Nafasi ya Jeshi la Polisi la Tanzania katika viwango vya ubora duniani

Electric Drive

Senior Member
Nov 2, 2016
113
87
NAFASI YA JESHI LA POLISI LA TANZANIA KATIKA VIWANGO VYA UBORA DUNIANI

Ripoti iliyotolewa na World Internal Security & Police Index (WISPI) imeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye Jeshi la Polisi dhaifu barani Afrika na duniani.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa kati ya nchi 127 zilizofanyiwa uchunguzi wa ubora wa Jeshi la Polisi duniani, Tanzania imeshika nafasi ya 110 duniani huku kwa Afrika ikishika nafasi ya 11 kwa kuwa na jeshi dhaifu zaidi.

Ripoti hiyo iliyotolewa na ‘International Police Science Association, (IPSA)’ na Taasisi ya Uchumi na Amani, inahusisha wataalamu, wanazuoni pamoja na watafiti wa masuala ya usalama na ulinzi kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Vigezo viliyotumiwa katika kupata matokeo kutoka nchi hizo 127 vimetajwa kuwa uwezo, mchakato, uhalali na matokeo pamoja na lengo la kupima uwezo wa vifaa vya usalama ndani ya nchi ili kukabiliana na changamoto za usalama wa ndani kwa sasa na baadaye.

Nchi nyingine za Afrika zilizotajwa kuwa na jeshi la Polisi dhaifu zaidi ni pamoja na Madagascar, Zambia, Ethiopia, Sierra Leone, Cameroon, Msumbiji, Uganda, Kenya, Jamhuri ya Afrika ya Kati huku iliyoshika nafasi ya mwisho ikiwa ni Nigeria.

Katika nchi zote 127 zilizofanyiwa utafiti, nchi za Afrika zilizotajwa kuwa na Jeshi la Polisi imara zaidi ni pamoja na Botswana iliyoshika nafasi ya 47 huku nchi ya Rwanda ikitajwa kushika nafasi ya 50.

Nchi nyingine zilizotajwa ni Algeria, Senegal, Tunisia, Egypt, Burkina Faso, Ghana, Afrika Kusini na Mali.

Source:Swahili Times
 
Hivi vyombo vya usalana ilitakiwa visiwe chini ya serikali yaani sijui nisemeje yaani viwe na uwezo wa kuikosoa na kuikemea serikali ila huu mtindo wa kuwa chini ya gov unasababisha kufanya wasiyoyataka
 
Majeshi yote duniani yanapokea amri kutoka kwa kiongozi mkuu wa nchi sio wanasiasa uchwara kama lisu na mboe
 
Rwanda haina jeshi la polisi, inatumia wanajeshi Sawa kabisa na Uganda pia nayo ililalamikuwa kuchukua wanajeshi na kuwapa majukumu ya kipolisi.

Ila nchi yetu iko salama zaidi waache unaaa.

Jambo moja, tunapaswa kuelewa ni kuwa kwa sasa Tanzania inatafutwa sana na kila kikalagosi hasa wazungu koko kutusema vibaya.
 
Kichwa au Heading ilitakiwa iwe wazi kama vazi la Kahaba yaani Jeshi la Polisi maana kuna Majeshi mengine zaidi ya Jeshi la Polisi.
 
Kazi pekee ya jeshi letu la polisi ni kupambana na vyama vya upinzani ili kulinda maslahi ya Sizonje na CCM. Hakuna jingine walijualo.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom