NAFASI YA MGO,BEA BINAFSI AS WE APPROACH 2015:mtikila vs rep-hukumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NAFASI YA MGO,BEA BINAFSI AS WE APPROACH 2015:mtikila vs rep-hukumu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by OMEGA, Mar 19, 2012.

 1. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Hukumu ya Mahakama Kuu ya mgombea binafsi​
  KATIKA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA(OFISI YA MSAJILI MKUU YA DAR ES SALAAM)​
  ILIYOKETI DAR ES SALAAM​
  MISC. CIVIL CAUSE NO 10 YA 2005JAJI KIONGOZI MANENTO, JAJI SALUM MASSATI, JAJI THOMAS MIHAYO​
  ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,​
  CHRISTOPHER MTIKILA MLETA MAOMBI
  DHIDI YA​
  MWANASHERIA MKUU MJIBU MAOMBI
  HUKUMU​
  Tarehe ya kusikilizwa 6/2/2006
  Tarehe ya kutoa maamuzi 5/5/2006
  MASSATI, JAJI:
  Mleta Maombi, REV. CHRISTOPHER MTIKILA, ni mtu asiyetetereka. Mwaka 1993 alipeleka maombi katika Mahakama Kuu ya Tanzania iliyoketi Dodoma, akiomba pamoja na mambo mengine, tamko la mahakama kwamba raia wote wa nchi hii wanayo haki ya kugombea nafasi ya urais, ubunge na udiwani bila kulazimishwa kujiunga na chama chochote cha siasa. Mahakama Kuu ilitoa maamuzi ya kukubaliana na maombi yake. Serikali ilikata rufani kupinga maaumuzi hayo, lakini baadaye iliachana na rufani hiyo na kuandaa muswada na kuupeleka bungeni kutunga sheria inayopinga maamuzi yale ya Mahakama Kuu. Kama tutakavyoona baadaye hapa chini sheria hiyo ndiyo kiini cha maombi haya yaliyo mbele yetu leo.
  Ingeweza kufikiriwa kuwa Mleta Maombi alikuwa na nia ya kufanya hivyo mwaka 1993, kwa sababu wakati huo alikuwa akipambana akitaka kusajiliwa chama chake cha siasa, Chama cha Demokrasia (DP), kama ilivyoonyeshwa katika maombi yake ya awali.
  Alipofanikiwa kusajili chama chake cha siasa, Mleta Maombi ambaye anajitambulisha kama Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (DP) amekuja tena katika Mahakama hii akiomba amri zifuatazo:
  Tamko kwamba marekebisho ya katiba kwenye vifungu 39 na 67 vya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama vilivyoingizwa na marekebisho yaliyomo katika Sheria nambari 34 ya 1994 yanakiuka katiba.
  Tamko kwamba Mleta Maombi anayo haki ya kikatiba chini ya ibara ya 2(1) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na/au nafasi ya ubunge katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama mgombea binafsi.
  Gharama za kuendesha maombi haya mahakamani zilipwe na Mjibu Maombi.
  Gharama na nafuu zingine zozote ambazo Mahakama Hii Tukufu itaona zinastahili kutolewa kwa Mleta Maombi.
  Kiini cha malalamiko ya Mleta Maombi kipo katika aya za 7, 8 na 9 za maombi yake ambayo ni kusema: kwanza, kwamba hayo marekebisho ya katiba yanapingana na misingi ya haki za binadamu kama ilivyotamkwa katika ibara ya 21(1) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pili, kwamba hayo marekebisho ya katiba yanapingana na ibara za 9(a) na (f) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tatu, kwamba hayo marekebisho ya katiba yanapingana na ibara ya 20(4) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na nne, kwamba hayo marekebisho ya katiba yanakwenda kinyume cha mikataba ya kimataifa ya Haki za Binadamu ambayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeridhia na hivyo kuwa sehemu ya sheria zake. Kulingana na maombi haya maana halisi ya marekebisho haya ya katiba ni kwamba Mtanzania wa kawaida analazimishwa kujiunga na chama cha siasa ili aweze kushiriki katika mambo ya kiutawala serikalini ili aweze kuchaguliwa kwenye nafasi yoyote ya urais au ubunge.
  Mjibu Maombi, Mwanasheria Mkuu amepinga maombi haya. Kiini cha upinzani wake kwa maombi haya kipo katika aya ya 4 ya majibu yake akijibu maombi kama yalivyorekebishwa. Anasema hivi:
  kutungwa kwa sheria namba 34 ya 1994 kulikoelekeza marekebisho ya katiba katika vifungu vilivyotajwa ni halali, kulifanywa kisheria kwa hali ya kawaida, kwa lengo la kutimiza matakwa ya umma na siyo kinyume cha haki zozote za binadamu. Zaidi ya hayo, Mjibu Maombi anatamka kwamba hayo marekebisho ya katiba hayakumbagua mtu yeyote kwa vyovyote vile kwa sababu sheria inatumika kwa watu wote na wagombea wote wanaotaka kugombea kwenye uchaguzi."
  Kwa kifupi, kiini cha mgogoro baina ya pande mbili hizi katika maombi haya ni kama marekebisho ya katiba yaliyoingizwa na sheria nambari 34 ya 1994 yanakiuka katiba au la.
  Ingawa Mahakama haikuandaa hoja zinazobishaniwa zinazostahili kufafanuliwa na mahakama, Mleta Maombi ameziandaa na pande zore mbili zimefafanua hoja tatu zifuatazo:
  Je ni kweli vifungu husika, yaani ibara ya 39(1)(c) na 39(2) na ibara ya 67(b) na 67(2)(e) vimekiuka katiba au la?
  Je ni kweli vifungu husika vinakidhi kipimo cha uwiano (proportionality test)?
  Je ni kweli marekebisho hayo yaliyoletwa na sheria nambari 34 ya 1994 yanapingana na mikataba ya kimataifa iliyoridhiwa na
  kutunzwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
  Tunaamini kwamba hakuna ubaya wowote utakaotokea kama tukiamua shauri hili kwa kufafanua hoja zilizotolewa na Mleta Maombi hata kama siyo sisi tulioziandaa hoja hizo toka mwanzo wa kusikilizwa maombi haya ambayo kimsingi yaliendeshwa kwa maandishi. Mawakili wote walipewa nafasi kujieleza kwa mdomo na kufafanua zaidi maelezo yao waliyotoa kwa maandishi.
  Mawakili Bw Rweyongeza na Bw Mpoki walimwakilisha Mleta Maombi (Mtikila). Wanasheria wa Serikali Bw Mwaimu na Bi Ndunguru walimwakilisha Mjibu Maombi (Mwanasheria Mkuu).
  Maelezo ya Mleta Maombi ni kwamba marekebisho ya ibara za 39 na 67 yaliyoletwa na sheria nambari 34 ya 1994 yanaruhusu haki ya kugombea katika uchaguzi wa rais na ubunge kwa wagombea wa chama cha siasa tu kinyume cha misingi ya haki za binadamu kama zilivyoelezwa katika ibara ya 21(1) ya katiba, ambayo inampa raia haki ya kujiunga na wenzake, na pia ni kinyume cha ibara ya 20 (4) ya katiba inayopinga kutungwa kwa sheria zinazolazimisha watu kujiunga na chama chochote au shirika. Bw Rweyongeza na Bw Mpoki walitoa hoja kwamba vifungu hivyo ni kizuizi kwa raia wanaohitaji kugombea nafasi hizo za uongozi wa kisiasa. Wanatoa hoja kwamba vifungu hivi ni vya kibaguzi kwa sababu vinawapendelea raia ambao ni wanachama wa chama cha siasa dhidi ya wale raia ambao si wanachama wa chama cha siasa katika kugombea nafasi za uongozi wa kisiasa. Mawakili hawa wananukuu misingi kadhaa ya kisheria iliyowekwa na Jaji Lugakingira (kama alivyokuwa wakati huo) katika kesi ya REV. MTIKILA VS ATTORNEY GENERAL [1995] tlr. 31.
  Mawakili hawa wanaeleza zaidi kwamba REV. MTIKILA VS ATTORNEY GENERAL (supra) ilithibitisha haki za msingi za binadamu zilizomo kwenye katiba, na kwamba kutungwa kwa sheria namba 34 ya 1994 kulikuwa potofu na kinyume cha mambo. Walinukuu kutoka Kitabu cha SYLVIA SNOWSIS kiitwacho JUDICIAL REVIEW AND THE LAW OF THE CONSTITUTION (Universal Law Publishing Co Pot Ltd, 2[SUP]nd[/SUP] Reprint 1996, ambamo kumenukuliwa kesi za LESSEE VS DORRANCE na KEMPER VS HEWKINS.
  Wakijibu hoja ya pili kama vifungu husika vinakidhi kipimo cha uwiano (proportionality test) Rweyongeza na Mpoki wanasema, kwanza, kwamba ilikuwa juu ya Mjibu Maombi kuthibitisha kwamba sheria inayopingwa haina kasoro. Kwa msingi huu Mawakili hawa walitegemea hoja zilizotolewa katika kesi mbili za Kihindi: SAPHIR AHMED VS STATE OF UTTAR PRADESH [1954] AIR SC 729 na DEANA VS UNION [1984] 1 SCRI.
  Karibu hapa kwetu nyumbani, Mawakili hawa walinukuu hukumu ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania katika kesi ya KUKUTIA OLE PUMBUN & ANOTHER VS ATTORNEY GENERAL AND ANOTHER [1993] TLR. 159, ambapo iliamuliwa kuwa kwa sheria kukidhi kipimo cha uwiano, ni lazima ionyeshwe kuwa siyo ya kiimla iliyofikiwa bila kujali, na kwamba mapana yake ni ya lazima ili kufikia lengo la kisheria. Walihitimisha hoja hii kwamba sheria inayolalamikiwa haikukidhi kipimo cha uwiano.
  Mwisho, Bw Rweyongeza na Bw Mpoki, walitoa hoja kwamba sheria husika ilipingana na Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu (Universal Declaration of Human Rights) na Tamko la Nchi za Afrika juu ya Haki za Binadamu na Makundi ya Watu (African Charter on Human and People
  ’s Rights). Mikataba hiyo muhimu ya kimataifa lazima iwekwe maanani wakati wa kutafsiri haki za msingi za binadamu na wajibu wao. Kuthibitisha hoja hii, mawakili hawa walitegemea na kunukuu uamuzi wa Mahakamu ya Rufani ya Tanzania katika kesi ya DPP VS DAUDI PETE [1993] TLR. 22.
  Wakihitimisha hoja zao za maandishi kwenye hoja ya tatu, mawakili hawa wa Mleta Maombi walisema kwamba katika shughuli zake zote, Katiba inaitaka serikali kufuata maelekezo, misingi ya sera za nchi, na hii inajumlisha nyakati za kutunga sheria. Mawakili hawa walihitimisha kwa kuomba kuwa maombi haya na gharama zake vikubaliwe na mahakama.
  Bw Mwaimu, Mwanasheria wa Serikali Mwanadamizi na Bi Ndunguru Mwanasheria wa Serikali walitoa hoja kwa maandishi kuhusiana na hoja ya kwanza kwamba marekebisho ya katiba yalifanyika kulingana na uwezo wa Bunge wa kutunga sheria na kwamba marekebisho hayo hayakwenda kinyume cha ibara yoyote ya katiba. Kwa msimamo huu, wanasheria hawa walitegemea na kunukuu ibara ya 98 (1) & (2) ya katiba. Waliongezea kwamba msimamo huu uliungwa mkono na Jaji Lugakingira (kama alivyokuwa wakati huo) katika kesi ya REV. MTIKILA VS ATTOENEY GENERAL (supra).
  Kuhusu hoja kwamba huenda marekebisho haya yalipingana na ibara ya 21(1) ya katiba, mawakili hawa wa serikali walitoa hoja kwamba marekebisho haya yalifanywa ili kukidhi matakwa maalumu ya umma. Wanasema katika maelezo yao kuwa:
  "Kizuizi kwa wagombea binafsi katika uchaguzi mkuu na uchaguzi wa madiwani ni njia mojawapo ya kupatikana demokrasia ya uwakilishi. Kimsingi yanalenga kuanzisha na kudumisha demokrasia ya uwakilishi ambayo ndiyo sera inayofuatwa na nchi yetu, ambayo ni sera, yenye nia ya kulinda amani, utulivu, usalama na utengamano."
  Na chini zaidi mawakili hawa wa serikali wanatoa hoja kwamba:
  "msingi unaomtaka mtu anayegombea uongozi afanye hivyo kupitia chama cha siasa umelengwa kuhakikisha kwamba yeyote anayefanywa mgombea anafahamika kwa watu anaotaka kuwaongoza."
  Hizi mawakili hawa wa serikali walieleza Mahakama kuwa ndizo sababu kwa nini Bunge liliamua kuzuia wagombea binafsi.
  Ilielezwa na upande wa Mjibu Maombi kwamba swali kama kizuizi hiki kina mantiki yoyote litaamuliwa kipekee kwa kila shauri, na wakanukuu maamuzi ya Mahakama ya Kikatiba ya Afrika Kusini (SOUTH AFRICA VS MAKWANYANE) [1995] (3) S.A. 391 na katika
  S VS BHULWANA [1996] (1) S.A. 388 (CC). Walisema kwamba maoni katika mashauri hayo mawili yana ushawishi katika Mahakama zetu. Kutokana na maamuzi hayo hapo juu Bw Mwaimu na Bi Ndunguru walieleza kwamba marekebisho yale ya katiba hayakuwa mazuri kwa demokrasia ya uwakilishi tu bali pia kwa kulinganisha maslahi ya umma kwa ujumla wao.
  Wakijibu hoja ya ubaguzi, mawakili hawa wa serikali walisema kwamba marekebisho hayo yalilengwa watu wote wenye nia ya kugombea uongozi kwa sababu misingi ya usawa haitarajii kila mtu kutendewa sawa na mwingine, bali kiujumla kwamba watu wenye hadhi inayofanana watendewe mambo yanayofanana. Wakinukuu shauri jingine kutoka Afrika Kusini la PRESIDENT OF REPUBLIC OF SOUTH AFRICA VS HUGO [1997] 4 SA I CC lililonukuliwa katika kitabu cha BILL OF RIGHTS HANDBOOK mawakili hawa wa serikali walisema kwamba hata kama si hivyo wakati mwingine inawezekana kuhalalisha ubaguzi kama njia ya kipekee kama lengo ni kutekeleza matakwa ya kuwainua Wafrika (affirmative Action). Msingi huu unaitwa Msingi wa ubaguzi wa kuleta usawa (fair discrimination).
  "
  Mawakili wa serikali walisema zaidi kuwa ibara za 21(1), 39(1)(2), 67(1)(b) 2, na ibara ya 20 (4) zikisomwa pamoja, itagundulika kwamba ibara ya 21(1) haianzishi utaratibu wowote. Wakasema kwamba utaratibu wa uwezeshaji unapatikana katika sheria ya uchaguzi na kanuni zake. Kwa hiyo si sahihi kusema hakuna utaratibu wa uwezeshaji. Wakaongeza kuwa uoga kwamba ibara hizi zinaweza kutumika vibaya na kuwapa haki ya kutawala watu wachache tu na hivyo kufifisha uwezekano wa kushamiri demokrasia ya kweli katika jamii siyo jambo la kweli na haliwezi kuwa ndicho kigezo cha kutoa tamko kuwa kifungu hicho kinakiuka katiba. Wakasema kuwa kinyume cha hayo wagombea binafsi hawana hakika, na hawaaminiki na wanaweza kirahisi kabisa kukiuka madaraka yao kwa vile hawatokani na watu.
  Wanasheria hawa wa serikali wakaendelea kuchambua mashauri yaliyonukuliwa na upande wa Mleta Maombi kuhusu shauri la kipimo cha uwiano kwa vile kesi zote zilizonukuliwa zilijihusisha vifungu vya sheria, ambapo shauri la sasa linahusu katiba yenyewe ambayo ni matokeo ya matakwa ya watu.
  Kuhusu hoja ya mwisho, mawakili hawa wa serikali walisema kwamba ingawa haipingiki kuwa Tanzania ni miongoni mwa mataifa yaliyoridhia Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu na kwamba pia imeridhia Tamko la Nchi za Afrika kuhusu Haki za Binadamu na Makundi ya Watu, matamko haya yana mipaka yake. Walinukuu mfano wa ibara ya 29 (2) ya Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu, linalosema kwamba ili kutekeleza haki hizo itafuatana na mipaka ambayo itakuwa imewekwa na sheria kwa lengo la kuzipata haki hizo na kuzitambua na haki na uhuru wa watu wengine. Kwa msimamo huu, mawakili wa serikali walisema kwamba kwa vile katiba ya nchi inatetea demokrasia ya uwakilishi, marekebisho yale yalikuwa ya lazima ili kudumisha mahitaji ya tabia njema, utulivu na maslahi ya kawaida ya watu. Na kwa hiyo marekebisho yale yalikuwa na makusudio ya utekelezaji wa mikataba ya kimataifa ya Haki za Binadamu. Mwisho wa siku wanasheria wa serikali waliiomba mahakama kutupilia mbali maombi ya Mleta Maombi na kumtaka alipe gharama za shauri.
  Katika nyongeza yao, Mawakili wa Mleta Maombi Bw Rweyongeza na Bw Mpoki walisema kwamba hata kama Bunge limepewa uwezo mpana wa kurekebisha vifungu vya katiba uwezo huwa upo ndani ya mipaka iliyowekwa na ibara ya 30 (2) na 31 za katiba. Kwa msimamo huu walitegemea na kunukuu sababu zilizotolewa na Jaji Lugakingira (kama alivyokuwa wakati huo) katika shauri la REV. MTIKILA VS ATTORNEY GENERAL (supra) ambaye alinukuu mashauri ya PETER NGOMANGO VS KIWANGA AND ANOTHER [1993] TLR. 77, DPP VS DAUDI PETE [1993[ TLR 22, na MBUSHUU VS REPBLIC [1995] TLR 97. Mawakili hawa wa Mleta Maombi walisema marekebisho yanayotakiwa kufutwa hayakukidhi kipimo cha uwiano. Walisema ugombea binafsi haukupingana na demokrasia ya uwakilishi. Kwa hiyo wagombea binafsi hawatafifisha misingi ya demokarasia ya uwakilishi. Wakasema zaidi kwamba hakukuwapo vifungu vya kutosha kulinda na kuwatetea wananchi kutokana na matumizi mabaya ya madaraka na watu waliowekwa madarakani na mfumo wa vyama vya siasa na kwa hiyo vifungu hivi havikidhi kabisa kipimo cha uwiano. Wakizungumzia shauri la Afrika Kusini la MAKWANYANE (supra), lililonukuliwa na Wakili wa Mjibu Maombi, Bw Rweyongeza na Bw Mpoki walisema kuwa hata kama maaumuzi katika shauri hili yanashawishi mahakama zetu, shauri hilo pia linahimiza ulazima wa kuhimiza umuhimu wa kupanua wigo wa msingi wa kipimo cha uwiano, ili kwamba, ipendeze kwa matokeo ya matumizi ya kifungu fulani kutokuwa chanzo cha kuzuia haki inayotakiwa kupatikana na kwamba, mawakili hao wakaendelea, hiyo ndiyo kiini cha uamuzi katika shauri la REV. MTIKILA VS ATTORNEY GENERAL (supra), yaani kwamba uamuzi huo ulitolewa ili kwamba, kutotoa nafasi ya kunyang
  ’anywa haki yake mgombea binafsi. Na kwa hiyo uamuzi huo katika shauri la Afrika Kusini ni muhimu katika kuthibitisha uhalali wa kupanua wigo wa kipimo cha uwiano.
