Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

Discussion in 'Great Thinkers' started by Mchambuzi, Feb 15, 2012.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Napendekeza nadharia tete (Hypotheses) zifuatazo, lengo kuu ikiwa ni kutupa sote nafasi ya kuzipima nadharia hizi tete, kwa kutumia uzoefu wetu na uelewa wetu juu ya utamaduni wa CCM, hasa kwa kuzingatia matukio na mazingira ya nyakati hizi. Matokeo ya zoezi hili la kupima nadharia tete hizi yatatoa majibu ya aina mbili: Aidha majibu - KWELI, hivyo kufanya nadharia hizi tete kusimama, au majibu - SIO KWELI, hivyo kuziangusha hizi nadharia tete. Nadharia tete zipo nne kama ifuatavyo:

  I. Ingawa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM halazimiki atoke miongoni mwa wajumbe wa NEC na pia suala hili halipo kikatiba, Chama Cha Mapinduzi hakina utamaduni wa kuteua wagombea wake wa Urais ambao sio miongoni mwa wajumbe wa NEC.

  II. Ili mwana CCM awe na nafasi nzuri ya kuteuliwa kubeba bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, inamlazimu mwanachama huyu, agombee na ashinde uchaguzi wa wajumbe wa NEC kwenye uchaguzi wa ndani wa CCM mwaka huu wa 2012. Kwa kufanya hivyo, mwana CCM huyo atakuwa ni mjumbe wa NEC-CCM ifikapo mwaka wa uchaguzi mkuu, 2015, hivyo kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuteuliwa kubeba bendera ya CCM mwaka 2015.

  III. Wanachama wa CCM wenye malengo ya kugombea Urais kupitia CCM mwaka 2015, ambao kwa sasa wanashikilia nafasi mbili kwa pamoja – yani ubunge na ujumbe wa NEC, chini ya mabadiliko ya katiba ya CCM ya hivi karibuni, itawalazimu aidha waachie nafasi zao za ubunge na kubakia wajumbe wa NEC, au waendelee na Ubunge na waachane na ujumbe wa NEC, huku wakisubiri Baraka za Mwenyekiti wa CCM Taifa za kuwateua kuwa wajumbe wa NEC, kupitia zile nafasi kumi, miezi michache kabla ya mchakato wa kutafuta mgombea Urais kupitia CCM, ili mwanachama huyo awe katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda katika kinyang’anyiro hicho May, 2015.

  IV. Kwa maana hii, Mchezo wote wa kinyang’anyiro cha Urais kupitia CCM mwaka 2015, umebadilika kutokana na mabadiliko ya katiba ya CCM, hivyo tutarajie majina mapya kutawala mbio hizi baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa CCM Novemba mwaka huu wa 2012, majina ambayo wengi hatukuyatarajia.
   
 2. Eric Cartman

  Eric Cartman JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,816
  Likes Received: 1,352
  Trophy Points: 280
  Nadhani jamii ya wana CCM (na watanzania kama CCM ikiendelea na nadharia yake ya kushinda kwa namna yeyote)
  itakuwa ni ku-gamble na kiongozi wa kitaifa especially point 'III and IV' kama zitapewa vipaumbele. Ni muhimu sana kujua political superstars wetu wanaongea na ukiangalia siasa za taifa na media reporting style jamaa ambae hana platform NEC in most cases hana publicity na msimamo wake auweleweki, in other terms huko ndio kuuziwa mbuzi ndani ya gunia.

  Cha muhimu watu wenye nia ya kutaka kugombea uongozi wajuu Tanzania waanze kuongea sera kwa kuangalia bajeti na jinsi watakavyotusogeza nayo and offcourse the mention of katiba yenye accountablity ndio hiwe kigezo chao. Vinginevyo hawa jamaa hawata eleweki just as the slogan 'maisha bora kwa kila mtanzania' bila ya explained approach to do so (including checks of accountability). Maana baadae itakuwa lawama tu hoo sio mimi bali watekelezaji.
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,814
  Trophy Points: 280
  Nadhalia tete zote tano kwangu mimi zinasimama. Kuna kitu kikubwa kipo nyuma ya mabadiliko yaliyofanyika. Sijui mapendekezo ya Kamati ya Mwinyi yalikuwa na nini ndani yake. Lakini pia ikumbukwe ya kwamba JK amekulia ndani ya chama hivyo anakijua vyema na anazijua vyema FITINA za NEC ya CCM kwa hiyo kwa kuasisi na kusomamia mabadiliko haya ya Katiba sina shaka ana siri nzito moyoni. Katika siri hiyo ndipo naona nadharia tete namba IV inasimama na kupata mashiko. Time will tell.
   
