Nafasi ya JamiiForums katika kuwahudumia watoto wenye ulemavu wa akili

JOSIA PATRICK

New Member
Jul 24, 2021
4
2
Kumekuwa na mtazamo tofauti katika kuwahudumia Watoto wenye ulemavu wa akili ambapo jamii nyingi zimekuwa na mtizamo tofauti ambao sio mzuri ambapo huchangiwa sana na kukosa elimu. Ambapo hupelekea kuwanyanyasa na kuwatenga Watoto wenye ulemavu hupeleka hadi muda mwingine kuacha hata kuwapa mahitaji yao muhimu kutokuwapa hata haki zao.

Mtazamo ambao upo kwa sasa sio mzuri kwani wazazi wengi wanaohudumia Watoto wenye ulemavu wa akili wanakosa hata muda wa kufanya shughuli zao mbalimbali za kiuchumi kwa sababu tu wanakosa ushrikiano kwenye jamii muda mwingine kushindwa hata kuwaacha Watoto na watu wengine kwa sababu mbalimbali za unyanyasaji na ukatili ambao wanapitia wazazi Pamoja na Watoto wao.

Asilimia kubwa ya wazazi wanaohudumia Watoto wenye changamoto wanapitia mambo mengi sana ikiwemo msongo wa mawazo uliopitiliza hadi muda mwingine hupelekea wazazi kupata changamoto mbalimbali ikiwemo AFYA YA AKILI hii yote inatokana na mambo mengi wanayo pitia ikiwemo unyanyasaji na kukataliwa na jamii kupewa maneno mabaya yenye kukatisha tamaa na kutengwa.

Elimu kwa jamii iko wapi katika suala ili?
Ulemavu wa akili husababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo kabla ya mtoto kuzaliwa, Baada ya mtoto kuzaliwa. Wakati wa mtoto kuzaliwa. Na sio Imani za kishirikina kama ambavyo watu wengi wanakuwa wakifikiri inapaswa jamii kuamka na kuangalia ni kwa namna gani tunaweza kusaidia Watoto wenye ulemavu wa akili Pamoja na kuangalia pia namna gani tutaweza kusaidia wazazi kuondokana na msongo wa mawazo na kuangali ni namna gani tunaweza kuwasaidia ili kuweza kulata Faraja kwa wazazi Pamoja na Watoto.Kupitia hivyo kwa Pamoja tunaweza kujenga taifa lilibora.
 
ELIMU ZAIDI YA SERIKALI NA NGO'S kwenda kwa jamiii inahitajika sana maana wengi wetu hatuna muamko mzuri juu ya suala hili
 
Elimu ni muhimu sana haswa kwa jamii maana watu wanamtazamo tofauti sana kuhusu ulemavu
Wengi wetu tunawatenga na kuwaona hawafai kitu ambacho sio sahihi.... tunajisahau kuwa na sisi wazima ni walemavu watarajiwa iwe kwa akili au viungo
 
Back
Top Bottom