Nafasi ya Jeshi la Polisi la Tanzania katika viwango vya ubora duniani


E

Electric Drive

Senior Member
Joined
Nov 2, 2016
Messages
113
Likes
86
Points
45
Age
41
E

Electric Drive

Senior Member
Joined Nov 2, 2016
113 86 45
NAFASI YA JESHI LA POLISI LA TANZANIA KATIKA VIWANGO VYA UBORA DUNIANI

Ripoti iliyotolewa na World Internal Security & Police Index (WISPI) imeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye Jeshi la Polisi dhaifu barani Afrika na duniani.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa kati ya nchi 127 zilizofanyiwa uchunguzi wa ubora wa Jeshi la Polisi duniani, Tanzania imeshika nafasi ya 110 duniani huku kwa Afrika ikishika nafasi ya 11 kwa kuwa na jeshi dhaifu zaidi.

Ripoti hiyo iliyotolewa na ‘International Police Science Association, (IPSA)’ na Taasisi ya Uchumi na Amani, inahusisha wataalamu, wanazuoni pamoja na watafiti wa masuala ya usalama na ulinzi kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Vigezo viliyotumiwa katika kupata matokeo kutoka nchi hizo 127 vimetajwa kuwa uwezo, mchakato, uhalali na matokeo pamoja na lengo la kupima uwezo wa vifaa vya usalama ndani ya nchi ili kukabiliana na changamoto za usalama wa ndani kwa sasa na baadaye.

Nchi nyingine za Afrika zilizotajwa kuwa na jeshi la Polisi dhaifu zaidi ni pamoja na Madagascar, Zambia, Ethiopia, Sierra Leone, Cameroon, Msumbiji, Uganda, Kenya, Jamhuri ya Afrika ya Kati huku iliyoshika nafasi ya mwisho ikiwa ni Nigeria.

Katika nchi zote 127 zilizofanyiwa utafiti, nchi za Afrika zilizotajwa kuwa na Jeshi la Polisi imara zaidi ni pamoja na Botswana iliyoshika nafasi ya 47 huku nchi ya Rwanda ikitajwa kushika nafasi ya 50.

Nchi nyingine zilizotajwa ni Algeria, Senegal, Tunisia, Egypt, Burkina Faso, Ghana, Afrika Kusini na Mali.

Source:Swahili Times
 
mlimilwa

mlimilwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
2,077
Likes
1,371
Points
280
mlimilwa

mlimilwa

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
2,077 1,371 280
Jeshi lolote likishakua la kupelekeshwa hata na akina bashite ni hovyo.

Anateuliwa mkuu wa wilaya aliefeli. Anakuja anamuamlisha mtu na minyota yake mabegani
Anatumwa mambo ya hovyo na yeye anakubali bila ya hata ya kuhoji au hata kushangaa hashangai.
 
Seaman86

Seaman86

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Messages
370
Likes
391
Points
80
Seaman86

Seaman86

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2017
370 391 80
Hivi vyombo vya usalana ilitakiwa visiwe chini ya serikali yaani sijui nisemeje yaani viwe na uwezo wa kuikosoa na kuikemea serikali ila huu mtindo wa kuwa chini ya gov unasababisha kufanya wasiyoyataka
 
Root

Root

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Messages
28,382
Likes
15,415
Points
280
Root

Root

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2012
28,382 15,415 280
Vigezo gani htumika
 
S

songera

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2014
Messages
1,290
Likes
449
Points
180
S

songera

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2014
1,290 449 180
Majeshi yote duniani yanapokea amri kutoka kwa kiongozi mkuu wa nchi sio wanasiasa uchwara kama lisu na mboe
 
Allen Kilewella

Allen Kilewella

Verified Member
Joined
Sep 30, 2011
Messages
8,929
Likes
13,699
Points
280
Allen Kilewella

Allen Kilewella

Verified Member
Joined Sep 30, 2011
8,929 13,699 280
Soma tena vigezo vimewekwa ambavyo ni; Uwezo,mchakato,uhalali, uwezo wa vifaa katika kukabiliana na changamoto za uhalifu katika nchi husika!
 