 4. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Nadhani kamati ya mwinyi, kinana na Msekwa nia yake ilikuwa ni kuvunja makundi yaliyotokana na vurugu za Richmond, kazi ambayo hawakufanikiwa kuimaliza. Pengine kazi hiyo ikahamishia nguvu zake kwenye mabadiliko ya katiba ambayo ndiyo tumeyasikia majuzi. Lakini kuna kitu kimoja ambacho nashindwa kuelewa. katika katiba ya CCM ibara ya 106 sehemu ya 4, inaelezea kazi za mkutano mkuu wa CCM taifa kuwa ni pamoja na:

  "Kubadili sehemu yoyote ya katiba ya CCM kwa uamuzi wa theluthi mbili za wajumbe walio na haki ya kupiga kura kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar".

  Kwa maana hii, Je, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wameporwa kazi hii? Au yaliyopitishwa majuzi ni mapendekezo ambayo yatapelekwa mbele ya mkutano mkuu wa taifa? Na lini mkutano huu utakaa? Kwani sidhani kama kutakuwa na mkutano mkuu wa taifa kabla ya Mwezi November 2012 wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa NEC CCM, Dodoma. Na iwapo mapendekezo haya ya mabadiliko yatahitaji baraka za mkutano mkuu wa taifa, ina maana kwamba sheria hizi mpya zitaanza kutumika baada ya uchaguzi mkuu wa chama November mwaka huu au kabla? Kama ni kabla, basi ina maana kwamba itabidi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa waanze na shughuli hii kwanza ya kubariki mabadiliko haya kabla ya kuanza mchakato wa uchaguzi wa NEC. Kwa kweli inachanganya kidogo kuhusu nini kinaendelea sasahivi ndani ya CCM, hasa pale taarifa zinapomnukuu Nape akisema kwamba haya kwa sasa ni mapendekezo tu, na yatapelekwa NEC.

  Katiba ya CCM ibara ya 108 sehemu ya 10 inasema hivi kuhusu kazi za halmashauri kuu ya taifa:

  "Kuandaa katiba, kanuni, na kuweka taratibu za kuongoza shughuli mbalimbali za CCM".

  Je katika suala hili la mabadiliko ya katiba, nani ni kuku na nani ni Yai kati ya NEC na Mkutano Mkuu wa Taifa? Wenye uzoefu na CCM tusaidieni katika hili, sisi huku 'site' mambo mengine kuhusu CCM yanatupita kushoto kidogo.
   
 5. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Watafanikiwa kweli kwa njia hii badala ya kuendeleza utamaduni ule ule wa kujaribu wakubalike ndani ya chama kwanza? Maana ni jadi kwa viongozi wa CCM wenye ubunifu na wachapa kazi kuonekana hawafai; ni kawaida kupigwa majungu na kumalizwa kisiasa, hata kama wanachofanya kina maslahi kwa taifa.
   
 6. Eric Cartman

  Eric Cartman JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,816
  Likes Received: 1,352
  Trophy Points: 280
  Kwa maana hiyo WaTz ambao ni wana CCM ndio mnaowekwa njia panda. Iwapo mchakato wa kuwafikisha viongozi wenu bora umejaa majungu kwa maana hiyo viongozi wengi wanaofikia ngazi za juu hawaitaji umuhimu wa kujua kuchanganua sera kama wewe za kutupeleka mbele ki maendeleo (be it your philosophy). Particularly hiwapo wana wania nafasi za kiserikali na taifa au hata uongozi wa kichama. Ina maana hawana ulazima wa kujielezea ki-sera jinsi ya kukipeleka chama mbele wala kuki imarisha chama mbele ya wanachama (somen tell me wanachama wengi si waelevu wa siasa).

  Si ajabu wewe ukaishia JF na Tambwe Hizza (or somen) akawa kiongozi wa kichama au hata ya huyo raisi aliyotokea kwenu kushindwa kuelezea sababu za umaskini wa taifa analoliongoza kwa sababu za kutatua matatizo hayo hayo ya umaskini yaliyomfanya agombanie urais in the first place..

  If it was me and those were the facts ndani ya CCM, nadhani ungekuwa muda wa kuamisha majeshi if politics was my ambition.
   
 7. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Kama hata Nyerere alitamka kwamba CCM sio Mama Yake Kwani anaweza kuachana nayo, mimi ntakuwa mtu wa namna gani kuona CCM ni kama mama yangu? Wengi tunavuta subira kuona kama mabadiliko ya kweli yatakuja, hasa ukizingatia kwamba katika organization yoyote, "the only thing that is constant is change". Vinginevyo mimi bado ni mwanachama hai wa CCM, niliyelipia kadi yangu hadi mwaka huu wa 2012. Mwaka huu ni muhimu sana kwangu kuhusu maamuzi magumu.
   
 8. K

  Keil JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Pendekezo la Mabadiliko ya Katiba lilitoka kwenye Kamati ya Mukama ambayo ilichunguza kiini cha CCM kufanya vibaya sana kwenye uchaguzi uliopita.

  Utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati ya Mukama ndio ulianza na ile kauli ya JK ya kujivua gamba 5/2/2011. Lengo haswa la kujivua gamba ilikuwa ni kuwatosa wale wote ambao walionekana mbele ya jamii kwamba ni mafisadi.