  Kuhusu kama kulikuwepo utaratibu uliowekwa na sheria, mawakili hawa wa Mleta Maombi waliikumbusha mahakama kuwa hoja hiyo ilitatuliwa na Jaji Ligakingira (kama alivyokuwa wakati huo) katika shauri la REV. MTIKILA VS ATTORNEY GENERAL (supra) ambapo kwa kutumia hoja ya ujumuisho ambayo kitendo cha ulinganifu kisipowezekana mahakama lazima zijielekeze kutoa haki za msingi hata kama gharama zake zitakuwa pamoja na kutovitilia maanani vifungu vya maneno katika kifungu cha sheria ikiwa kama kutekelezwa kwake kutasababisha kutotolewa haki.
  Kuhusu umuhimu na ushawishi wa mikataba ya kimataifa, mawakili wa Mleta Maombi walisisitiza imani yao kwamba uzito zaidi uwekwe kwenye mikataba hiyo kama ilivyoonyeshwa katika shauri la DAUDI PETE (supra). Mawakili hawa wakahitimisha maelezo yao kwa kuiomba mahaka hii kuyakubali maombi ya Mleta Maombi.
  Sasa ni zamu yetu kuyatazama na kuyachambua maelezo ya pande zote mbili za mawakili zinazopingana. Lakini kabla ya kufanya hivyo ni vema tukaweka wazi msingi utakaotuongoza katika kazi hii. Misingi hiyo ni ile inayoongoza namna ya kutafsiri katiba na utatuzi wa mashauri ya kikatiba. Misingi hiyo imewekwa na maamuzi ya kisheria katika mashauri mbalimbali nayo ni mingi, lakini katika shauri hili tumeamua kutumia ile tu ambayo tutaona ni muhimu na inaendana na mazingira ya shauri hili.
  Katika shauri Civil Appeal no. 64 la 2001 JULIUS ISHENGOMA & FRANCIS NDYANABO VS THE ATTORNEY GENERAL (unreported) Mahakama ya Rufani ya Tanzania (Samatta, Jaji Mkuu) katika uk. 17 - 18 aliweka misingi mitano.
  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni chombo kinachoishi, kikiwa na roho na kikijitambua chenyewe. Mahakama kwa hiyo lazima zijielekeze kutokilemaza kwa kufasiri kitaaluma au kwa njia nyembamba. Lazima kifasiriwe kwa kulingana na malengo yaliyokuwa vichwani mwa wale waliokiandaa.
  Vifungu vinavyogusa haki za msingi vifasiriwe katika njia pana na ya kiliberali, na kwa njia hiyo kulinda na kuendeleza mapana ya haki hizo na kuhakikisha kwamba watu wetu wanafurahia haki, demokrasia yetu changa isiwe tu inafanya kazi, bali ikue na matakwa na mahitaji ya watu yalindwe. Pale penye vizuizi kwa haki za watu lazima tafasiri yake iwekewe kizuizi. Kwa hiyo mahakama zina wajibu kutafasiri katiba kwa njia ambayo itaendeleza malengo mahsusi na maelekezo ya sera ya nchi.
  Mpaka hapo itakapothibitishwa vinginevyo, sheria yoyote ile inachukuliwa kuwa haikiuki katiba. Inapowezekana sheria lazima iwekewe tafsiri ambayo itaiwezesha kufanya kazi na siyo kutofanya kazi.
  Kwa vile kuna mawazo kwamba sheria haikiuki katiba isipokuwa pale ambapo kuna kifungu maalum kinachozuia au kinachotenga ambacho kimewekwa ili kuijenga misingi ya katiba (clawback or exclusion) ni jukumu la wale wanaopinga uhalali wa vifungu vya sheria, kulazimika kuthibitisha upotofu wa mawazo ya kuwepo vifungu hivyo kisheria.
  Na wale ambao wanaunga mkono kutopanuliwa kwa tafasiri ya haki fulani ya msingi kwa kutegemea kifungu kinachonyima haki (clawback or exclusion clause) katika kufanya hivyo, ni jukumu lao kuthibitisha uhalali wa kutopanua tafasiri ya haki inayotakiwa.
  Ingawa haikuelezwa katika msingi wa tano ilikuwa msimamo wa mahakama kuwa (ukichukuwa msimamo katika KUKUTIA OLE PUMBUN AND ANOTHER VS ATTORNEY GENERAL AND ANOTHER [1993] TLR. 150; kama nyongeza ya msingi kwamba):
  "Yeyote anayetegemea vifungu vinavyonyima haki analazimika kuthibitisha kuwa vifungu hivyo havionei, havina maana na havilingani na madai ya maslahi ya dola."
  Misingi mingine ya kutafsiri katiba ni pamoja na:
  Mahakama hazijali (not concerned) na busara ya Bunge ya kutunga sheria bali zinajali tu uwezo wake wa kutunga sheria.
  Ingawaje Bunge haliwezi moja kwa moja kutojali maamuzi ya mahakama ya sheria yaliyotamka kuwa sheria fulani ni kinyume cha katiba na kusema eti kifungu hicho kilikuwa halali, Bunge linaweza kutunga sheria nyingine mpya ambayo haina utata wa kuwa kinyume cha katiba.
  Mahakama zinakubali kuwa ustaarabu mwingi unategemea kwa kiwango sawa watu wanaofifisha uhuru pamoja na wale wanaopanua uhuru.
  Katiba haiwezi kutafasiriwa kipekee, bali kulingana na mambo mengine ikiwa pamoja na historia na msingi wa kukubalika katiba yenyewe. Lazima pia itafasiriwe kwa njia ambayo inahakikisha watu wanapata kile kilichokusudiwa wakipate kutokana na vifungu vya katiba hiyo.
  Tukianzia na misingi hiyo hapo juu ya kutafasiri katiba, hebu kwa kifupi tujaribu kueleza historia inayohusiana na vifungu vinavyohusiana na demokrasia ya uwakilishi katika historia ya Tanzania huru.
  Historia ya katiba ya Tanzania inaanzia na katiba ya Tanganyika (Constitution) Order in Council, 1961 iliyochapishwa kama Tangazo la Serikali no. 415 la 1/12/61. Orodha (shedule) ya pili katika tangazo hilo ilikuwa KATIBA YA TANGANYIKA. Kifungu cha 20 cha katiba kilitamka haki ya kila raia wa Tanganyika aliyefikisha umri wa miaka 21 kupiga kura alimradi hazuiwi na sheria ya Bunge. Vifungu vya 18 na 19 vya katiba hiyo vilielekeza namna sifa za anayefaa na asiyefaa kushiriki kupiga kura za wabunge. Kifungu cha 18 kilisema:
  "18 Pamoja na kutekelezwa kwa matakwa ya kifungu cha 19 cha katiba hii, mtu yeyote ambaye:
  ni raia wa Tanganyika.
  amefikisha umri wa miaka ishirini na moja, na
  ana uwezo wa kusema, na kama hazuiwi na upofu au ulemavu mwingine kusoma kwa lugha ya Kingereza bila tatizo lolote inayomwezesha kushiriki kikamilifu katika mijadala ya Bunge.
  "atakuwa na sifa za kupigiwa kura kuwa mbunge, na hakuna mtu zaidi ya hao atakayeonekana kuwa na sifa."
  Katiba iliyofuata ilikuwa sheria ya C.A No 1 ya 1962. (Katiba ya Tanganyika) kifungu cha 24 cha katiba ya Jamhuri kilibakiza sifa za mtu kuweza kugombea ubunge. Lakini kifungu cha 4(3) nacho kiliorodheshwa sifa za mtu kugombea urais. Kinasomeka hivi:
  "4 (3) Mtu yeyote raia wa Tanganyika ambaye:
  Ana sifa za kuandikishwa kama mpiga kura kwa ajili ya kugombea kwenye uchaguzi wa Bunge.
  Aliyefikisha umri wa miaka 30 na,
  Kama ni uchaguzi uliotokana na kuvunjwa Bunge, atakayeteuliwa na watu wasiopungua elfu moja waliosajiliwa kama wapiga kura katika uchaguzi wa Bunge atakuwa na sifa za kugombea urais.
  "
  Itagundulika katika maelezo haya kwamba katika katiba hizi hakukuwa na sifa ya u lazima wa mtu kuwa mwanachama wa chama cha siasa, ingawaje kulikuwa na vyama kadhaa vya siasa.
  Iliyofuata, ni katiba ya muda ambayo ilifuatia muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Hasa katika ibara ya 3(1) ilitamkwa bayana kuwa Tanzania ni nchi ya chama kimoja cha siasa.
  …
  "3 (3) Shughuli zote za kisiasa katika Tanzania zaidi ya shughuli za vyombo vya dola vya Jamhuri ya Muungano … zitaendeshwa kwa au chini ya chama."
  Ibara ya 4(4) iliharamisha:
  "Hakuna sheria ya Bunge itakayoruhusu kuondolewa sifa za raia yeyote wa Tanganyika na kumzuia asijiandikishe kama mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa watu au kwa ajili ya kumwondolea sifa mtu yeyote aliyejiandikisha kama mpiga kura kumzuia asipige kura katika uchaguzi isipokuwa kama ataamua kuwa raia wa nchi nyingine, ataugua ugonjwa wa akili, atapatikana na kosa la jinai, utoro au kushindwa kuthibitisha umri wake, uraia wake na kutojiandikisha."
  Kwa hiyo ingawa shughuli za kisiasa ziliruhusiwa tu kufanywa chini ya mwamvuli wa chama raia wote walikuwa na haki ya kushiriki uchaguzi kwa kupiga kura. Lakini katiba hii haikutaja bayana sifa za mgombea urais, kama kifungu cha 4 (3) cha katiba ya Jamhuri ya mwaka 1962. Badala yake, katiba ya 1965 iliacha jukumu la kutaja sifa za mgombea kwa Mkutano wa Uchaguzi kuteua mgombea urais. Huu ulikuwa Mkutano wa TANU wa Uchaguzi kama ilivyofafanuliwa katika sehemu E ya katiba ya chama iliyoambatanishwa kama orodha mojawapo ya katiba ya muda ya mwaka 1965.
