu tulionao!
Kama raisi wa marekani alipigiwa kelele kwa kuchelewa 'kufanya maamuzi' wakati wa suala la kuvuja kwa mafuta - BP na bado anaendelea kupigiwa kelele kuhusu mambo mengine ambayo hata hakusababisha yeye, kwa nini huyu Bwana Chenge aipigiwe kelele na kufunzwa adabu kwa yote aliyoyafanya au aliyoshindwa kufanya? badala yake tunamwacha achezee karatasi zilizotengenezwa kwa fedha za wavuja jasho kujaza eti anataka kuwa spika!! amuongoze nani? kwa heshima ipi watakayompa?