OMOYOGWANE
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 4,459
- 11,327
Hellow wakuu, natumaini mu wazima wa siha njema.
Wakuu kila siku asubuhi nielekeapo kwenye mihangaiko yangu ya kimaisha huwa napanda daladala. Kutoka ninapoishi mpaka ninaposhukia ni umbali wa vituo vinne tu. Kuna wizi wa kisaikolojia ambao makondakta huwa wananifanyia na huwa wanajua ni dhahiri kabisa kuwa siwezi kufanya chochote.
Iko hivi wakuu, kila siku nitokapo geto huwa natupia kipapaa (kiheshimiwa) mkononi na kibegi changu cha mpakato. Sasa nikitoa nauli mfano nikimpa kondakta shilingi mia tano ya noti au silver huwa wanajikausha na ni dhahiri kabisa wanajua kuwa siwezi kudai shilingi mia yangu. Wakati mwingine nikitoa shilingi elfu moja huwa wananirudishia mia tano. Maajabu ni kuwa watu wengine ambao hawajatupia haswaa wakitoa mia tano hurudishiwa chenchi (shilingi mia) kwa umbali ule ule na kituo kile kile ninachoshukia mimi.
Hii tabia imekuwa endelevu, na hapa mjini sio wakuja yaani kosa tu nikitupia lazima wanidhulumu shilingi mia yangu na wanajua siwezi kudai sababu watu watanishangaa na kunicheka.
NB: Sijisifii ila kiukweli huwaga sijisikii vizuri nikitoka bila kutupia kipapaa, na ninaamini wengi wetu tunakutana na hii kitu ila tunaumia kimoyomoyo kwa jinsi maisha yalivyo magumu na hizi mia mia zetu wanazotudhulumu.
Wakuu nilikuwa naomba mnipe trick ya kunasua huu wizi wa kisaikolojia