Nadharia ya binadamu wa specie tofauti kuwahi kuishi duniani

hypothalamus

Member
Joined
Feb 19, 2018
Messages
94
Points
125

hypothalamus

Member
Joined Feb 19, 2018
94 125
Specie ni kundi la viumbe wenye uwezo wa kujamiiana na kupata kiumbe mwengine ambae ni fertlile(mwenye uwezo wa kuja kuzaa).

Viumbe kutoka specie tofauti huunda kundi moja linaloitwa Genus ambalo hubeba viumbe wanaofanana kwa asilimia zaidi ya 90,ni kusema kwamba binadamu wa genus moja hawawezi kujamiina kirahisi lakini wanafanana kila kitu.

Binadamu specie ya homo sapiens tumekuwa tukijifikiria kwamba sisi ndio binadamu pekee kuwahi kuishi duniani kwa kuwa kwa takribani miaka elfu 10 dunia imekuwa ikikaliwa na specie moja tu binadamu ya homosapiens,ukweli ni kwamba kuna specie nyengine za binadamu zilizowahi kuishi duniani kwa kipindi tofauti.

Kwa kipindi fulani ndani ya dunia ulaya na asia ya magharibi iliishi specie ya binadamu aina ya neanderthals ambao walikuwa na misuli zaidi ya wale wa specie ya sapiens na walikuwa adopted kuishi mazingira ya baridi.

Asia ya mashariki waliishi specie nyengine aina ya erectus ambao waliishi kwa miaka takribani milioni mbili.Specie hii ya binadamu inasemekana kuwa ndio walikuwa binadamu dhaifu zaidi kuwahi kutokea.Kuna mabaki mengine mengi ya specie zilizowahi kuishi lakini kumekuwa hakuna record za kutosha.

Leo hii kuna specie nyingi za ndege, samaki, paka, nyoka lakini kuna specie moja tu ya binadamu. Sababu za upekee huu zimekuwa moja ya swali gumu kwenye ulimwengu wa sayansi.

Kuna nadharia mbili zinazokinzana kwa nini sapiens ndio specie pekee iliyosalia duniani.

1.Nadharia ya muingiliano

Nadharia hii inasema sapiens baada ya kuevolve uwezo wa akili walisambaa duniani wakitokea Afrika mashariki na walipokuwa wakikutana na specie nyengine walijamiiana hivyo binadamu wa leo hii ni matokeo ya muingiliano huu.

Kama nadharia hii ni kweli binadamu wenye asili ya ulaya na asia ya magharibi na mashariki ya asia(wakorea na wachina)sio sapiens halisi.Binadamu wenye asili ya Afrika ndio sapiens asili. Nadharia hii inawapa nguvu wabaguzi wa rangi kwa kuwa kiasili binadamu wote si sawa.

2.Nadharia ya Replacment

Nadharia hii imejikita kwenye ukweli kwamba binadamu hawa wa specie tofauti walikuwa na muundo tofauti wa mwili(anatomy),pia hawakuwa na tabia zinazofanana za kujamiiana(mating behaviours) hivyo hawakuwa na matamanio ya kimwili kati yao hivyo kujamiiana haikuwa rahisi na pia ata kama ikitokea wakajamiiana wasingeweza kupata mtoto ambae ni fertile(anaeweza kuja kuzaliana).

Nadharia hii inasema kuna uwezekano zilikuwa zikitokea vita zilizo sababisha mauaji ya kimbari kwa binadamu specie tofauti na ya sapiens.

Kuanzia miaka ya 2010 wanabailojia wamegundua jambo moja la kushangaza.
Imeonekana genetics za mabaki ya nearthderthals kwa asilimia 1 mpaka 4 zinafanana na genetics za binadamu wa sasa wenye asili ya ulaya.
Research nyengine zinaonesha asilimia 6 ya genetics za binadamu wa sasa zinafanana na binadamu specie ya denisovans waliokuwa wakiishi Australia miaka elfu 30 iliyopita.
Matokeo haya yanaipa nguvu nadharia ya kwanza ya muingiliano hivyo kwa kiasi fulani unaweza sema binadamu hawafanani lakini kwa kiasi kikubwa wote tuna asili ya sapiens kutokea Afrika mashariki.

Nguvu kidogo inayopata nadharia ya pili ni ukweli kwamba binadamu aina ya sapiens wamekuwa na tabia ya kutokuwa wavumilivu wa kuishi na binadamu alie na tofauti na yeye(hii inaonekana hata leo hii ambapo tofauti ndogo tu ya kikabila imekuwa ikileta ugomvi)

Conclusion ambayo inaweza fikiwa mpaka sasa ni kwa kuwa wanyama kutoka specie tofauti hawawezi kuzaliana kirahisi kupata mtoto fertile,Sapiens na specie nyengine walijamiiana katika special occasions tu ambazo ndio zimepelekea utofauti huu mdogo wa asilimia za genetics.


