Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Wiki iliyopita mitandaoni kulikuwa na habari za nafasi kumi ambazo kikatiba mheshimiwa Rais anazo.
Yaliibuka maneno mengi kuhusiana na wabunge sita kati ya nane ambao tayari wameshateuliwa, kuwa ni wanaume na wawili tu ndio wanawake.
Lakini uamuzi wa mheshimiwa Abdallah Possi kuteuliwa kuwa balozi, umepunguza idadi ya wabunge wanaume waliokwisha teuliwa, na kubakia watano. Na akateuliwa Mama Anna Kilango, ambaye ameongeza idadi ya wabunge wanawake na kufikia watatu.
Kwa sasa wapo wanane, lakini tukumbuke kuwa kuna masuala ya mtu kushindwa kuzalisha kile alichotegemewa akizalishe siku alipoteuliwa. Kuna masuala ya kuugua kwa mbunge na kushindwa kuendelea na kazi.
Hizi nafasi kumi haziwezi kuwa zinao wabunge kumi kwa wakati mmoja. Baadhi yetu tulisahau kuwa uteuzi wa wabunge hawa kumi huendana na mahitaji maalum, yanayojitokeza ndani ya muda fulani.
Mfano Mheshimiwa Possi kateuliwa kuwa balozi, kesho mwingine katika hao wabunge wanane waliobakia, anaweza kupewa kazi nyingine maalum na nafasi yake ikachukuliwa na mbunge mwanamama.
Ni vigumu kuvunja katiba kwenye suala la uteuzi wa wabunge kumi kwa kigezo cha wanaume kupendelewa zaidi ya wanawake, kwani Rais anayewachagua hajapewa mipaka ya muda kwenye uteuzi wao.
Maadam idadi ya wabunge kumi inakuwa haijatimia, basi kwenye kundi la wanaokuwepo, wanaweza kuingizwa na kutolewa, iwapo inaonekana kuwa umuhimu wa kufanya hivyo upo.