Nafasi mbili za kazi - PHP Developers

Jan 21, 2011
11
0
Je wewe ni Computer Programmer? Nafasi mbili za kazi hizi hapa.

Nitaandika kwa lugha ya nyumbani.
Kampuni ya E-Fulusi Africa (T) Ltd iliyopo Dar Es Salaam, imebobea katika nyanja za kutengeza systems hasa za Mobile Banking, Payment Systems, SMS projects n.k. Njoo ufanya kazi na vijana machachari kwenye uwanja huu, huku unapata donge nono na fursa nyingi sana za kukuza uwezo wako.

Karibu kama wewe ni “PHP developer “, njoo tuzungumze.
Tunakuhitaji kama tu:
  1. Unafahamu PHP, Java, Javascript, Jquery, Mysql (ushindani ni mkubwa, inabidi ujue hasa!!).
  2. Unaweza na umezoea kutumia Linux.
  3. Una maarifa kuhusu (lazima!!) IP networking, Network analysis, performance and application issues.
  4. Una uzoefu walau wa mwaka mmoja tu kwenye hayo masuala hapo juu itapendeza zaidi.
  5. Vingine ukiwa navyo vitafanya tupendelee kuwa nawe na si wenzako: Mfano: XML/RPC, Web Services(JaxWS), REST, JSON, CodeIgnigter frame work, Ruby and Shell.
Karibu ufanye kazi nasi.
Andika na tuma CV kwenda: rmushi [at] efulusi.com.
Waombaji wote watajibiwa.
Tembelea www.efulusi.com upate mwangaza wa kazi zetu…
 
What's the "dongo nono"? (provide a range at least) What are the "nafasi nyingi za kukuza uwezo?", be clearer.
 
wewe mushi acha usengerema wako, maguya mwenyewe alikukamata C leo, eti unataka kuajiri watu wenye ujuzi wa c programmining, kwanza kimeo chako cha maguya umekiclear kweli? usitake lutuibia wazee wama PHP tumelia hatuongei,
 
wewe mushi acha usengerema wako, maguya mwenyewe alikukamata C leo, eti unataka kuajiri watu wenye ujuzi wa c programmining, kwanza kimeo chako cha maguya umekiclear kweli? usitake lutuibia wazee wama PHP tumelia hatuongei,

Maguya? Iitakuwa umechanganya, akina Mushi wapo wengi sana.
 
Tunashukuru tumepata vijana wawili watakaoungana nasi. Hatutapokea maombi zaidi hadi wakati mwingine kwa nafasi nyingine. Ahsanteni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom