NADHIRI: Unapoiweka usisahau kuikamilisha na kuiondoa

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,666
729,801
Nadhiri ni ahadi na agano maalum Kati yako na Mungu kwa wale waaminio, japo kuna nadhiri za nguvu za giza.

Wengi wetu hukumbwa na Changamoto na mapito mengi ya kidunia na hufika mahali na kuweka nadhiri kuwa hili likipita salama nitafanya hili au lile ikiwa ni sehemu ya shukrani yangu kwa Mungu...

Nadhiri huwa kwenye mfumo wa sadaka zaka au matoleo yoyote yale kutotimiza nadhiri yako nikutotimiza ahadi uliyoahidi mwenyewe ni sawa na kutolipa deni... Hiki ni kitu kibaya.

Kwahiyo ni vema unapoweka nadhiri yako Kumbuka kuitimiza kishapo kuitoa au kuitengua
Kuna baadhi ya watu wanachanganya Kati ya kutoa na kuweka nadhiri... Kutoa ni siku ya kuitekeleza na kuweka ni siku ya kuahidi.

Kuwa makini nadhiri yako isije kuwa kiama kwako...

Jichunguze Kama huna nadhiri yoyote.
 
Je kama uliweka nadhiri angali u mtoto mdogo na leo hii huikumbuki vizuri kuna tatizo??
 
Nadhiri ni ahadi na agano maalum Kati yako na Mungu kwa wale waaminio, japo kuna nadhiri za nguvu za giza.

Wengi wetu hukumbwa na Changamoto na mapito mengi ya kidunia na hufika mahali na kuweka nadhiri kuwa hili likipita salama nitafanya hili au lile ikiwa ni sehemu ya shukrani yangu kwa Mungu...

Nadhiri huwa kwenye mfumo wa sadaka zaka au matoleo yoyote yale kutotimiza nadhiri yako nikutotimiza ahadi uliyoahidi mwenyewe ni sawa na kutolipa deni... Hiki ni kitu kibaya.

Kwahiyo ni vema unapoweka nadhiri yako Kumbuka kuitimiza kishapo kuitoa au kuitengua
Kuna baadhi ya watu wanachanganya Kati ya kutoa na kuweka nadhiri... Kutoa ni siku ya kuitekeleza na kuweka ni siku ya kuahidi.

Kuwa makini nadhiri yako isije kuwa kiama kwako...

Jichunguze Kama huna nadhiri yoyote.

Duh hii imenigusa sana....ngoja nijitahidi nitimize.
 
Kama uliweka nadhiri ambayo huna uwezo wa kuitoa unafanyeje mkuu
Mmh Hapana nadhiri si kitu cha lazima ni jambo la hiari sasa utawezaje kuahidi kitu usichokuwa na uwezo wa kukitimiza? Kuna mazingira ya ugonjwa na ulemavu mkubwa waweza kusababisha usitimize nadhiri yako... Kwa hali hii unaweza kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki wakakusaidia
 
mwaka huu MUNGU anisaidie nitimize nadhiri nilizoziweka kwenye mambo fulanii..nisije pata laana buree
 
Ahsante mshana jr kwa kutukumbusha

Ni afadhali usiiweke nadhiri, kuliko kuiweka alafu ukashindwa kuiondoa. Nadhiri isipoondolewa hubadilika na kuwa kifungo/laana

Siku hizi nikiona nimebanwaa ni bora niombe, nifunge au nitoe sadaka. Ukiweka nadhiri basi make sure unaiondoa/ kuitekeleza
Kinachoumiza ni kwamba eti siku hizi kuna waombaji mitume na manabii wanaotoa/kutengua nadhiri kwa malipo
 
Back
Top Bottom