SoC02 Nafasi ya elimu ya Tanzania katika kuzalisha wataalamu wa Kiswahili duniani

Stories of Change - 2022 Competition

Baker mwinyi

New Member
Jul 22, 2022
1
1
Kiswahili ni miongoni mwa lugha za kibantu zinazokua kwa kasi barani Afrika na duniani kwa ujamla ikiwa na watumiaji zaidi ya milioni 120 Kama alivyosema Audrey Azoulay " ikiwa na wazungumzaji kati ya milioni 120 na 150 ,lugha ya kiswahili ni moja ya lugha zinazoshamiri kuvuka mipaka ya kule inamozungumzwa.Lugha ya kiswahili ina maneno kutoka kusini mwa Afirka,Uarabuni na India". (news.un.org.) Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO limetoa msukumo mkubwa katika kufufua na kuchagiza hamasa ya kukuza na kueneza lugha ya kiswahili duniani kwa kutanganza kuwa siku ya 07/07 ni siku ya kiswahili duniani. Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inahitaji kufanya jitahada za makusudi katika kuunga mkono harakati hizo licha ya kuwapo hatua za awali nchini Tanzania kuhakikisha kiswahili kinakuwa katika nyanja zote za maisha ikiwemo uchumi, siasa na elimu .


Nafasi ya elimu katika kuzalisha wataalamu.

Serikali ina nafasi ya kuzalisha wataalamu wa kutosha wa lugha ya kiswahili kuanzia ngazi za awali na sekondari ili kukidhi soko la kitaifa na kimataifa kwa kuhakikisha kiswahili ndio lugha ya kufundishia na mawasiliano katika ngazi zote za elimu, vitabu vya masomo yote vichapishwe kwa lugha ya kiswahili kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa Elimu na taassisi za lugha ya kiswahili kama vile BAKITA na BAKIZA na kuondoa kasumba ya kwamba kiswahili hakina msamiati wa kutosha kukidhi mahitaji hayo ,kwani kila lugha hujitosheleza kwa kadri ya matumizi ya watumiaji wake na zipo njia nyingi za kuongeza msamiati wa lugha mathalani kukopa maneno kutoka lugha nyingine na kuyasanifisha lengo ni kuondoa mkanganyiko na sintomfahamu kwa wanafunzi kwani hata vitabu vya masomo vilivyo kwa lugha ya kiingereza huwa vinafundishwa na walimu kwa kuchanganya lugha (code mixing and code switching) na muda mwingine kwa kufanya tafsiri moja kwa moja, katika hilo lipo la kujifunza kwa wazawa wa lugha Kama vile kifaransa na kichina ambapo vitabu vyao vya taaluma kwa kiasi kikubwa vipo katika lugha zao mama (lugha zao za kwanza) Jambo linaloakisi uzalendo na kusaidia kukua kwa lugha hizo . Kimsingi zipo mbinu nyingi za kufundisha kiswahili kwa wageni kwa kutumia kiswahili chenyewe lakini katika kuleta ufanisi yapo marekebisho ya msingi yanayopaswa kufanyika katka mitaala ambayo ipo kwa ajili ya kuwaandaa wataalamu wa kiswahili duniani kutokea nchini Tanzania mfano kwa wataalamu tunao waandaa kufundisha kiswahili nje ya nchi inabidi wawe na ujuzi wa kufundisha kiswahili na wawe na utambuzi wa angalau lugha moja ya kigeni mfano katika mtaala mtu anaendaliwa kuwa mtaaalamu wa kiswahili asome na kichina , au kiswahili - kifaransa au kiswahili - kireno hivyo itakuwa rahisi kwake kuwafundisha watu hao huku kiingereza kikibaki kuwa ni lugha ya lazima kukifahamu kwa kufanya hivyo wataalamu wetu wa kiswahili wataweza kufundisha nchi zote ambazo zinazungumza lugha hizo yaani ndani na nje ya bara la Afrika . ( Anglo-phone, Franco-phone and lusophone countries).


Nafasi ya Bodi ya Mikopo Tanzania (HESLB).

