Nafasi ya Jeshi la Polisi la Tanzania katika viwango vya ubora duniani

Jeshi? Kamuulize amini
1978 hadi 2017 imeshapita miaka zaidi ya 39 na hapa halizungumziwi jeshi la Wananchi ambalo kazi yake ni kulinda mipaka ya nchi yetu. Hapa linazungumziwa Jeshi la Polisi.

Jeshi la polisi halikupigana na Idd Amin na kazi yake kubwa ni usalama wa raia na siyo vita. Ukiangalia vigezo vilivyotumika utaona kuna ukweli fulani katika hilo. Kwa mfano ni mara ngapi wananchi wamelalamika kuwa Jeshi la Polisi huwa hawafiki kwa wakati kwenye matukio ya Uhalifu wanapopewa taarifa ya kutokea kwa matukio hayo?
 
Kama Jeshi la Polisi ni dhaifu, kwa nini nchi yetu ina hali ya amani na utulivu kuliko hizo nchi nyingine za Afrika zilizotajwa? Au wanafikiri amani imejileta yenyewe?
Hapa kuna kitu kinatafutwa, sio bure!
 
Jeshi lolote likishakua la kupelekeshwa hata na akina bashite ni hovyo.

Anateuliwa mkuu wa wilaya aliefeli. Anakuja anamuamlisha mtu na minyota yake mabegani
Anatumwa mambo ya hovyo na yeye anakubali bila ya hata ya kuhoji au hata kushangaa hashangai.
Hili ni jeshi la CCM
 
Hivi vyombo vya usalana ilitakiwa visiwe chini ya serikali yaani sijui nisemeje yaani viwe na uwezo wa kuikosoa na kuikemea serikali ila huu mtindo wa kuwa chini ya gov unasababisha kufanya wasiyoyataka
Kwa mfano nchi ipi ina mfumo huo unaoufikiria wewe? Mi sioni mantiki ya ulichokiwaza,unataka viweje labda? Vitumwe na nani kwa minajili ya nani na nini?

Kiutawala na kiuongozi, nchi inagawanyika ktk mihimili mitatu, la kwanza ni Bunge (kutunga sheria) pili ni Mahakama (kutafsiri sheria) tatu ni Serikali (kutekeleza sheria) na ktk kulifanya hili jukumu zito, linatakiwa liwe na vyombo vya dola, hapa nayazungumzia majeshi ya ulinzi na ya Usalama, we ulitaka yawe yanajitegemea ili yafanye yapi labda?

Rais aagize utekelezaji wa sheria au sera yenyewe yapinge? Nini sasa itakuwa maana ya kufanyika kwa uchaguzi na kuwepo kwa sera, irani na itikadi za vyama na wagombea?
 
Rwanda haina jeshi la polisi, inatumia wanajeshi Sawa kabisa na Uganda pia nayo ililalamikuwa kuchukua wanajeshi na kuwapa majukumu ya kipolisi.

Ila nchi yetu iko salama zaidi waache unaaa.

Jambo moja, tunapaswa kuelewa ni kuwa kwa sasa Tanzania inatafutwa sana na kila kikalagosi hasa wazungu koko kutusema vibaya.
Ni mtu wa ajabu sana na wa kipekee sana ambaye, kwa levo tu ya std 7 ataendelea kuishi akidhani mataifa ya kimagharibi wana jambo jema kwa mataifa ya ulimwengu wa tatu, wa ajabu sana. Tangu uhuru, hawa jamaa ni wapingaji wetu kwa kila jema tulitendalo, wameuua Ujamaa ili itikadi zao zionekane ni zenye mashiko, ila hata waliozifuata tangu awali wako wapi kwa sasa?
 
Jeshi linalotumiwa na watawala dhidi ya raia wake ulitegemea lipewe nafasi gani
Jeshi linajipanga na kutunga mbinu ya kudhibiti raia katika kushiriki mambo yao msingi mlitarajia nini?
Mambo ya raia ya msingi ni kama yapi labda? Nani aliyesema hayo ndio mambo ya msingi ya raia wa Tz? Mi nilidhani baada ya kumalizika kwa uchaguzi tu, mambo ya msingi ya raia ni yale tu waliyoyaamua yawaongoze kwa miaka 5, kama walibugi basi watarekebisha baada ya hapo, ndo demokrasia hiyo, sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, wengi wape.
 
NAFASI YA JESHI LA POLISI LA TANZANIA KATIKA VIWANGO VYA UBORA DUNIANI

Ripoti iliyotolewa na World Internal Security & Police Index (WISPI) imeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye Jeshi la Polisi dhaifu barani Afrika na duniani.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa kati ya nchi 127 zilizofanyiwa uchunguzi wa ubora wa Jeshi la Polisi duniani, Tanzania imeshika nafasi ya 110 duniani huku kwa Afrika ikishika nafasi ya 11 kwa kuwa na jeshi dhaifu zaidi.

Ripoti hiyo iliyotolewa na ‘International Police Science Association, (IPSA)’ na Taasisi ya Uchumi na Amani, inahusisha wataalamu, wanazuoni pamoja na watafiti wa masuala ya usalama na ulinzi kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Vigezo viliyotumiwa katika kupata matokeo kutoka nchi hizo 127 vimetajwa kuwa uwezo, mchakato, uhalali na matokeo pamoja na lengo la kupima uwezo wa vifaa vya usalama ndani ya nchi ili kukabiliana na changamoto za usalama wa ndani kwa sasa na baadaye.

Nchi nyingine za Afrika zilizotajwa kuwa na jeshi la Polisi dhaifu zaidi ni pamoja na Madagascar, Zambia, Ethiopia, Sierra Leone, Cameroon, Msumbiji, Uganda, Kenya, Jamhuri ya Afrika ya Kati huku iliyoshika nafasi ya mwisho ikiwa ni Nigeria.

Katika nchi zote 127 zilizofanyiwa utafiti, nchi za Afrika zilizotajwa kuwa na Jeshi la Polisi imara zaidi ni pamoja na Botswana iliyoshika nafasi ya 47 huku nchi ya Rwanda ikitajwa kushika nafasi ya 50.

Nchi nyingine zilizotajwa ni Algeria, Senegal, Tunisia, Egypt, Burkina Faso, Ghana, Afrika Kusini na Mali.

Source:Swahili Times
Ok
 
Ni mtu wa ajabu sana na wa kipekee sana ambaye, kwa levo tu ya std 7 ataendelea kuishi akidhani mataifa ya kimagharibi wana jambo jema kwa mataifa ya ulimwengu wa tatu, wa ajabu sana. Tangu uhuru, hawa jamaa ni wapingaji wetu kwa kila jema tulitendalo, wameuua Ujamaa ili itikadi zao zionekane ni zenye mashiko, ila hata waliozifuata tangu awali wako wapi kwa sasa?

Mkuu, umeandika vizuri.

Ila sasa vijana wanashabikia hata mambo ya kudharaulisha nchi yao hapo utasikia upinzani wanaenda KTN TV station na London kusema "actually" oooh oooh ze ze ze polisi.

Bila kuangalia maslahi mapana ya nchi yetu.
 
Mwiba unapoingilia ndipo unapotolewa!!
 
Kama Jeshi la Polisi ni dhaifu, kwa nini nchi yetu ina hali ya amani na utulivu kuliko hizo nchi nyingine za Afrika zilizotajwa? Au wanafikiri amani imejileta yenyewe?
Hapa kuna kitu kinatafutwa, sio bure!

Wazungu koko, wanatakiwa kuelewa kuwa hata kwao na vifaa vyao tunaona udhaifu mkubwa sana wa vyombo vyao vya ulinzi na usalama.

Mfano, UK kila siku watu wanauawa je hakuna vifaa na polisi imara!?

USA nako ni yaleyale watu wanauawa , polisi inaua watu je nako hako tuseme polisi ni dhaifu na haina vifaa na mbinu za kupambana na wahalifu!?

