Nafanya kazi lakini nahisi kama nimeshafukuzwa

Anza kutafta kazi hiyo ni taa nyekundu,inawezekana kampuni imekuwa ya undugu na wewe sio miongoni,kikubwa endelea kufanya kazi huku ukitafta kazi
 
Kama hujawahi kuomba likizo Omba sasa kama ni ya mwezi au nusu mwezi. Kwenye likizo hiyo jaribu kufanya mambo yako kama kuomba kazi kwa nguvu na kuanzisha biashara ndogo ndogo. Iwe likizo kweli uwe mbali na ofisi. Itakusaidia akili yako kujua kuwa kunamaisha nje ya kampuni iyo. Yakibuma rudi kazini. Uwe unaomba likizo mkuu. Likizo ni muhimu kwa afya ya akili!
Fata huu ushauri, maana mbali ya kujipima wewe kama wewe; Vilevile kutapelekea mwajiri wako kuona "potential" yako eneo la kazi, in essence mambo lazima yalale kidogo/kwa muda.

All in all, tambua kuna maisha nje ya "hiyo kazi". Kuliko kuwa mtumwa, ni bora ukaachia ngazi; kama ipo ipo tu - ridhiki popote.

All the best
 
Habari Wana jukwaa?

Kampuni ninayofanyia kazi nina miaka mitano kasoro Sasa. Wakati naanza kazi kulikuwa hakuna hesabu. Iliyowahi kufungwa maana kazi yangu ni ya kihasibu. Nimepambana kwasasa kuna hesabu zilizokaguliwa za miaka sita.

Mwanzoni tulikubaliana salari kiasi kwa maelewano kwamba nitaongezewa. Lakini baada ya pale kazi zimekuwa nyingi lakini Boss akagoma kabisa kuongeza.
Nilipoona kazi zinanizidi na mshahara ni mdogo nikamwambia aniongezee mtu mmoja. Akamamleta mtu akampa mshahara Mara mbili ya mshahara wangu lakini jamaa hakuwa na muda maana anachelewa kufika kazini au akaamua haji ndani ya wiki anaweza kuja Mara tatu au mbili hivyo kazi ikawa bado inaniangalia Mimi tu na jamaa kila akija ni mgeni hajui kinachoendelea. Sikutaka hata kumsemea kwa Boss niliendelea kukomaa na hali yangu.

Mwajiri akaamua kumwajiri mzee mmoja rafiki yake akamlipa Mara tatu ya mshahara wangu na nyumba akampa lakini Mimi Wala hataki kuniongezea hivyo nikawa namuelekeza huyu mzee ambaye kimsingi alipewa kuwa Boss wangu.

Ikapita muda akamwajiri mtu mwingine raia wa India akamlipa Mara 6 ya mshahara wangu, nyumba na gari.

Juzi tu akamwajiri mtu mwingine naye ni mzee akamlipa Mara mbili ya mshahara wangu!

Sasa tupo watano wao ni over 40 Mimi ni under 40 wote wananizidi mshahara lakini kila kitu wananitegemea Mimi niwaelekeze.

Wao wenyewe wananiambia nikosana nini na mwajiri mbona ananifanyia hivyo!

Kiukweli Mimi nimevunjika moyo kabisa na sielewi kinachoendelea na kwanini mwajiri ananifanyia hivyo!

Naona ule msemo usemao akufukuzae hakuambii toka.

Kweli natamani niondoke lakini nategemewa na familia ya mke na watoto kadhaa naona kuacha kazi kabla sijapata kazi naona nitaionea familia yangu.

Ebu wadau mniambie kwanza kisaikolojia huyu mwajiri ananipa ujumbe gani Mimi? Na bado kila kitu ananiambia nifanye yaani haoneshi kama hanitaki.

Pia nipeni ushauri niweze kufanya maamuzi sahihi! Please!!
Mimi kwa ushauri wangu anza maombi ya mfungo utaona matokeo. Mambo mengine sio ya mwilini na inawezekana mwajiri anatumika tu hata yeye hajui kwanini anakufanyia hivyo. Chunguza background yako, kwenu familia uchumi mkoje kisha fanya maamuzi anzia hapo
 
Kuna mabosi vichomi, Mimi niligoma kuajiriwa bora nife masikini!
Kuna mabosi vichomi, Mimi niligoma kuajiriwa bora nife masikini!
Kuna maboss huwa hawafikirii mbali..yani boss anaamua tu kukukomoa hujamkosea,uwezo ujuzi unao ila basi anaamua,huwa wanadhani waliowaajiri na kuwanyanyasa watawafanyia hivo siku zote wanashindwa kufikiri kuna Leo na kesho si ajabu kampuni ikafa na watoto wao wakaja kuomba msaada...aloo japo so vyema kulipa kisasi anikute anga zangu lazma nimualert kuwa nliwahi fanyiwa ukatili na baba ake au mzazi wake
 
Onyo, usiache kazi , mkopo kakupa sh ngap ili Wana apa wakupe Raman au una mpango gani na huo mkopo
 
Onyo, usiache kazi , mkopo kakupa sh ngap ili Wana apa wakupe Raman au una mpango gani na huo mkopo
Mkuu kuacha kazi hadi nipate kazi nyingine. Mkopo amenipa lakini nimeshatumia maana nilipoona sintofahamu hiyo ilibidi nijihami kwa kujenga makazi ya familia yangu ili hata ikitokea ananiondoa nisipange.
 
As long umesema kwamba hao 40+ wote wanakutegemea wewe simple chukua likizo ya mwezi mzima automatic gape lako litaonekana

Then changamoto zitakazoonekana kwasababu ya wewe kutokuwepo ofsn ndio gape la ww kuomba salary increase

Akigoma hapo sasa maamuzi juu yako ubakie uendelee kuteseka ama usepe ukaanze upya
Chukua ushauri huu , ufanyie kazi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom