Nafasi ya mgombea mwenza wa Rais, mwanamama Samia Suluhu

Mugisher

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
411
360
Katika chaguzi zote zilizopita ni wazi kuwa wanawake/wakinamama ndio wapigaji kura wakubwa na wenye uhakika na kura zao. Kote mijini na vijijini hili ni kundi la wapigakura ambalo huwezi kulifumbia macho hata kidogo. Kwa takwimu wanawake ndio wapigaki kura wengi kuliko makundi mengine. Hii ni fact wandugu. Sasa je kwaCCM kumchagua mwanamama kuwa mgombea mwenza hii inamaana gani kwenye ile pattern (mtiririko) ya upigaji kura Tanzania?

Kwa maoni yangu naona ya kuwa wakinamama wengi watampigia kura mwanamama mwenzao kwa kuona kuwa kwa mara ya kwanza kwa Taifa letu mwanamama atakuwa makamu wa Rais pengine na Rais baadaye. Hii haijawahi kutokea na naona kuwa itakuwa kete kubwa na muhimum kwenye uchaguzi wa mwaka huu na huenda ikamua mshindi ‘asubuhi na mapema’. Wenzangu mnalionaje hili?
 
Wewe una mawazo mgando. Halafu hujui historia vizuri. Mwaka 2005 mwanamke wa kwanza aitwaye Anna Senkoro aligombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mbona wanawake hawakumpa kura? Kama ni hivyo kwa nini CCM wasingeacha mwanamke awe ndiye Rais? Hawo wanawake sasa hivi wanagawanyika na wala sio kweli kuwa wengi au wote watampigia kura kwa kuwa ni mwanamke
 
Hayo mawazo yako ni mgando sana, kiuhalisia kwanza kabisa wanawake wengi hawapendani na hawako tayari kuona mwanamke mwenzao anawaongoza kwani kama hoja yako ingekuwa sawa tumeshuhudia wanawake wengi wanaangushwa katika chaguzi nyingi za Ubunge, Udiwani NK huku maeneo hayo yakiwa na wanawake wengi. kwa walichokifanya CCM kumuweka huyo Samia wamechemka kwani na watalijutia hilo kosa lao hapo baadae kwani hana nguvu ya kusimama pekeyake latika kampeni na wananchi wakamkubali tutatachokishuhudia atazomewa.
 
Kama ni hivyo kwanini basi hawakumteua Mwanamke kuwa mgombea urais?
Kwanini uanamke utumike kama ngazi za mwanaume kupata madaraka?

Ukichunguza vizuri utagundua kuwa zaidi ya 40% ya wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM walikuwa wanawake, lakini jumla ya kura zote walizopigiwa wagombea wanawake(Amina na Migiro) ndani ya mkutano mkuu zilikuwa 12% . Sasa kwa mwendo huo inadhihirisha kabisa hata wanawake wa CCM wenyewe hawapendi kabisa kuwa na kiongozi mwanamke.
 
Wewe una mawazo mgando. Halafu hujui historia vizuri. Mwaka 1995 mwanamke wa kwanza aitwaye Anthony Komu aligombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mbona wanawake hawakumpa kura? Kama ni hivyo kwa nini CCM wasingeacha mwanamke awe ndiye Rais? Hawo wanawake sasa hivi wanagawanyika na wala sio kweli kuwa wengi au wote watampigia kura kwa kuwa ni mwanamke

Na hata 2005 Dr. Anna Senkoro aligombea urais, na still wanawake hawakumpigia kura....

Ninachokiona hapa ni uwezo mdogo sana wa Samia Suluhu ukilinganisha na mgombea mwenza wa Ukawa Dr. Duni Haji
 
Katika chaguzi zote zilizopita ni wazi kuwa wanawake/wakinamama ndio wapigaji kura wakubwa na wenye uhakika na kura zao. Kote mijini na vijijini hili ni kundi la wapigakura ambalo huwezi kulifumbia macho hata kidogo. Kwa takwimu wanawake ndio wapigaki kura wengi kuliko makundi mengine. Hii ni fact wandugu. Sasa je kwaCCM kumchagua mwanamama kuwa mgombea mwenza hii inamaana gani kwenye ile pattern (mtiririko) ya upigaji kura Tanzania?