Kimsingi hatuweza kuizungumzia elimu ya Tanzania na kuweka kando bodi ya mikopo.Bodi ya mikopo (HESLB) itoe kipaumbele kwa wanafunzi wa kiswahili kama ilivyo kwa wanafunzi wa masuala ya Afya na masomo mengine yanayopewe kipaumbele katika nchi, mfano wizara ya elimu imejipanga kutoa ufadhili wa masomo (Schoolarship) kwa wanafunzi wa michepuo ya sayansi iwapo watapata alama ' A ' katika masomo yote hivyo hivyo kwa wanafunzi watakaopata Alama 'A 'katika masomo ya lugha na kuonyesha umahiri wa hali ya juu kwenye lugha ya kiswahili na wenye vigezo stahiki vya kupata ufadhili wa masomo ambavyo vitawekwa na serikali na wadau wengine wa elimu hasa katika taaluma za lugha; juu ya hayo serikali kwa kushirikiana na bodi ya mikopo ianzishe mkakati wa kutoa Ufadhili na mikopo ya ziada kwa wanafunzi wanaotaka kujiendeleza shahada ya pili na ya tatu na kuwaweka mkakati wa namna bora ya kulipa madeni hayo kwani wanafunzi wengi wanakwama kupata mikopo kutoka bodi ya mikopo sababu ya kuwa na deni la awali yaani shahada ya Kwanza, kama haitoshi bodi ya mikopo isitegemee ruzuku kutoka serikalini pekee katika kuwafadhili wataalamu tarajali wa lugha ya kiswahili badala yake kwa kushirikiana na serikali watafute vyanzo vingine vya fedha ili kuwasomesha wataalamu hao mfano kwa kushirikiana na mashirika Kama vile Benki ya Dunia, Benki ya Afrika na wafadhili wengine Kama vile Umoja wa Ulaya ili kuchangamkia fursa za kiswahili barani Afirika na duniani kwa ujumla kwani hivi karibu nchi Kama Uganda nazimeonesha njia ya kufanya somo la kiswahili kuwa la lazima na hivyo ni fursa ya wataalamu wa Tanzania katika kwenda kufundisha kiswahili na wataalamu tulonao inabidi tuweze kuwakomaza katika taaluma za lugha hii ili waweze kushindana na wataalamu wa nchi nyingine katika soko la kimataifa .


Mchango wa Vyuo vikuu Vya Tanzania .

Vyuo vikuu nchini Tanzania navyo vina nafasi ya kukuza kiswahili duniani kwa kuwa na ufadhili wa masomo kutokana na vigezo watakavyoviweka kadri ya sheria na taratibu za vyuo hivyo lakini ni katika ngazi za juu katika mifumo ya elimu kama vile shahada za uzamiri na uzamivu kwa masomo ya kiswahili ili kutoa fursa pana ya watanzania hasa walimu wa kiswahili kuijiendeleza na kujiweka katika soko la kimataifa kama walimu waliobobea katika ufundishaji wa lugha ya kiswahili kimataifa, pia kuandaa matamasha na maonyesho makubwa na makala mbalimbali yatakayofadhiliwa na vyanzo vya ndani vya vyuo hivyo na kuwaalika wadau mbali mbali ndani na nje ya nchi na kwa kushirikiana kwa ukaribu na vyuo vingine duniani vinavyofundisha lugha ya kiswahili duniani kote Kama haitoshi kuwe Kuna kawaida ya kubadilishana uzoefu wa namna ya kufundisha kiswahili mfano wataalamu wa Tanzania wanaweza kwenda kuchukua uzoefu kutoka Kenya na Kenya wakaja kuchukua uzoefu katika vyuo vya Tanzania Kama haitoshi iundwe taasasi huru miongoni mwa vyuo hivyo mahususi katika kukipeleka kiswahili duniani na kukitanganza kwa dhati.
 
Hapa tukikazania sana tunaweza kuzalisha ajira nyingi sana maana kiswahili kinaenea kwa Kasi sana duniani kote
 
Back
Top Bottom