  Tofauti na katiba za mwaka 1961 na mwaka 1962, ibara ya 27 ya katiba ya muda ya mwaka 1965 iliingiza katika katiba kwa mara ya kwanza sharti la mtu kuwa mwanachama wa chama ndipo aweze kugombea ubunge katika jimbo la uchaguzi. Kifungu hicho kilisema:
  "27(1) Raia yeyote wa Tanzania aliyefikisha umri wa miaka 21 na ni mwanachama wa chama ataruhusiwa, labda aondolewe sifa chini ya vifungu vifuatavyo vya kifungu hiki au na sheria ya Bunge ambayo inahusiana na kifungu hiki aondolewe sifa za kushiriki uchaguzi kama mbunge mwakilishi wa jimbo, na hakuna mtu mwingine atakayeweza kupata sifa kinyume cha sifa hii."
  Kwa hiyo sifa ya uanachama wa chama cha siasakama sifaya mtu kugombea nafasi ya kuchaguliwa Iliingizwa nchini
  pamoja na kukubalika mfumo wa chama kimoja cha siasa.
  Huu ni ukweli usioweza kupingika.
  Tunalazimika kuharakisha kuongeza hapa kuwa ingawa
  kulikuwepo vyama vingine vya siasa hadi mwaka 1965katiba
  zilizotangulia hazikuweka sifa ya mtu kuwa mwanachama
  wa chama cha siasa. Mwaka 1977 Tanzania ilitunga katiba
  yake ya kwanza ya kudumu, CHAMA CHA MAPINDUZI
  kikiwa kimejikita kama chama pekee nchini. Ibara ya 4 (2) ilibakisha haki ya wote kushiriki uchaguzi kama ilivyokuwa
  katika katiba. Hakuna sifa pekee iliyoelezwa kumhusu
  mgombea urais lakini uhusiano wake kisiasa na watu
  wengine unanjionyesha waziwazi kwa sababumgombea
  alilazimika kuteuliwa na Mkutano Mkuu wa chama. Lakini kwa
  wagombea wa ubunge wa majimbo, ibara ya 26 ya Katiba ya
  mwaka 1977 ilitamka kuwa:
  26 (1) ili mtu aweze kuchaguliwa kuwa mbunge wa kuwakilisha wilaya ya uchaguzi ni, lazima awe na sifa zifuatazo:
  ????
  awe mwanachama wa chama anayetimiza masharti ya uwanachama kama yalivyoelezwa katika katiba ya chama na pia awe na sifa za kiongozi zifuatazo: nakadhalika
  Katiba hii ilirekebishwa mwaka 1985 ili kuingiza haki za msingi. Ibara ya 3 (3) ilisisitiza serikali ya chama kimoja:
  "3 (3) Chama Cha Mapinduzi, kwa kifupi CCM ndicho chama cha siasa pekee katika Jamhuri ya Muungano."
  Ushiriki wa wote katika uchaguzi ulibakishwa tena katika ibara ya 5 ya ibara ya 110 inasema hivi:
  "10 (1) Shughuli zote za kisiasa nchini na zinazohusu Jamhuri ya Muungano zitaendeshwa ama na chama chenyewe au chini ya uongozi, usimamizi wa chama."
  Toleo hili la katiba liliingiza ibara ya 20 na 21, ambazo tunagundua ni muhimu katika maombi haya. Ibara ya 20(1) inasema:
  "20 (1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila kuathiri sheria za nchi kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.
  (2) Bila ya kuathiri sheria za nchi zinazohusika ni marufuku kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote.

  Ibara ya 21 inasema:
  "21(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja, au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
  (2) Kila raia anayo haki na uhuru wa kushiriki kikamilifu katika kufikia maamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha yake au yanayolihusu taifa.
  "

  Hebu sasa twende katika vifungu vinavyotawala sifa kwa ajili ya mgombea wa urais na sifa za wagombea wa ubunge majimboni ambayo ndiyo yanayohusika na mabishano katika maombi haya.
  Pamoja na marekebisho ibara ya 39 inasomeka hivi:
  "39 Mtu hatastahili kuchaguliwa kushiriki kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama:
  ametimiza umri wa miaka 40 na
  anazo sifa za kumwezesha kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.
  "
  Sifa za mgombea wa ubunge zimeorodheshwa katika ibara ya 67(1) ya katiba:
  "67(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa mbunge endapo:
  ………………………???
  ni mwanachama wa chama anayetimiza masharti yote ya uanachama yaliyoelezwa katika katiba ya chama
  …"
  Na neno chama limetafsiriwa katika ibara ya 151 likimaanisha:
  "Chama cha Mapinduzi kilichotajwa katika ibara ya 3 (3) na ya (10) ya katiba hii."
  Ukiritimba wa siasa wa Chama Cha Mapinduzi ulikomeshwa na marekebisho ya ibara ya 10, na kuingizwa na sheria namba 4 ya mwaka 1992, siasa za vyama vingi ziliporejeshwa tena Tanzania ambapo ibara za 20 na 21 zilibaki bila kufanyiwa marekebisho yoyote.
  Kifungu cha 13 cha sheria nambari 4 ya mwaka 1992 kilirekebisha ibara ya 39 lakini kikaacha bila kuirekebisha aya (c) ya sifa za mgombea urais.
  (c) ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chamacha siasa.
  "
  Kilichofanywa na sheria hapa ni kuhamisha sifa zile, ambazo awali hazikutamkwa wazi na sasa kuzitamka wazi. Kwa upande mwingine ibara ya 67(1)(b) ilibaki vilevile isipokuwa kwa mtu kuchaguliwa kuwa mbunge, sasa alitakiwa kuwa:
  "mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa."
  Marekebisho ya 8 (sheria namba 4 ya mwaka 1992) pia yalirekebisha ibara ya 77(3) ya katiba kwa kuruhusu kuwa:
  "(3) Wagombea uchaguzi katika jimbo la uchaguzi watatakiwa watimize yafuatayo:
  (a) wawe wamependekezwa mmoja mmoja, na chama cha siasa kinachoshiriki uchaguzi katika jimbo hilo.
  "
  Kabla ya hapo, ibara ya 77(1)(2) ilimhitaji mteuliwa wa uchaguzi wa bunge kuthibitishwa na Halmashauri Kuu ya chama, msimamo uliowekwa tangu wakati wa kuundwa katiba ya muda ya mwaka 1965 (ibara ya 28)(b)) na katiba ya mwaka 1977 (ibara ya 27(2)(b).
  Hivi ndivyo vifungu ambavyo Mleta Maombi alivipinga mahakamani katika shauri lake Misc. Civil Cause No. 5 of 1993. Baada ya kulitafakari sana shauri hilo na baada ya kupitia na kutafakari mashauri, vitabu na kanuni kadhaa Jaji Lugakingira katika shauri hilo (lililowekwa katika kumbukumbu kama) REV. CHRISTOPHER MTIKILA VS ATTORNEY GENERAL (supra) katika ukurasa wa 68 alihitimisha hivi:
  "Kwa yote niliyohitaji kuyataja na bila kuathiri aya zinazonyima haki katika ibara ya 39, 67 na 77 za katiba pamoja na kifungu cha 39 cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ya mwaka 1979, natamka na kuelekeza itakuwa halali kwa wagombea binafsi pamoja na wagombea watakaodhaminiwa na vyama, kugombea urais, ubunge na kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa. Uamuzi huu hautahusisha uchaguzi wa serikali za mitaa unaokaribia kufanyika katika siku chache zijazo."
  Kwa kutoridhika na uamuzi huu, Mjibu Maombi alikata rufani katika Mahakama ya Rufani wakati Mleta Maombi naye alikata rufani dhidi ya sehemu kadhaa katika uamuzi huo zilizotolewa dhidi yake. Hili lilikuwa shauri la rufani namba 3 la mwaka 1995. Haiwezi kupingwa na yeyote kwamba wakati shauri hili lilipokuwa linasubiri kusikilizwa mahakamani Mjibu Maombi (Mwanasheria Mkuu wa Serikali) aliandaa muswada wa sheria na kuendelea kutunga sheria ambayo ilisababisha maamuzi ya Mahakama Kuu yasiweze kutekelezeka na/au yakawa batili.
  Kwa msingi huo Mjibu Maombi aliomba kuiondoa rufani yake mahakamani. Mahakama haikuwa na jingine bali kukubali maombi ya shauri hili kuondolewa mahakamani lakini ikizungumza kupitia kwa Jaji Kisanga, Kaimu Jaji Mkuu Mahakama ya Rufani ilisema katika ukurasa wa 3 wa hukumu iliyochapwa kwamba:
  Tunalazimika kuonyesha mambo kadhaa namna Mrufani alivyoliendesha shauri hili ambayo yanasababisha tashwishwi kubwa. Wakati maamuzi yalikuwa yanasubiriwa, serikali hapo tarehe 16/10/94 ilipeleka muswada bungeni ikitaka kurekebisha katiba ili kwamba kuzuia kuwepo haki hiyo, na kwa hiyo kuyawahi maamuzi ya mahakama (pre-emptying) kama yangeenda kinyume cha matakwa ya serikali. Hapa ndipo mambo yalipoanza kuharibika. Serikali ilikuwa sasa inakumbatia njia mbadala ya kufikia malengo yake yaleyale kwa kuliomba Bunge kushughulikia shauri lilelile kwa wakati mmoja wakati Mahakama Kuu nayo inalishughulikia. Hii ilikuwa mbaya sana kwa sababu ambazo zitaonyeshwa hapa.
  Kwa hiyo serikali huku ikijua tena kwa makusudi ikaiingiza Mahakama katika mgongano wa waziwazi na Bunge kwa kuiiomba mihimili miwili ya dola kushughulikia suala moja kwa wakati mmoja. Mambo kama haya yalikuwa ya kusikitisha na yasiyotakiwa. Hayakuendana kabisa na unyoofu katika utoaji haki ndani ya nchi na njia zozote zile lazima zifanyike kuzuia mtindo huu wa utendaji.
