Nafasi ya Kazi Arusha.

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
May 11, 2015
23,372
54,909
Natumaini tu salama wana JF na kila mmoja yupo katika ujenzi wa Taifa kuhakikisha mkono unaenda Kinywani.

Najitokeza hapa Kumwombea Nafasi ya Kazi Mdogo wangu (miaka 20) kwa mkoani Arusha.

Elimu yake ni kidato cha nne ( hana ujuzi wa fani yeyote ile) kwa yeyote ambaye atakuwa na usaidizi wa aina yeyote katika hili nitashukuru sana.

NB: Awali pia nimejaribu kuulizia nafasi katika viwanda hapa Arusha ila sijafanikiwa kupata sehemu kwa ajili yake ( Nilitazamia pia katika viwanda vya utengenezaji Mikate ila sijapata Mawasiliano na wakuu wa sehemu hizo)

Natanguliza shukurani........
 
kwa nini usimshauri aende chuo cha ufundi akapate ujuzi hata kidogo
 
ameamua kuishia hapo moja kwa moja? amepata alama gani? haya maswali ni muhimu! Inaonekana wewe una kazi, sasa ndugu yangu ukisema pesa pesa pesa unamaanisha nini, anyway, jibu hayo maswali yangu kwanza then tuone kama anaweza kusaidika.
 
Ok, Alipata division four point 32.
 
kwa hiyo issue sio pesa pesa pesa, ni qualification
Kikubwa ni yeye kupata sehemu ya kupata chochote,kuna watu wana qualification ila hawana pesa za kuwasaidia kusonga mbele mkuu.

Kikubwa apate tu sehemu ambayo ataweza kupata mkate wa kila siku Ndugu.
 
Back
Top Bottom