Kwa maoni yangu naona ya kuwa wakinamama wengi watampigia kura mwanamama mwenzao kwa kuona kuwa kwa mara ya kwanza kwa Taifa letu mwanamama atakuwa makamu wa Rais pengine na Rais baadaye. Hii haijawahi kutokea na naona kuwa itakuwa kete kubwa na muhimum kwenye uchaguzi wa mwaka huu na huenda ikamua mshindi ‘asubuhi na mapema’. Wenzangu mnalionaje hili?
Hicho ndicho kigezo mojawapo cha kujiua wenyewe hawa kijani members (CCM). Uliwahisikia wapi Wamasai, Wakurya (Mara kiujumla) na wengineo huko Usukumani Wakachagua japo Mbunge tu awe mwanamke? Hata Wanyakyusa majimbo yao hayajawahi kuongozwa na wamama.
Wanawake wanatabia moja, hawawezi kumkubali mwanamke mwenzao na pia kwa mliyo ofisini nadhani mnaona adha mnayoipata endapo boss wako akiwa mwanamama.
Makinda ndiyo mfano mzuri.
Huwa naamini huwezi kupingana na Neno la Mungu, Soma Waraka wa Mtume Paulo kwa Timotheo (1Timoheo 2:12.).
 
Hayo mawazo yako ni mgando sana, kiuhalisia kwanza kabisa wanawake wengi hawapendani na hawako tayari kuona mwanamke mwenzao anawaongoza kwani kama hoja yako ingekuwa sawa tumeshuhudia wanawake wengi wanaangushwa katika chaguzi nyingi za Ubunge, Udiwani NK huku maeneo hayo yakiwa na wanawake wengi. kwa walichokifanya CCM kumuweka huyo Samia wamechemka kwani na watalijutia hilo kosa lao hapo baadae kwani hana nguvu ya kusimama pekeyake latika kampeni na wananchi wakamkubali tutatachokishuhudia atazomewa.

wewe hamnazo kweli hadi amefika kuonekana na kuchaguliwa kuwa mgombea mwenza ulikuwa unasimama nae jukwani.

endeleeni kuota ndoto yenu ya kupeleka genge la wezi ikulu.
 
Tena kama watatumia uanawake kwa ajiri ya kura za urais ndo watazidi kujichinja na kujimaliza kwa midomo yao, labda kanda ya ziwa ihamie Uganda
 
CCM i esoma alama za nyakati. Ni ngumu kwa wazee ambao ni wagonjwa( Lowasa na Duni) kuwashinda akina Magufuli na Samia ambao bado wana nguvu na ari ya kufanya kazi
 
Na hata 2005 Dr. Anna Senkoro aligombea urais, na still wanawake hawakumpigia kura....

Ninachokiona hapa ni uwezo mdogo sana wa Samia Suluhu ukilinganisha na mgombea mwenza wa Ukawa Dr. Duni Haji

Aisee tena umenikumbusha vizuri. Huyo mama ni Anna Senkoro ndiye aligombea Urais mwaka 2005. Huyu Anna Komu alikuwa mgombea mwenza na Freeman Mbowe mwaka huo huo wa 2005. Bravo!
 
Aisee tena umenikumbusha vizuri. Huyo mama ni Anna Senkoro ndiye aligombea Urais mwaka 2005. Huyu Anna Komu alikuwa mgombea mwenza na Freeman Mbowe mwaka huo huo wa 2005. Bravo!
Walikuwa wanahombea kupitia chama gani? Ina maana mwaka 2005 CHADEMA walisimamisha mgombea Urais na mgombea mwenza wote wachagga? Kweli ndo maana walipigwa mweleka
 
Kwa Taarifa yako hapo ndipo wanaweza kukosa kura za wanawake hao unaodhani wnapendana kiasi hicho
 
Walikuwa wanahombea kupitia chama gani? Ina maana mwaka 2005 CHADEMA walisimamisha mgombea Urais na mgombea mwenza wote wachagga? Kweli ndo maana walipigwa mweleka

Anna Komu ni Mzanzibari, acha ukabila wewe. Halafu leo usiende kule unakopenda kwenda. Kuna kitu
 
Tanzania ya leo sio ya jana ambayo mlikuwa mnadanganywa na kanga kama wewe ambavyo unaendelea kudanganya na peremende kama mtoto aliyeanza kusimamia viti ili a move on....
 
Samia tutakupa kura zetu,kwani lazima Kila nafasi ya juu ashike mwanaume,kipindi hiki wanawake tunajitambua,kura yangu unayo,umethubutu naamini unaweza.kina mama hoyeee
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom