Nadiriki kusema: 70% ya waTanzania tumeshaugua na kupona Corona zaidi ya mara tatu au zaidi bila kujua, nadharia ni hii

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,045
40,705
Nimejaribu kukusanya ushahidi wa mdomo (word of mouth) toka kwa watu wengi sana kuhusu homa za mafua walizopata watu kipindi cha mwaka jana mwishoni na mwaka huu mwanzoni, ambapo hata mimi niliumwa, ukiangalia dalili walizopata na jinsi mafua yake yalivyokuja katika timing ile ile ya mlipuko wa China na waChina kurudi kutoka China (China new year) naanza kuona kabisa wengi tuliugua Corona muda ule, ila hatukujua.

Pia wizara ya afya ilitoa tangazo kwamba pametokea mfululizo wa mafua makali yanayosababishia watu homa ila wakasema sio mlipuko, kipindi hicho hakuna aliyejua kuhusu Corona, maana waChina walificha.

Wiki 2 zilizopita nikapata tena homa ya mafua na kukohoa iliyoambatana na kichwa kuuma na mwili kuchoka, haraka sana nikakimbilia dawa ninazozijua mimi, baada ya siku 2 tu nikapona kabisa, sikutaka kujua naumwa nini, ila nikapona, na kuna watu wengine kama 10 wamenipa story za kuumwa na kujitibu kwa njia wanazozijua wenyewe, wengi wanaogopa karantini.

Na pia nimesikia kwa ‘word of mouth’ toka kwa wafiwa wa waliokuwa wagonjwa wa Corona, unakuta kila mfiwa anakwambia ndugu yake alikuwa anakisukari, kama sio hicho basi alikuwa anashmbuliwa moyo miaka mingi, hivi vitu viwili naona ndio tatizo hasa, Corona ni kama inawamalizia tu.

Sasa mamlaka za utafiti wa kitabibu kama NIMRY ziingie kazini na kuona kama wanaweza kudhibitisha au kukanisha dodoso hili.

Nimetimiza wajibu wangu.
============================
D0B14C3A-2007-41FA-8825-B8AD5ACEEE50.jpeg

Update: 13/05/2020

NAMANGA: Madereva 23 toka Tanzania wamezuiliwa kuingia Kenya baada ya kukutwa na COVID-19 - JamiiForums
 
Mimi kwa dalili za covid19 walizozisema zilinipata wiki tatu zilizopita nikiwa dar es salaam nikapiga strong antibiotics plus kutafuna vitunguu dalili zote zikapotea nahisi ilikua covid dalili zote nilkua nazo nilijikarantin na kufanya social distancing kimya kimya bila wananzengo kujua pia mazoezi ya kukimbia ni muhimu (jogging)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hoja yako ina maana sana.
Katikati ya January mpaka mwanzoni mwa February 2020, kulikuwa na mlipuko wa kikohozi na mafua makali sana ambayo yalikuwa yakisababisha homa kali sana.
Kwa sisi tulio kwenye sekta za afya hasa maabara tunaweza kukupa uthibitisho wa vipimo vingi ambavyo vilioyesha negative kwa malaria/typhoid lakini wagonjwa walikuwa na mafua mmakali kikohozi na maumivu ya kichwa.
Wengi walipewa dawa za kutuliza maumivu na kushusha homa pamoja na dawa za kikohozi.
Ni vile tu taasisi zetu ni dhaifu katika documentation lakini kuna ushahidi wa wazi wa kuwepo kwa ulichokisema.
Asante kwa kuchukua muda wako na kuandika haya.
 
Sisi wa kanda ya ziwa 90% mwezibwa kwanza tulipata hiyo kitu na kupona ndani ya wiki mbili,mimi binafsi nilikua naamka usiku kwenda kuwasaidia watoto namna kupata upumuaji mzuri maana mafua yalikua yamewabana hakuna mfano,mimi na wife pia jinsi tulivyokua tunahangaika ndo ilinifanya nisilale niwe natazama watoto muda wote. ni kweli kabisa hii kitu tutakua tuliipata na kupona

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Back
Top Bottom