Moja ya swali intresting kwenye ulimwengu wa sayansi ni ingekuwaje kama aina nyengine ya specie ndio ingebaki duniani tofauti na sapiens au kama mpaka leo kungekuwa na specie zote hizi nne tofauti.Je kungekuwa na utofauti gani wa kiutamaduni,kisiasa na mifumo ya kimaisha kuijumla? Je kitabu cha mwanzo kwenye biblia kingeandikwaje kuonesha utofauti huu?Je Quran bado ingeandika kwamba kuna makao maalumu kwa binadamu wa specie zote?Kwa miaka hii elfu 10 ambayo sapiens wamebaki peke yao imekuwa ni rahisi kujiona special na kuona wameumbwa.

Hata Charles Drawin aliposema binadamu ni kama wanyama wengine tu bado ilikuwa ngumu sapiens kuwaingia akilini.Je kama specie nyengine zingekuwepo bado tungeamini kwenye uumbwaji?

Swali jengine la kujiuliza kwa nini sapiens wameweza kuitawala dunia?
Wanasayansi wengi wa bailojia na wale wa mambo ya kale wanaamini kitu cha kipekee kilichowafikisha sapiens leo hapa ni uwezo wa juu wa akili(cognetive ability).

Uwezo huu mkubwa wa akili umewafanya sapiens miaka elfu 70 iliyopita kuendelea kwa haraka tofauti na specie nyengine ikichagizwa na utofauti wa uwezo wao wa lugha.

Lugha imeleta tofauti kubwa na kuwawezesha sapiens kuwasiliana kipekee kabisa.Hapa zimezaliwa nadharia mbili kuhusu sapiens walitumiaje lugha.

Nadharia ya kwanza inaamini uwezo wa sapiens kuhadithia tukio kwa urefu tofauti na specie nyengine umechangia mafanikio yake.Mfano nyani huwasiliana kwa sauti maalumu wanapoona mnyama hatari lakini sapiens wamekuwa na uwezo wa kuhadithiana tukio lile kwa sapiens wengine ambao hawakuwepo wakiongeza data nyengine kama ilikuwa eneo gani n.k uwezo ambao specie nyengine hawana.
Nadharia ya pili inazungumzia uwezo wa sapiens kusengenya(gossip) tofauti na specie nyengine hii imekuwa tabia kuu ya sapiens.

Ni rahisi kwenye chakula cha mchana kumkuta profesa wa physics amekaa na profesa mwengine wakigossip kuliko wakizungumzia physics.

Nadharia zote hizi mbili zinaonekana kuwa na ukweli fulani.

Sifa nyengine aliyonayo sapien ni uwezo wa kuvuta picha ya vitu hata ambavyo havioni au hajawahi kuviona.Mfano ni ngumu kumwambia nyani akupe ndizi kwa kuwa kufanya hivyo kutamfanya aende peponi hana uwezo huo wa kuvuta picha.
 

Anikajema

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Messages
364
Points
250

Anikajema

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2014
364 250
Ukweli nikwamba waafrica tunapenda. Kukumbatia story za kijinga kama hizi ambazo hazsaidii chochote katka Elimu,taifa, na familia zetu kwa ujumla ndio maana tunaendelea kuwa wa mwisho katka maendeleo ya science, nk: tukiamka katka usingzi huu tutakuwa wajanja sana ase! MF: nirahis sana kumuaminishi muafrica kuwa chini ya ardhi kuna nyoka Mkubwa ambaye anakaa kwenye bahar ilyopo chini ila ukimwambia uchawi hakuna Ni story tu za kutsha hapo mtagombana sana tu....
 

hypothalamus

Member
Joined
Feb 19, 2018
Messages
94
Points
125

hypothalamus

Member
Joined Feb 19, 2018
94 125
Ukweli nikwamba waafrica tunapenda. Kukumbatia story za kijinga kama hizi ambazo hazsaidii chochote katka Elimu,taifa, na familia zetu kwa ujumla ndio maana tunaendelea kuwa wa mwisho katka maendeleo ya science, nk: tukiamka katka usingzi huu tutakuwa wajanja sana ase! MF: nirahis sana kumuaminishi muafrica kuwa chini ya ardhi kuna nyoka Mkubwa ambaye anakaa kwenye bahar ilyopo chini ila ukimwambia uchawi hakuna Ni story tu za kutsha hapo mtagombana sana tu....
No research no right to speak
 

Forum statistics

Threads 1,343,293
Members 515,003
Posts 32,779,359
Top