Mfano, vifo vya viongozi wengi wa juu nchini USA mbona polisi yao haijawahi kutoa taarifa mahsusi kuhusu nani , kwa nini watu wasiojulikana walifanya huo uhalifu!?

September, 11 nayo jeshi la USA lilikuwa imara au dhaifu!?
Tena wale watekaji wa ndege zote wamefanya mchakato ule mzima ndani ya ardhi na Viwanja vya ndege vyao tena na ndege zilizotumika zikiwa za mashirika yao ya ndege!!

Je, hapo polisi yao na vyombo vyao vya ulinzi, vifaa na mbinu zilikuwa imara!?

Ulaya yote , hali ni tête mfano, ubelgiji , ujerumani kote huko matukio mabaya ya kiuhalifu na kiugaidi yanatokea. Je huko nako polisi , vifaa na mbinu ni dhaifu !???

Hapa Middle East, hasa Israel kila siku maelfu ya watu wanauawa je nako polisi ni dhaifu , vifaa vyao na mbinu zao ni duni!?

Wazungu koko waache unafiki waangalie mambo yao na Sisi yetu. Pa kusaidiana tusaidiane ili tusonge mbele kwa pamoja.
 
Mkuu, umeandika vizuri.

Ila sasa vijana wanashabikia hata mambo ya kudharaulisha nchi yao hapo utasikia upinzani wanaenda KTN TV station na London kusema "actually" oooh oooh ze ze ze polisi.

Bila kuangalia maslahi mapana ya nchi yetu.
Maslahi mapana ndio yapi hayo ?! Tunapoambiwa madhaifu yetu tuyafanyie kazi!! Bahati mbaya WaTz tumekaa kisiasa
 
Rwanda haina jeshi la polisi, inatumia wanajeshi Sawa kabisa na Uganda pia nayo ililalamikuwa kuchukua wanajeshi na kuwapa majukumu ya kipolisi.

Ila nchi yetu iko salama zaidi waache unaaa.

Jambo moja, tunapaswa kuelewa ni kuwa kwa sasa Tanzania inatafutwa sana na kila kikalagosi hasa wazungu koko kutusema vibaya.
Wao wameleta data na wewe pinga kwa data sio utuimbie taarab hapa!!
 
Jeshi la polisi kwa sasa ni wakusanya mapato ya serikali... Yani imekua kero kubwa kupita maelezo, Traffic wanalazimisha faini sijajua wanapewa % ngapi kwenye hiyo 30! wamekua wanyama na sio binadamu tena
 
Ni mtu wa ajabu sana na wa kipekee sana ambaye, kwa levo tu ya std 7 ataendelea kuishi akidhani mataifa ya kimagharibi wana jambo jema kwa mataifa ya ulimwengu wa tatu, wa ajabu sana. Tangu uhuru, hawa jamaa ni wapingaji wetu kwa kila jema tulitendalo, wameuua Ujamaa ili itikadi zao zionekane ni zenye mashiko, ila hata waliozifuata tangu awali wako wapi kwa sasa?
Muwapinge kwa mambo mengine lakini hili la Polisi wako sahihi sana labda ujivike miwani ya mbao.
 
Hivi vyombo vya usalana ilitakiwa visiwe chini ya serikali yaani sijui nisemeje yaani viwe na uwezo wa kuikosoa na kuikemea serikali ila huu mtindo wa kuwa chini ya gov unasababisha kufanya wasiyoyataka
Wazo zuri,je raia tuko tayari kuwalipa?
 
Ripoti hiyo imeeleza kuwa kati ya nchi 127 zilizofanyiwa uchunguzi wa ubora wa Jeshi la Polisi duniani, Tanzania imeshika nafasi ya 110 duniani huku kwa Afrika ikishika nafasi ya 11 kwa kuwa na jeshi dhaifu zaidi.

Hawa ndugu wamejikita zaidi kwenye kujineemesha wao na siyo raia na mfano mzuri ni wale wa usalama barabarani, wanapokea rushwa bila hata woga, huruma na aibu
 
Back
Top Bottom