Nafasi ya Mamlaka kwenye mchakato wa upimaji wa Vinasaba vya Binadamu (DNA)

Rahma Salum

Member
Sep 7, 2020
30
59
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, misingi ya Sheria ya Usimamizi wa Vinasaba namba 8 ya mwaka 2009 inaeleza umuhimu wa kushirikisha upande wa tatu

Upande huo huweza kuwa Jeshi la Polisi, Mahakama, Mwanasheria au Ustawi wa Jamii

Mamlaka hizo huandika barua kwa niaba ya mteja na lengo la kufanya hivyo ni kuzuia vurugu baada ya matokeo kutoka, kwani mamlaka hizo zitatumika kama washauri kwa wateja wao.


========================


Sheria ya Usimamizi wa Vinasaba vya Binadamu ya 2009,Sura ya 73.

NANI ANAWEZA KUPIMWA DNA.
Yeyote ambaye anahitaji kujua kuhusu uhalali wa uzazi wake anaweza kupima DNA. Upimaji huu hauna umri. Hata hivyo DNA si kwa jili ya masuala ya kuthbitisha uzazi tu, bali hutumika hata katika masuala ya ushahidi na upelelezi.

NANI ANA MAMLAKA YA KUOMBA DNA KUPIMWA.
Si kila mtu anaweza kuomba kupima DNA. Hata kama mwenye uhitaji ni wewe lakini bado huna mamlaka ya kuomba kupima DNA. Kifungu cha 25(2) cha Sheria niliyotaja hapo juu kinawataja wafuatao kuwa na mamlaka ya kuomba DNA kupimwa. Kinamtaja hakimu ambapo kuna kesi/shauri fulani linaendelea, Wakili, afisa ustawi wa jamii, afisa polisi mwenye cheo zaidi ya inspector,daktari, na mkuu wa wilaya.Hawa ndio wenye mamlaka(Requesting Authority).

Kwahiyo wewe ukiwa na shida ya DNA unaweza kumuona mmoja kati ya hawa ili aandae maombi ya kupima DNA na kuyapeleka kunakostahili.

MAOMBI YA DNA YANAPELEKWA WAPI.
Kifungu cha 24 cha Sheria ya Usimamizi wa Vinasaba kinaitaja maabara ya Vinasaba vya binadamu ya Mkemia Mkuu wa serikali kuwa na Mamlaka ya kupima DNA. Pia kinazitaja na maabara nyingine ambazo zitakuwa na leseni maalum ya kupima DNA kuwa na mamlaka hayo.

Kwahiyo maombi ya DNA yatapelekwa moja kati ya sehemu hizo mbili.

NANI ANAPELEKA MAOMBI NA KUFUATILIA MAJIBU.
Wahusika waliopimwa DNA(sample source) hawaruhusiwi kupeleka wala kufuatilia majibu ya DNA. Maombi na Majibu ya DNA yatapelekwa na kufuatiliwa na hao niliowajataja hapo juu katika 2 ambao ndio wenye mamlaka ya kuomba DNA kupimwa.

Hawa ndio watapeleka maombi na ndio watachukua majibu na kuwasomea wahusika.

MAOMBI YA KUPIMA DNA YANAKUWAJE ?.
Kifungu cha 26(1) cha Sheria hiyo kinasema maombi ya kuomba DNA kupimwa yatakuwa katika mfumo maalum wa maandishi. Yataeleza muombaji na cheo chake, yataeleza wanaotakiwa kupimwa DNA na sahihi zao,yataeleza DNA ipimwe katika nini na nini, yataeleza sababu za kupima DNA,yatakuwa na kiapo kuwa majibu hayatatumika kwa shughuli nyingine tofauti na iliyoombwa, na yatasainiwa na muombaji ambaye ni wale niliowataja katika 2 juu.

ADA YA KUPIMA DNA NI KIASI GANI.
Malipo yapo. Na mpaka disemba 2018 ada ni Tshs 100,000/=( laki moja tu) kwa kila mtu. Kawaida DNA ya kutambua uzazi(parentage) hupimwa watu watatu. Mama, baba na mtoto. Kwahiyo kila mmoja ni laki moja na hivyo watatu ni laki tatu.

Nani anatoa hiyo hela, anaweza kuwa yule anayehitaji kuthibitisha kwamba yeye ni mzazi halali, au yakawa ni maelewano ya wahusika, au kutokana na maelekezo ya mahakama.

DNA INAPIMWA KATIKA NINI NA NINI.
Kifungu cha 29(1) cha sheria hiyo kinaeleza maeneo ambayo DNA inaweza kupimwa kuwa ni kwenye mate, damu, mkojo, ute ute wa sehemu za siri, nywele,haja kubwa,ngozi,mifupa,meno,mbegu za kiume,unyayo na sehemu nyingine ambayo mhusika atakuwa amegusa,kukanyaga au kuwepo au alama yoyote ya uwepo wake.
 
Hili ni jambo zuri na la muhimu sana, itaepusha matatizo mengi.
 
Back
Top Bottom