  "
  Halafu Mahakama ikaendelea kuhitimisha kuwa:
  "katika shauri hili kama marekebisho ya katiba yangeanza na kupitishwa baada ya mahakama kutoa uamuzi wa rufani ile na kuhitimisha shauri hilo, katika sheria lingekuwa sahihi kiutaratibu, busara ya marekebisho yenyewe, hata hivyo, lingekuwa jambo jingine tofauti. Na hapo mgongano baina ya Mahakama na Bunge ungeepushwa. Na hii ingekuwa juhudi safi za kuendana na utawala wa kisheria ambao siku hizi unajumuishwa kuwa mojawapo ya sifa za jamii ya kidemokrasia."
  Marekebisho yanayoguswa katika uamuzi wa Mahakama ya Rufani ni yale yaliyofanywa na sheria namba 34 ya mwaka 1994 ambayo kama ilivyosemwa awali, yalipitishwa na Bunge tarehe 16/10/94 wakati uamuzi wa Jaji Lugakingira (kama alivyokuwa wakati huo) ulitolewa tarehe 24/10/94, kwa vile bado shauri lilikuwa mahakamani Bunge lilipopitisha sheria. Kwa kuzingatia utaratibu, ni lazima, kwa mara moja tulaani kitendo hiki cha Mjibu Maombi (Mwanasheria Mkuu) kwa vile kinapingana na matakwa ya Utawala Bora, na ambacho hatuwezi kufanya chochote zaidi ya kunukuu aya iliyotangulia ya hukumu ya Mahakama ya Rufani. Hili tutaliachia hapo na kwenda moja kwa moja kwenye suala la maombi yaliyopo mbele yetu.
  Sheria namba 34 ya mwaka 1994, ilirekebisha ibara ya 21, 39, na 67 za katiba kwa kuijumuisha ibara ya 21 na ibara za 5, 39, na 67. Ibara ya 5 inasisitiza ushiriki wa wote katika uchaguzi pamoja na kutekelezwa vifungu vingine vya katiba na sheria zingine zinazoweza kutungwa. Ili kutazama uzito wa marekebisho haya ya zamani na ya sasa ibara husika lazima zinukuliwe kikamilifu.
  Kabla ya marekebisho ibara ya 21 ilisomeka hivi:
  "21(1) kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayao haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria."
  Ibara mpya ya 21(1) sasa inasomeka ifuatavyo (toleo la 2005):
  "21(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 39, ya 47 na ya 67 ya katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria."
  Maneno yaliyopigiwa mstari yaliingizwa na marekebisho hayo kutokana na marekebisho ya 11 ya katiba. Ibara ya 39 inayotaja sifa za mgombea urais na zile za ibara ya 67(1), za katiba kama zilivyorekebishwa zinaelezea umuhimu wa kuwa mwanachama wa chama cha siasa kama sifa za wagombea urais na ubunge.
  Mleta Maombi anadai kuwa ibara hizi zinapingana na ibara ya 9(a) na (f), za katiba. Wakati huo Mjibu Maombi anadai kuwa marekebisho hayo ni sahihi, yalifanyika kisheria, kwa matakwa maalumu ya jamii kwamba hayapingani na misingi yoyote ya haki za binadamu. Ni kutokana na misimamo hii miwili inayopingana ambapo hoja ya kwanza inayobishaniwa iliandaliwa kuwa:
  "kama kweli ibara za 39(1)(c), 39(2), 67(b) na 67(2)(c) zinakiuka misingi ya katiba? "
  inaweza kuonekana kioja kwa akili ya kawaida kufikiria kuwa ibara za katiba zinaweza kupingwa mahakamani kwa kutokuendana na katiba na hivyo kukiuka katiba. Maombi haya yalipokelewa chini ya kifungu cha 4 cha sheria ya Basic Rigts and Duties Enforcement Act (Cap. 3) ambayo inawawezesha watu walioathirika kutokana na kuingiliwa kwa haki zao za msingi chini ya vifungu vya 12 na 29 vya katiba kuomba msaada wa mahakama. Kulingana na maombi yaliyorekebishwa, Mleta Maombi anaomba pamoja na ibara zingine chini ya ibara za 13(2), 20(4) na 21(1) na sehemu chini ya ibara ya 9(a) na (f). Kwa vile kifungu cha 4 cha sheria ya Haki za Msingi na Utekelezaji wa Wajibu (Basic Rights and Duties Enforcement Act) hakijumuishi ibara ya 9 sisi pia hatutatafakari maombi haya chini ya kifungu hicho, kwa vile ni nje ya mamlaka yetu. Hapa tutajishuhulisha na kutafakari kama kweli vifungu vya ibara ya 13(2) na 21 vya katiba vimekiukwa.
  Uwezo wa mahakama hii kuchunguza ukiukaji wa katiba wa ibara hiyo unapata nguvu ya kutoka ibara ya 30 (3) ya katiba ambayo inasomeka hivi:
  "30 (3) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika sehemu hii ya sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au wajibu kwake imevunjwa au inaelekea itavunjwa na mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu."
  Kwa Kingereza sahihi ibara hii inasema:
  "30(3) Any person alleging that any provision in this part of this chapter or in any law concerning his right or duty owed to him has been, is being or is likely to be violated by any person anywhere in the united Republic may institute proceedings for redress in the High Court."
  Katiba yetu imegawanyika katika sehemu 10 na sehemu zingine zina mafungu kadhaa. Sehemu ya kwanza ina mafungu matatu. Fungu la tatu la sehemu ya kwanza lina ibara 32. kwa hiyo ibara ya 30 (3) ya katiba inahusika tu katika utekelezaji wa fungu la tatu la sehemu ya kwanza ya katiba. Kwa hiyo mahakama hii inaweza kutamka kwamba mafungu na ibara fulani za katiba haziendani na/au zinakiuka katiba.
  Lakini kabla ya kuendelea, tunalazimika kugusia jambo moja, ambalo hakuna upande ulioliongelea. Na hili linahusu utaratibu wa kufungua malalamiko ya kupinga katiba chini ya sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi na Wajibu (cap. 3). Kifungu cha 5 cha sheria hiyo kinasema:
  "5. Kupeleka malalamiko au maombi Mahakama Kuu kulingana na matakwa ya kifungu cha 4 lazima kufanyike kwa kupeleka maombi kwa Msajili wa Mahakama Kuu husika kwa kutumia fomu maalum iitwayo originating summons."
  Katika shauri hili maombi yalipelekwa mahakamani bila kutumia originating summons. Hii inaonekana kupingana na kifungu cha 5 cha sheria hii ambacho ni lazima. Katika hali ya kawaida hali hii ingelazimu malalamiko haya yatupwe kwa kuwa hayafai kwa kutofuata utaratibu. Lakini shauri hili linahusu haki za msingi chini ya katiba. Katika shauri la THE JUDGE I/C HIGH COURT ARUSHA, AND ATTORNEY GENERAL VS N.I.N MUNUO NG’UNI Civil Appeal no. 45 of 1998 (unreported) Mahakama ya Rufani ya Tanzania ilikubali bila kinyongo aya ifuatayo kama ilivyoandikwa na mahakama iliyosikiliza shauri:
  Mahakama lazima zisichukue msimamo mkali (liberal approach) wakati wa kutekeleza kanuni za utendaji na utaratibu wakati wa kushughulikia mashauri ya haki za msingi na uhuru wa watu ili kwamba kumpa mlalamikaji nafasi ya kupata haki zake. Msingi wa msimamo huu ni kwamba kwa vile haki zinazotolewa na katiba zinalindwa kikamilifu na kwamba kukataa kuchunguza ukweli wa malalamiko ya kukiukwa katiba kwa msingi tu wa kutofuatwa utaratibu itakuwa kupingana na wajibu wa kutoa haki hizo. "
  Katika shauri hilo, Mahakama ilikuwa imeketi kusikiliza rufani kutoka Mahakama Kuu iliyoketi chini ya sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi na Wajibu kama tunavyofanya leo. Wao walikuwa wanatafakari namna ya kuomba nafuu maalumu ambalo lilikuwa jambo linalohusu utaratibu. Hapa hoja ni kukosekana fomu ile maalumu ya originating summons ambayo tunadhani inahusu mambo ya utaratibu wa kufuatwa. Kwa msingi uliowekwa katika shauri lililotajwa hapo juu, hatudhani kuwa kukosekana originating summons kunaweza kutuzuia sisi tusitende wajibu wetu.
  Bw Rweyongeza na Bw Mpoki wakimwakilisha Mleta Maombi wamesema kwamba ibara ya 21(1) ya katiba inalinda haki ya kila mtu kuchagua au kuchaguliwa au kuteuliwa kushiriki katika masuala yanayohusu serikali ya nchi, sheria namba 34 ya mwaka 1994 iliyorekebisha ibara ya 21(1), 39 na 67 inanyang
  ’anya haki hiyo kwa vile sheria hiyo inasema kuwa mtu anaweza tu kushiriki uchaguzi kama atateuliwa na chama cha siasa kugombea kiti cha urais au ubunge. Walisema kuwa marekebisho hayo pia yanapingana na ibara ya 20 (4) ambayo inazuia mtu kulazimishwa kujiunga na chama au shirika lolote. Mawakili hao waliendelea kueleza kuwa kifungu hicho cha sheria kinamaanisha kuwa ni wanachama tu wa chama cha siasa ambao wanakubalika kuchaguliwa kwa kura kuwa marais au wabunge. Wanahitimisha kuwa haya yanapingana au yanakiuka katiba.
  Mwanasheria wa Serikali Mwandamizi Bw Mwaimu alisema kuwa marekebisho hayo yalifanyika kisheria kupitia bunge kulingana na ibara ya 98 (1) ya katiba. Akirejea ibara ya 21(1) Mwanasheria huyo wa serikali kwanza alizungumzia kwa nini wagombea binafsi wakazuiwa. Alisema ilikuwa njia mojawapo ya kupata demokrasia ya uwakilishi, na ililenga kudumisha amani, utulivu, usalama na utengamano. Akithibitisha hoja yake juu ya kipimo cha uwiano, Bw Mwaimu alinukuu maamuzi kadhaa kutoka Afrika Kusini ambayo tutayazungumzia punde tu.
