Nafasi tano (05) za Afisa masoko na mauzo wa viwanja- J2 Real Estate

Manala An Academician

Senior Member
Oct 10, 2016
118
54
1. Utangulizi
J2 Real Estate inahusika na utoaji wa mafunzo ya udereva, uuzaji wa viwanja, huduma za usafi na upulizaji wa dawa. Ofisi zake ziko Goba, DSM

2. Nafasi za kazi
Tunawatangazia watanzania wenye sifa na uzoefu nafasi za afisa mauzo na masoko wa miradi ya viwanja, mashamba na nyumba zilizochini ya kampuni.

Sifa
-Uwezo mzuri wa kuongea na kushawishi wateja
-Uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutafuta wateja

-Uwezo wa kufanya kazi yenye matokeo bila usimamizi wowote

-Uzoefu katika kazi za masoko hasa zinazohusiana na viwanja zitazingatiwa zaidi

-Elimu kuanzia kidato cha nne

-Uwezo wakufanya kazi yenye matokeo bila usimamizi

Mshahara

Kutakuwa na malipo ya aina tatu kwa- mwezi kama ifuatavyo

A. TZS 600,000/- (kama mfanyakazi atavuka lengo la mwezi)

B. TZS 400,000/- (kama mfanyakazi atafika lengo la mwezi)

C. TZS 150,000/- (kama mfanyakazi hatofikia lengo la mwezi)

3. Utaratibu wa kuomba maombi

Maombi yatumwe kwa- WhatsApp number 0765374146 na kupitia email: manager@flydream.co.tz

4. Mwisho
Maombi yatapokelewa mpaka jumatano ya tarehe 07/09/2022 saa 11:59 usiku
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom