Nafasi ya Jeshi la Polisi la Tanzania katika viwango vya ubora duniani

wacha wewe.. haiwezi kuwa ya mia na kenda!,hivi hukuona wale ffu walivyofanya kazi nzuri baada ya mwenzao kuuliwa mpk wengine wakaja kulalamika humu kwa ile oparesheni! you can't be serious!!
jeshi letu lapolisi wapo vizuri.
 
Rwanda haina jeshi la polisi, inatumia wanajeshi Sawa kabisa na Uganda pia nayo ililalamikuwa kuchukua wanajeshi na kuwapa majukumu ya kipolisi.

Ila nchi yetu iko salama zaidi waache unaaa.

Jambo moja, tunapaswa kuelewa ni kuwa kwa sasa Tanzania inatafutwa sana na kila kikalagosi hasa wazungu koko kutusema vibaya.
Una uhakika?Hivi wale vijana wa Kinyarwanda ambao hujumuishwa na wenzao wa Tanzania kule Police Academy ya Moshi wakirudi kwao huwa wanakuwa akina nani? Kwamba walikuwa wanajeshi si hoja. Hata Tanzania wakati wa Mwalimu kuna baadhi ya JWTZ walipelekwa Polisi ya Tanzania kuliunda upya.
 
Kama Jeshi la Polisi ni dhaifu, kwa nini nchi yetu ina hali ya amani na utulivu kuliko hizo nchi nyingine za Afrika zilizotajwa? Au wanafikiri amani imejileta yenyewe?
Hapa kuna kitu kinatafutwa, sio bure!
Hahahahahaaa! Boss, AMANI siyo lidude fulani kama furushi unalikuta juu ya mti! Amani inaanzia katika jamii ya watu !Watanzania wana asili ya kuongozwa na hofu. Vilevile ,kwa namna tunavyochangamana katika kuishi hatuwezi kuharibu amani iliyopo kwa urahisi. Tumeoleana, tunaishi makabila mchanganyiko, kazini tupo wa aina zote. Hizo sifa za bure unazotaka kuwapa PT unapotosha.
 
Una uhakika?Hivi wale vijana wa Kinyarwanda ambao hujumuishwa na wenzao wa Tanzania kule Police Academy ya Moshi wakirudi kwao huwa wanakuwa akina nani? Kwamba walikuwa wanajeshi si hoja. Hata Tanzania wakati wa Mwalimu kuna baadhi ya JWTZ walipelekwa Polisi ya Tanzania kuliunda upya.

Moisemusajiografii ,

Naelewa ninachokiandika na nimekiishi hapo Rwanda.

Labda nikupe kazi kidogo sana, tafuta muundo wa jeshi la polisi la Rwanda utaelewa.

Ukiupata huo muundo uweke hapa jukwaani nikuoneshe tofauti.
 
NAFASI YA JESHI LA POLISI LA TANZANIA KATIKA VIWANGO VYA UBORA DUNIANI

Ripoti iliyotolewa na World Internal Security & Police Index (WISPI) imeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye Jeshi la Polisi dhaifu barani Afrika na duniani.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa kati ya nchi 127 zilizofanyiwa uchunguzi wa ubora wa Jeshi la Polisi duniani, Tanzania imeshika nafasi ya 110 duniani huku kwa Afrika ikishika nafasi ya 11 kwa kuwa na jeshi dhaifu zaidi.

Ripoti hiyo iliyotolewa na ‘International Police Science Association, (IPSA)’ na Taasisi ya Uchumi na Amani, inahusisha wataalamu, wanazuoni pamoja na watafiti wa masuala ya usalama na ulinzi kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Vigezo viliyotumiwa katika kupata matokeo kutoka nchi hizo 127 vimetajwa kuwa uwezo, mchakato, uhalali na matokeo pamoja na lengo la kupima uwezo wa vifaa vya usalama ndani ya nchi ili kukabiliana na changamoto za usalama wa ndani kwa sasa na baadaye.

Nchi nyingine za Afrika zilizotajwa kuwa na jeshi la Polisi dhaifu zaidi ni pamoja na Madagascar, Zambia, Ethiopia, Sierra Leone, Cameroon, Msumbiji, Uganda, Kenya, Jamhuri ya Afrika ya Kati huku iliyoshika nafasi ya mwisho ikiwa ni Nigeria.

Katika nchi zote 127 zilizofanyiwa utafiti, nchi za Afrika zilizotajwa kuwa na Jeshi la Polisi imara zaidi ni pamoja na Botswana iliyoshika nafasi ya 47 huku nchi ya Rwanda ikitajwa kushika nafasi ya 50.

Nchi nyingine zilizotajwa ni Algeria, Senegal, Tunisia, Egypt, Burkina Faso, Ghana, Afrika Kusini na Mali.

Source:Swahili Times
Vipi hadi somalia wametupita >?
 
Back
Top Bottom