  Akijibu hoja hiyo Bw Rweyongeza na Bw Mpoki walisema kuwa ingawa Bunge lina uwezo wa kurekebisha vifungu vya katiba, uwezo huo una kikomo, ndiyo maana kipimo cha uwiano kinahitajika. Hapa mawakili hawa walinukuu maamuzi kadhaa ya Mahakama hii na Mahakama ya Rufani kuthibitisha usemi wao. Walisisitiza kuwa demokrasia ya uwakilishi haipingani na wagombea binafsi. Walipingana na msimamo wa Mjibu Maombi kuwa vyama vya siasa vinawawezesha wagombea kuandaa na kutangaza filosofia zao, kwa sababu hakuna taratibu zinazofaa zinazotumika kuzuia kuingiliwa na wale waliopo madarakani.
  Ingawa Mwanasheria wa Serikali aliiambia Mahakama kijuujuu (generally) kuhusu kutokiuka katiba kwa ibara zinazolalamikiwa katika uamuzi wetu huu tunataraji kutafakari na kuamua kila hoja kivyake kama ilivyokubalika na pande zote.
  Mjibu maombi anasema kuwa marekebisho hayo yanaendana na katiba kwa sababu yalifanywa na Bunge ambalo lina uwezo huo kulingana na ibara ya 98 (1) ya katiba. Tunadhani hiyo siyo hoja hapa. Tunakubali hoja kwamba ingawa Bunge lina uwezo wa kutunga sheria uwezo huo una kikomo. Kama Profesa Issa Shivji alivyosema katika makala yake
  "Constitutional Limits of Parliamentary Powers" aliyochapisha katika toleo maalumu la THE TANZANIA LAWYER October, 2003 ukurasa wa 39:
  uwezo wa kurekebisha katiba nao una kikomo. Ingawa ni kweli kwamba Bunge likitumia nguvu yake ya uwakilishi (constituency capacity)…linaweza kurekebisha kifungu chochote cha katiba, haliwezi kufanya hivyo katika njia ambayo itabadilisha msingi mzima au uhalisia wa katiba."
  Hoja hapa kwa hiyo ni kama marekebisho kwenye ibara ya 21(1) na ibara za 39 na 67 za katiba yaliendana na katiba. Tumejaribu kueleza hapo juu historia ya demokrasia ya uwakilishi. Tumeonyesha kuwa mara tu baada ya uhuru katiba zote mbili ya 1961, na 1962 hazikuweka vizuizi kwenye sifa za kugombea urais na ubunge. Tumeonyesha kuwa kizuizi hiki cha kulazimisha mtu kujiunga na chama ndipo agombee vyeo vya urais na ubunge kilianza kuonekana kwenye katiba ya muda ya 1965 na kikadumishwa tena katika katiba ya 1977 wakati chama hicho kilikuwa katika mfumo wa chama kimoja. Lakini hadi hapo haki za msingi zilipoingizwa katika marekebisho ya katiba ya 1984, hakukuwepo vifungu vinavyofanana na ibara za 20 na 21 ndiyo maana ya umuhimu wa kuwepo ibara za 39 na 67 ambazo zilisisitiza umuhimu wa kuwa mwanachama wa chama. Tumeona hapo juu ibara hizo zinasema nini. Kwetu sisi matokeo ya jumla ya kuwapo ibara za 20 na 21 ni kupanua wigo wa demokrasia ya uwakilishi. IIi kuthibitisha hili mtu na alinganishe ibara ya 20 (2) kama ilivyoonekana punde tu baada ya kuingizwa kwenye katiba haki za msingi na kuonekana katika katiba ya 1985 na ibara ya 20 (4) kama ilivyoonekana katika katiba ya 2005 ambapo inasomeka:
  "20 (4) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote au shirika lolote au kwa chama chochote cha siasa kukataliwa kusajiliwa kwa sababu tu ya itikadi au falsafa ya chama hicho."
  Kwetu sisi hii inaonekana kuwa, ingawa ibara za 20 na 21 za katiba zililenga kupanua wigo wa demokrasia na haki ya kushiriki katika masuala ya utawala wa nchi, ibara za 39 (1) (c) na 67 (1)(b) za katiba kama zilivyorekebishwa zinaonekana kufisha na kuzuia haki ya kugombea nafasi za kuchaguliwa isipokuwa kwa wanachama wa chama cha siasa pekee. Tunadhani kuwa ibara hizo haziwezi kwenda pamoja.
  Tumefikiri na kuona kuwa haki ya kujiunga au kutojiunga na vyama vya siasa ni muhimu kama haki ya kuabudu ambayo haiwezi kuwekwa kuwa msingi wa kugombea nafasi ya kuchaguliwa. Na hapa tunaendelea kuamua kuwa vifungu vya ibara za 21(1), 39(1) (c) na 67(1)(b) vinapingana na ibara za 20 na 21 za katiba. Lakini kupingana pekee hakuwezi kuwa msingi wa kutamka kuwa vifungu hivyo vinakiuka katiba. Hili sasa linatupeleka katika hoja ya pili ya kama vifungu vinavyolalamikiwa vinakidhi kipimo cha uwiano?
  Kuviweka vifungu hivyo katika kipimo cha uwiano lazima ionyeshwe kuwa ibara hizo zinaokolewa na ibara za 30 na 31 za katiba, lakini ibara ya 30 (1) kwa mawazo yetu ni muhimu zaidi. Inasomeka hivi:
  30 (1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
  "
  Kama tulivyoona hapo juu, mara tu mlalamikaji anapothibitisha kuwa haki zake za msingi zimekiukwa jukumu linamwelemea Mjibu Maombi kuthibitisha kuwa vifungu vinavyolalamikiwa vipo kwa maslahi ya jamii. Kama Mahakama ya Rufani ilivyoliweka katika shauri la KUKUTIA OLE PUMBUN (supra):
  "Sheria inayotaka kuweka kikomo au kupingana na haki za msingi za mtu kwa kigezo cha maslahi ya taifa itatangazwa kuwa ni kinyume cha katiba hadi hapo itakapothibitishwa kukidhi mambo mawili:
  kwamba haionei watu, na
  kwamba kikomo kilichowekwa na sheria hiyo siyo zaidi ya ambavyo ingehitajika ili kupata zuio la kisheria lililohitajika.
  "
  Mahitaji ya kupima vifungu vinavyolalamikiwa kwa kipimo hiki hayalalamikiwi na pande zote mbili. Pia haibishaniwi kuwa jukumu sasa lipo kwa Mjibu Maombi kuthibitisha uhalali wa vifungu vinavyolalamikiwa.
  Wakifafanua jambo hili mawakili wa Mleta Maombi walisema kuwa ili kupita kipimo cha uwiano lazima ionyeshwe kuwa vifungu vinavyolalamikiwa vililengwa kukidhi mahitaji ya jamii na maslahi ya umma, na kwamba pingamizi lililowekwa lilikuwa sahihi ili kufikia malengo. Wakasema kuwa vifungu vinavyolalamikiwa kama vilivyorekebishwa havishindi kipimo cha uwiano.
  Mwanasheria wa Serikali Bw Mwaimu aliieleza mahakama kwa kirefu kwa nini Bunge lilipitisha sheria hiyo. Namnukuu kama ifuatavyo:
  marekebisho haya yalifanywa ili kukidhi mahitaji maalumu ya jamii… Zuio kwa wagombea binafsi katika Uchaguzi Mkuu na katika chaguzi za Serikali za Mitaa ni njia mojawapo ya kupata demokrasia ya uwakilishi … ni sera ambayo inalenga kulinda amani, utulivu, usalama na utengamano…"
  Mwanasheria wa Serikali pia alisimika utetezi wake kwenye ibara ya 3 (1) ya katiba na kuhitimisha kwa kusisitiza umuhimu wa kiongozi mtarajiwa kupimwa kupitia chama cha siasa. Hapo ndipo Bw Mwaimu alipoingiza mashauri ya Afrika Kusini ya SOUTH AFRICA VS MAKWANYANE [1995] (3) S.A. 391(CC) and S VS. BHULWANA [1996] (1) SA 388 (CC).
  Bila kuterereka, Bw Rweyongeza na Bw Mpoki wakimwakilisha mlalamikaji walijibu kwamba kipimo cha uwiano hakikufikiwa. Walinukuu maamuzi ya Mahakama hii katika shauri la PETER NGOMANGO VS KIWANGA & ANOTHER [1993] TLR, 77 na maamuzi ya Mahakama ya Rufani katika mashauri ya DPP VS DAUSI PETE [1993] TLR 22, na MBUSHUU VS REPUBLIC [1995] TLR. 97. Waliendelea kunukuu hata mashauri yaleyale kutoka Afrika Kusini ya MWAKWANYANE (supra) na BHULWANA (supra) kuthibitisha hoja yao wakisema kuwa pamoja na kupanua wigo wa msingi wa kipimo cha uwiano mazuio yanayowekwa na sheria yataweza kukubalika tu kama yatakuwa:
  ya maana,
  yanaonekana muhimu katika jamii iliyo wazi na ya kidemokrasia kwa msingi kuwa iko huru na sawa, na
  kwa vyovyote vile hayatapingana na maelezo muhimu yanayoelezea haki inayotakiwa.
  Kwa hiyo wakasema kuwa maamuzi ya Jaji Lugakingira (kama alivyokuwa wakati huo) yalikuwa sawa na hayakupingana na maelezo muhimu yanayoelezea haki iliyotakiwa ya mtu kugombea kama mgombea binafsi au kupitia chama cha siasa anachokichagua.
  Kwa hakika hatuna haki ya kuhoji busara ya kutunga marekebisho ya katiba yanayolalamikiwa hapa lakini kama tukifikiri kwamba Mjibu Maombi alikuwa akitekeleza jukumu lake la kutoa uthibitisho, hatukuridhika kwamba katika shauri hili Mjibu Maombi amefanikiwa kutoa uthibitisho huo. Hoja zake zaweza kuwa tamu masikioni lakini hazikuthibitishwa na ushahidi wa taarifa muhimu. Hakuna ushahidi kabisa kuthibitisha kwamba kuwepo mtindo wa wagombea binafsi ni kinyume cha demokrasia ya uwakilishi. Kwa uhakika kama tulivyoonesha hapo juu hakukuwepo na zuio kama hilo kwa wagombea binafsi mara tu baada ya nchi yetu kuwa Jamhuri. Hakuna hoja kwamba kutokuwepo wakati huo kwa sifa ya kuwa mwanachama wa chama cha siasa kuliisumbua jamii wakati huo.
  Tumepata bahati pia ya kusoma mashauri ya Afrika Kusini yaliyotajwa na Bw Mwaimu. Katika shauri la S VS. BHULWANE [1996] 1 South African Law Report, Mlalamikiwa alipatikana akiwa na gramu 8569 za bangi. Alihukumiwa kwa sheria inayosimika mawazo ya kuwepo hatia chini ya kifungu cha 21(1)(a) cha sheria ya madawa na usafirishaji madawa. Vifungu vya sheria hii vilipingwa kwa msingi kuwa vilikiuka haki za msingi ikiwemo haki ya kuchukuliwa kama mtu asiye na makosa hadi apatikane na hatia mahakamani. Halafu kifungu cha 33 (1) cha katiba ya Afrika Kusini kilifikiriwa na kujadiliwa na Mahakama ya Katiba kupitia kwa Jaji O
  ’REGAN katika uk. 395 wa ripoti ilisema:
  Kwa ujumla kwa hiyo, Mahakama huweka malengo, matokeo na umuhimu wa sheria inayolalamikiwa upande mmoja wa mzani na hali na matokeo ya athari ya sheria hiyo upande mwingine wa mzani. Kadiri inapodhihirika kama kuna ukiukaji wa haki za msingi unaoonekana ndivyo ushawishi wa hoja ya kukiukwa haki hizo unavyozidi."
  S. VS MWAKANYANE AND ANOTHER (supra) lilikuwa shauri jingine ambapo kifungu cha 277(1)(a)(c) cha sheria ya mwenendo wa mashauri ya Jinai namba 51 ya 1977 iliyoruhusu hukumu ya kifo kilipolalamikiwa kuwa kilikiuka katiba. CHASKASON P. wa Mahakama ya Katiba alifanya majumuisho yafuatayo katika ukurasa wa 403 GH kwamba:
  Sihitaji kusema zaidi katika hukumu hii zaidi ya kuwa kifungu cha 11(7) cha katiba hakiwezi kufikiriwa kipekee bali katika ujumla wake ambao unajumuisha historia na mwanzo wake wakati wa kutunga katiba yenyewe na hasa hasa vifungu vya sura ya tatu ambayo katiba hiyo ni sehemu yake. Ni lazima pia ifikiriwe katika njia ambayo itawawezesha raia kupata mafanikio kamili ya vifungu hivyo."
  Tumebahatika pia kusoma maamuzi katika shauri la SAGHIR AHMED AND ANOTHER VS STAFF OF V.P. AIR 1954 SC 728. Mrufani katika shauri hili alilalamikia sheria iliyonyima wengine haki ya kutumia barabara kuu. Tunakubaliana na Bw Mwaimu kuwa hali katika shauri hilo ilikuwa tofauti, kwa vile pale malalamiko yalikuwa juu ya sheria na siyo vifungu vya katiba yenyewe. Hata hivyo maamuzi katika shauri hilo ni muhimu kwa sababu yaliweka msimamo kuwa:
  "Bila shaka kuna mawazo ya sheria kuendana na katiba. Lakini pale sheria hiyo inapoonekana kunyima haki za msingi zinazolindwa na ibara ya 19 (1)(g) ya katiba, lazima itamkwe kuwa sheria hiyo ni batili mpaka hapo wale wanaoishabikia sheria hiyo watakapoihakikisha kuwa inakubalika kutokana na kukubalika sababu ya kuwepo kizuizi kilichowekwa."
  Na kwamba:
  "Hoja kwamba huenda kizuizi kilichowekwa na sheria fulani katika kutekeleza haki za msingi chini ya ibara ya 15 (1)(g) zina mantiki au la itategemea hali halisi ya shughuli na mazingira yake."
  Tunafikiri kwamba maelezo haya ya tafsiri ya katiba yanatumika kwa wote popote pale iwe kinacholalamikiwa ni vifungu vya katiba yenyewe au vifungu vya sheria fulani."
  Katika shauri la DEENA @ DEENA DAYAL ETC VS UNION OF INDIA AND ANOTHER [1984] 1 SCR, 1, hukumu ya kifo ilikuwa inalalamikiwa kuwa inakwenda kinyume cha katiba. Pale pamoja na mambo mengine Mahakama Kuu ya India ilishikilia msimamo kuwa:
  "Katika mashauri yanayoletwa chini ya ibara ya 21 ya katiba, kama itaonekana kwamba mtu ananyang’anywa uhai wake au amenyang’anywa uhuru wake, jukumu linabaki kwa serikali kuthibitisha uhalali kikatiba wa sheria iliyotumika kunyang’anya uhai au uhuru wa mtu huyo."
  Msingi huu unakubalika pia katika shauri kama katika shauri hili mtu anapodai kuwa haki yake ya msingi ya kushiriki katika uendeshaji wa serikali ya nchi imenyang’anywa na kifungu fulani cha katiba.
  Tulichokipata kutoka maamuzi haya yanayoshawishi yaliyonukuliwa na wakili wa Mleta Maombi chaweza kuwekwa kwa kifupi kama ifuatavyo:
  Pale ambapo mtu anadai kapokonywa haki yake ya msingi jukumu huhama na kuilemea serikali kuthibitisha uhalali wa sheria inayopokonya haki.
  Iwe kweli au isiwe kweli kuwa kupokonywa huko au zuio lililowekwa lina mantiki yoyote au halina itategemea hali halisi ya upokonyaji haki au zuio lililowekwa.
  Katika kuamua kama sheria au kifungu cha katiba kinacholalamikiwa ni cha msingi au siyo lazima kitafasiriwe kwa kufuata historia yake na mwanzo wake, ili kwamba kuhakikisha kuwa raia anapata kikamilifu haki zake, ili kwamba yale mambo muhimu katika haki hizo yapatikane yote.
  Tumejraribu hapo juu kuonyesha historia ya ibara za 20 na 21 za katiba zilivyoingizwa ili kupanua wigo wa demokrasia ya uwakilishi na ushirikishwaji katika masuala ya kitaifa. Katika mpangilio wa katiba, hii ndiyo mojawapo ya haki za msingi za raia wa Tanzania. Tumeona vilevile kuwa sifa ya kuwa mwanachama wa chama cha siasa ili uweze kugombea nafasi ya uongozi haikuwa inafahamika kabla ya katiba ya muda ya mwaka 1965 na kusimikwa kwa serikali ya chama kimoja. Kwa hiyo ilitokea na kuendelea kutawala katiba zingine zote zilizofuatia kama kumbukumbu ya sera ya siasa ya chama kimoja. Kwa hiyo haiwezi kusemwa kwamba wakati wa serikali ya chama kimoja, haki ya kushiriki kuchaguliwa kuwa kiongozi ilihodhiwa na wanachama wa chama cha siasa tu. Baada ya kuingizwa haki za msingi kwenye katiba mwaka 1985 na baadaye kukubalika siasa ya vyama vingi mwaka 1992, uanachama wa chama cha siasa ulibaki hauna maana yoyote, isipokuwa kama kumbukumbu ya utawala wa chama kimoja kwa sababu siyo tu kwamba ukiritimba wa chama ulikomeshwa na ibara ya 3 ya katiba bali pia ilikataliwa waziwazi chini ya ibara ya 20 (4) kumlazimisha mtu kujiunga na ushirika wowote au chama. Ni kutokana na ukweli wa habari hii tumekuwa na msimamo thabiti kuwa ibara za 20 (4) na 21 (1) zinahimiza haki za msingi, na ibara za 39 (1) (c) na 67 (1) (b) lazima zitafsiriwe ili kupata manufaa kamili ya haki za msingi. Kwa kutafakari sana tumekuwa na msimamo kuwa ibara ya 39 (1)(c) na 67 (1)(b) zinaingilia na kufisha haki za msingi ambazo zimehakikishwa chini ya ibara za 20 (4) na 21(1) za katiba. Pia tumeridhika kwamba Mjibu Maombi ameshindwa kutekeleza jukumu lake la kuthibitisha uhalali wa zuio la haki ya kugombea bila kujiunga na chama, kwa sababu kwanza jambo hili ni la kihistoria na pili hawakutoa uthibitisho kuhalalisha uoga wao juu ya wagombea binafsi. Ni kweli kwamba ibara ya 3 inaingiza mfumo wa siasa ya vyama vingi lakini hatudhani kuwa jambo hili linapingana na kuwepo kwa wagombea binafsi. Kuwepo wagombea binafsi kunaweza bila shida yoyote kuendelea wakati nchi ikifuata siasa ya vyama vingi kama ilivyokuwa wakati huo kabla ya katiba ya muda ya mwaka 1965.
  Vilevile tumepima mizania ya malengo, matokeo na umuhimu wa ibara zinazolalamikiwa ikilinganishwa na hali halisi na matokeo ya kuporwa haki kutokana na matumizi ya ibara hizo, na tumeridhika kuwa madhara yake ni makubwa na si halali kabisa kupora haki za msingi za mtu na tunadhani mwenendo kama huu lazima ukomeshwe kama tunataka katiba yetu ibakie kuheshimika kwa kulinda haki za msingi za raia. Kama Mwalimu Julius K. Nyerere alivyoliweka jambo hili katika kitabu chake OUR LEADERSHIP AND THE DESTINY OF TANZANIA, HARARE AFRICAN PUBLISHING GROUP 1995, p. 9, akinukuliwa na Profesa Issa Shivji katika makala yake CONSTITUTIONAL LIMITS ON PARLIAMENTARY POWERS (supra).
  "Hii ni hatari sana. Tutakomea wapi? Kama sehemu moja ya haki za msingi inaweza kubadilishwa (kurekebishwa), nini kitazuia haki zote za msingi kubadilishwa na kufanywa si chochote kwa kuvihoji na kuvibadili vifungu vyote vya haki hizo?"
