Naendelea ku-enjoy mitindo na matambo ya wanasiasa wetu

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
Naendelea ku-enjoy mitindo na matambo ya wanasiasa wetu. Naendelea pia ku-enjoy kuona wanasiasa wakifanya kazi za kipolisi na kiintelijensia, kwa mitindo ya filamu za maigizo. Nasubiri siku waje kutusaidia kutibu watanzania huku mahospitalini. Wanasiasa wetu wanajua kila kitu.
Hii vita nimejiridhisha kwamba! Ni vita kati ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya na vibaraka wao, dhidi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya na vibaraka wao, inayopiganwa chini ya anga la siasa.

Vifaranga vitaminywaminywa na mapapa yatachubuana. Nawaona vijana wa pale Jo'burg, mitaa ya Rissik na Bree wakiwaza namna ya kurudi nyumbani. Nawaona wakiulizana; Boss katajwa? Bado. Hatajwi, kama hakutajwa Agnes kwa sababu ya wowowo lake, atatajwa boss?
 
Hiyo ndo Tanzania tunayoishi, tumepiga mark time, tukijidhania tunakwenda mbele. Ajabu wasomi wengi wanaochangia humu, wanashangaza unajiuliza wazazi wao waliwapeleka shule ili iweje. Maana hawajitambui wamelewa na maneno yasiyo na tija ya wanasiasa wetu.
 
Wauzaji kwa sasa wanasikilizia tu upepo wametulia tu kwenye viyoyozi vivuli vyao ndio vipo kazini kwa sasa wakichomoza wenyewe sijui itakuaje ngoja tuone itaishia wapi
 
Back
Top Bottom