Allen Kilewella

Allen Kilewella

Verified Member
Joined
Sep 30, 2011
Messages
8,929
Likes
13,699
Points
280
Allen Kilewella

Allen Kilewella

Verified Member
Joined Sep 30, 2011
8,929 13,699 280
Majeshi yote duniani yanapokea amri kutoka kwa kiongozi mkuu wa nchi sio wanasiasa uchwara kama lisu na mboe
Kwa ulichoandika kuna kilichobadilika kwenye huo utafiti?
 
Poise

Poise

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2016
Messages
7,471
Likes
7,480
Points
280
Poise

Poise

JF-Expert Member
Joined May 31, 2016
7,471 7,480 280
Rwanda haina jeshi la polisi, inatumia wanajeshi Sawa kabisa na Uganda pia nayo ililalamikuwa kuchukua wanajeshi na kuwapa majukumu ya kipolisi.

Ila nchi yetu iko salama zaidi waache unaaa.

Jambo moja, tunapaswa kuelewa ni kuwa kwa sasa Tanzania inatafutwa sana na kila kikalagosi hasa wazungu koko kutusema vibaya.
 
Cannibal OX

Cannibal OX

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2014
Messages
2,331
Likes
2,452
Points
280
Cannibal OX

Cannibal OX

JF-Expert Member
Joined Aug 27, 2014
2,331 2,452 280
Kichwa au Heading ilitakiwa iwe wazi kama vazi la Kahaba yaani Jeshi la Polisi maana kuna Majeshi mengine zaidi ya Jeshi la Polisi.
 
MAWAZO UJENZI

MAWAZO UJENZI

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
2,002
Likes
1,054
Points
280
MAWAZO UJENZI

MAWAZO UJENZI

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
2,002 1,054 280
Mi ningeshauri makamishna wote wa kanda maalum, wangepimwa mkojo kabla ya kuteuliwa, maana huwa ni waongo balaa
Mtangulizi wa Sirro aka Macho manne,macho kumuchuzi,alikua mzee wa sound hatari sana
 
Mamndenyi

Mamndenyi

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
29,388
Likes
7,438
Points
280
Mamndenyi

Mamndenyi

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2011
29,388 7,438 280
Jeshi? Kamuulize amini
 
Mdudu halisi

Mdudu halisi

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2014
Messages
2,609
Likes
4,160
Points
280
Mdudu halisi

Mdudu halisi

JF-Expert Member
Joined May 7, 2014
2,609 4,160 280
Kazi pekee ya jeshi letu la polisi ni kupambana na vyama vya upinzani ili kulinda maslahi ya Sizonje na CCM. Hakuna jingine walijualo.
 
KweliKwanza

KweliKwanza

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2016
Messages
3,072
Likes
2,224
Points
280
Age
25
KweliKwanza

KweliKwanza

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2016
3,072 2,224 280
Mwalimu aliesomea degree anaenda kukabidhiwa kikosi kisa2 maisha yamempiga vilivyo mbele ya vita anakua muoga kama mbwa koko. Mkurya mwenye ujasili wake wanamuacha mbali
 
kenstar

kenstar

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2015
Messages
2,304
Likes
1,398
Points
280
kenstar

kenstar

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2015
2,304 1,398 280
Ndio kusema tuombe ulinzi toka mkoa wa Luanda
 
Allen Kilewella

Allen Kilewella

Verified Member
Joined
Sep 30, 2011
Messages
8,929
Likes
13,699
Points
280
Allen Kilewella

Allen Kilewella

Verified Member
Joined Sep 30, 2011
8,929 13,699 280
Jambo moja, tunapaswa kuelewa ni kuwa kwa sasa Tanzania inatafutwa sana na kila kikalagosi hasa wazungu koko kutusema vibaya.
Kwani huo utafiti umeihusisha Tanzania peke yake?
 

Forum statistics

Threads 1,236,317
Members 475,099
Posts 29,254,087