  Tulianza hukumu yetu kwa kusema kuwa moja ya misingi ya kutafsiri katiba ni kwamba katiba lazima ichukuliwe kama kiumbe chenye uhai. Pamoja na elimu kidogo tunayoweza kuwa nayo, tunajua msingi mkuu wa uhai kuwa vitu vyote vyenye uhai hukua na kuongezeka ukubwa baada ya muda, lakini, labda kitu hicho kife, hakikui kwa kupungua ukubwa wake. Kwa maana hiyo, vifungu vya katiba yetu vinavyosimamia demokrasia ya uwakilishi, baada ya kuzinduka kutoka kwenye giza nene la mfumo wa chama kimoja lazima itafsiriwe ili kwamba iweze kupanua wigo wa demokrasia ya uwakilishi na siyo kuififisha na kuturejesha katika enzi hizo zilizopita kama ilivyodhihirishwa na majaribio yaliyofanywa na sheria namba 34 ya mwaka 1994. Hili linakuwa muhimu zaidi leo hii ukiangalia hali tete ya vyama vyetu vya upinzani vilivyopo pamoja na chama tawala cha CCM kama ilivyodhihirishwa na matokeo ya hivi karibuni ya Uchaguzi Mkuu.
  Kwa hiyo katika kuhitimisha hoja mbili za hapo juu, tunapenda kusema waziwazi kuwa katika mtazamo wetu sheria namba 34 ya 1994 iliyorekebisha ibara ya 21(1) ili kwamba iendane na ibara za 5, 39, na 67 ambazo ziliingiza kwenye katiba vizuizi kwa watu wengine kwenye ushiriki katika mambo ya kiutawala wa nchi na uendeshaji wa serikali isipokuwa tu kwa wanachama wa chama cha siasa tu ilikuwa kuingilia haki za msingi na kwamba kuingilia haki hizo kulikuwa hakuhitajiki kabisa na hakukuwa na mantiki yoyote, na kwa hiyo hakukupita kipimo cha uwiano. Kwa hiyo tunatamka kwamba marekebisho ya ibara za 21(1), 39(1) (c) na 67(1)(b) yalikiuka katiba.
  Tutamalizia hoja ya tatu kwa kifupi, ingawa hatudhani kuwa ni ya muhimu baada ya haya tuliyoyaona na kuyagundua katika hoja mbili za kwanza. Hoja ya tatu ni kama vifungu vinavyolalamikiwa vinakiuka mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia?
  Bw Rweyongeza na Mpoki wakimwakilisha Mleta Maombi wamesema kwamba ibara zile zinakiuka Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Binadamu na Mkataba wa Nchi za Afrika wa Haki za Binadamu na Makundi ya watu. Walinukuu ibara za 20 (1) na (2) na 21(1) za mkataba huo na ibara za 10 (2)(1) na 29 za mkataba wa Nchi za Afrika juu ya Haki za Binadamu katika kufafanua hoja zao, na shauri la DPP VS DAUDI PETE (supra) kuonyesha umuhimu wa mikataba hii katika kutafsiri katiba yetu.
  Kwa upande mwingine, Bw Mwaimu akimwakilisha Mjibu Maombi haonekani kupinga kwa nguvu kuwepo mikataba hiyo na matokeo yake lakini akasema mikataba hii itazamwe na kufikiriwa kulingana na mipaka yake. Alinukuu ibara ya 29(2) ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Binadamu kufafanua hoja yake. Alisema kwamba kwa msingi wa mipaka ya mikataba hiyo ibara za katiba zinazolalamikiwa zilitungwa ili kudumisha tabia njema, utulivu na maslahi ya watu. Kwa hiyo akasema mahakama lazima igundue kuwa hata kwa kufuatana na mikataba hii ya kimataifa, marekebisho yale yalikuwa halali na yana mantiki. Na hivyo aliomba kuwa maombi haya yatupiliwe mbali na Mleta Maombi alipe gharama za shauri hili.
  Kama Mahakama ya Rufani ilivyosema katika shauri la DAUDI PETE, hatuna shaka kuwa mikataba ya kimataifa lazima ifikiriwe wakati wa kutafsiri, siyo tu katiba yetu bali pia na sheria zingine, kwa sababu Tanzania haipo tu ikielea hewani tu au kama kisiwa bila kuwepo nchi zingine. Ni sehemu ya jumuia ya kimataifa. Kwa hakika, kundi zima la haki za msingi lilichukuliwa kutoka kwenye Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Binadamu. Tukirejea shauri lililopo mbele yetu, ibara za 20 na 21 (kama zilivyoandikwa mwanzo kabla ya marekebisho) ya katiba ni sawasawa kabisa na ibara za 20 (1) na (2) na 21 za Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Binadamu. Mkataba wa Haki za Kiraia na Kisiasa uliofuatia Tamko la Mkataba wa Haki za Binadamu na ambao uliridhiwa na Tanzania Juni 1976 unasema katika ibara yake ya 25 kuwa:
  "Kila raia atakuwa na haki na fursa bila kuwapo utofauti uliomo katika ibara ya 2 na bila kuwapo pingamizi la kipuuzi:
  kushiriki mambo ya kiutawala moja kwa moja au kupitia kwa wawakilishi waliochaguliwa kwa uhuru.
  Kupiga kura na kuchaguliwa katika chaguzi zilizopangwa katika vipindi mbalimbali ambazo zitakuwa kwa wote na kwa usawa zitakazofanyika kwa kura za siri ili kuhakikisha wapigakura wanatoa maamuzi yao kwa uhuru na haki.
  "
  Ibara ya 2 ya mkataba huu, inahakikisha haki ya mtu bila kujali tofauti yoyo te kama vile mwelekeo wake kisiasa au mawazo yake.
  Ibara ya 29(2) ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Binadamu, uliotegemewa na Bw Mwaimu una uzito ule ule sawa na ibara ya 30 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama ilivyoonekana hapo juu uzoefu wa maamuzi ya Mahakama umelazimisha uhalali wowote wa kubana haki za msingi chini ya ibara ya 30 (1) ufuate kipimo cha uwiano. Tunadhani tumeweza kuthibitisha hapo juu kuwa marekebisho yaliyoletwa na sheria namba 34 ya mwaka 1994 na kuyaingiza kwenye ibara za 21(1), 37(1)(c) na 69(1) na (2) za katiba, hazivuki kipimo hicho kwa vile zinajaribu kuingilia haki za msingi za raia kushiriki katika masuala ya utawala wa serikali yao. Tuna msimamo usiotetereka kuwa mtu kuwa mwanachama wa chama cha siasa kufanywa sifa ya kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi ya uongozi ni zuio lisilokuwa muhimu eti kwa lengo la kupata na kudumisha tabia njema, utulivu na maslahi ya umma. Tunafahamu kuna njia mbadala na nzuri zaidi za kuyafikia hayo. Na kwa hiyo kwa mawazo yetu vifungu vya sheria vinavyolalamikiwa haviokolewi hata chini ya ibara ya 29(2) ya mkataba wa Haki za Binadamu. Kwa msingi huo, tunakubaliana na Wakili wa Mleta Maombi kwamba marekebisho ya ibara za 21(1), 39(1)(c) na 67(1)(b) za katiba pia yanakiuka mikataba ya kimataifa. Kwa hiyo tunajibu hoja ya tatu kwa kukubaliana na Mleta Maombi.
  Kwa sababu zote zilizotolewa hapo juu sasa tunafikia hitimisho la shauri hili kwamba lazima maombi haya yakubaliwe. Tunao mtizamo ulio imara kuwa marekebisho ya ibara ya 21(1), ibara ya 39(1)(c) na ibara ya 67(1)(b) zilizoingizwa kwenye katiba na sheria namba 34 ya 1994 au kama ilivyozoeleka kuwa marekebisho ya 11 si ya muhimu na yameweka mazuio yasiyokuwa na mantiki yoyote kwenye haki za msingi za raia wa Tanzania kugombea nafasi kadhaa za uongozi wa nchi kama wanachama wa vyama vya siasa au kama wagombea binafsi. Kwa hiyo tunaendelea mbele na kutamka kuwa marekebisho hayo yamekiuka katiba na pia yamekiuka mikataba ya kimataifa ambayo Tanzana imeridhia.
  Katika shauri la REV. MTIKILA VS ATTORNEY GENERAL [1995] TLR 31, uk. 68 Mahakama hii kupitia kwa Jaji Lugakingira (kama alivyokuwa wakati huo) ilitamka na kuamuru kwamba:
  itakuwa halali kwa wagombea binafsi kwa pamoja na wagombea watakaodhaminiwa na vyama vya siasa kugombea, urais, ubunge na nafasi yoyote katika chaguzi za serikali za mitaa."
  Nasi lazima tutamke kwamba kimsingi itakuwa halali kwa wagombea binafsi kugombea nafasi za urais na ubunge kwa pamoja na wagombea walioteuliwa na vyama vya siasa. Lakini tofauti na alivyoelekeza Marehemu Jaji Lugakingira, hatutaliachia hapo suala hili. Tukitumia mamlaka yetu chini ya kifungu cha maombi kilichotutaka tutoe haki nyingine yoyote tutakayoona inafaa, na kwa kutambua kwamba kutokea ombwe la uongozi kunaweza kusababisha vurugu na mivurugano ya kisiasa, tunaamuru kwamba Mjibu Maombi kwa misingi iliyowekwa na ibara ya asili ya 21(1) na kuongozwa na malengo makuu na misingi ya sera za dola kama zilivyoelezwa katika seheu ya II ya katiba tangu sasa hadi wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao, aandae sheria zitakazoongoza na kusimamia shughuli za wagombea binafsi. Ili kuweza kuhakikisha mapenzi ya watu yanakubalika na kuheshimiwa kama wagombea hao wanafaa au hawafai. Na kwa vile shauri hili lilikuwa shauri lenye kugusa maslahi ya umma kila upande utajilipia gharama zake wenyewe.
  Imeamriwa hivyo.
  Sahihi A.R. MAENTO - JAJI
  Sahihi S.A. MASSATI - JAJI
  Sahihi T.B. MIHAYO - JAJI
  Maneno 10,137
   
Loading...