  Ili kufikia malengo hayo, ndipo mwezi April mwaka jana CC ilipovunjwa, lengo ikiwa ni kumsaidia Mwenyekiti aweze kumuondoa RA na Chenge kwenye CC. Baada ya hapo pia walitakiwa kuondolewa kwenye NEC, lakini bahati mbaya imeshindikana kwa kuwa wote ni magamba, yaani watosaji na watoswaji.

  Pia Kamati ya Mukama ilipendekeza mfumo mpya wa uchaguzi wa ndani wa CCM na hasa kwa wajumbe wa NEC kwa kuwa kuna baadhi ya wana CCM wanatumia ukwasi wao kupata support kubwa kwenye vikao vya maamuzi [CC na NEC] na hivyo wanaweza kutumia vibaya influence yao ili kukiyumbisha chama.

  Swala jingine ambalo lilipendekezwa ilikuwa ni pamoja na kuwa makini na matokeo ya kura za maoni, kwamba inabidi kuheshimu matokeo ya kura za maoni ili kuepusha majeraha ya kura za chuki. Kama kuna mtu atafyekwa jina basi kuwe na concrete evidence.

  Pamoja na mapendekezo yote hayo, bado hawajaweza kuja na muarobaini ambao unaweza kuzuwia watu kutumia ukwasi wao ili kupata uongozi. Ninausubiri kwa hamu huo muarobaini maana once ukianza kutumika unaweza kuwagusa wengi walioshikilia utamu kwenye chama twawala.

  Kwangu mimi haya mabadiliko ya Katiba sioni kama yanawasaidia CCM, sana sana yanazidi kuongeza uhasama tu na kuwafanya wenye ukwasi mwingi wa kumwaga kwenye wilaya 120 au zaidi, waweze kupata wajumbe wanao wataka. Wale wenzangu akina kakamiye ambao wanategemea sera zao na politiki za maneno matupu, wataambulia pakavu maana ndani ya CCM mkono mtupu haulambwi! Kuna mtu amesema mfumo huu umeongeza KIOSK cha wapiga kura kujipatia vijisenti mwaka huu, maana lazima watakula sana.
   
 9. Eric Cartman

  Eric Cartman JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,816
  Likes Received: 1,352
  Trophy Points: 280
  Blaza,

  ur more of a weapon inside the political life than as an observer, at times you got to weigh your chances and do the right thing, deep down you care for Tanzanians problems than party affiliation.

  It's ya call based on ur understanding of our political life umeshachambua vya kutosha now you need the platform to influence. Huwezi jua labda unaweza kuwa kivutio cha wengine kuamia elsewhere as CCM is proving to be a dead ear. All the best on ya choices, either way your political stance is almost clear to everyone and appreicated (in my part).
   
 10. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Diagnosis yako nzuri sana, hasa kuhusu mapungufu ambayo bado yapo bayana. Kwa mtazamo wako, ni mambo yepi makuu matatu, kwa mfano, unaona kwamba yakifanyika, CCM itarudi katika mstari? Iwapo katika orodha yako, utataja suala la kuwafukuza wale wote wanao tuhumiwa kwa mafisadi, naomba pia utoe mwongozo juu ya nini CCM ifanye ili kuzuia chama kisiyumbe baada ya kuchukua maamuzi hayo magumu.
   
 11. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Asante Eric,
  Daima nitakumbuka maneno yako mazito na ya kutia moyo, na muda wa maamuzi magumu ukiwadia, you will be among the first to know. Otherwise the sun is setting.
   
 12. Eric Cartman

  Eric Cartman JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,816
  Likes Received: 1,352
  Trophy Points: 280
  Nothing to add but wishing ya all the best.

  CIAO.
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Feb 15, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Tatizo kubwa ni kwamba CCM imetaka kufanyia mabadiliko Katiba yake lakini imeamua kufanya mabadiliko nusunusu. Ni mabadiliko ya kusaidia siasa za ndani zaidi kuliko ya kutaka kupata mgombea bora zaidi. Mabadiliko ya kweli ambayo yangerudisha nguvu kwa wanachama moja kwa moja na kufungua wigo wa demokrasia hayawezekani kwa sababu yatawezesha kweli mgombea bora kuibuka! Kwa mfano:


  a. Mabadiliko haya yanashikilia bado uamuzi wa mwisho wa mteuliwa yeyote kwenye Kamati Kuu na siyo wanachama! Wamebadilisha chini bila kubadilisha juu.

  b. Mabadiliko haya hayaweki ulazima wala utaratibu wa wagombea wa Urais kushindanishwa kwa hoja. Kwa mfano, kuweka midahalo ya ndani na ya wazi ya wagombea wa Urais - kama tunavyoona wanavyofanya Marekani kwa mfano. Hili lingefanyika 2005 kuna watu wasingeingia Ikulu kwa kweli.

  c. Mabadiliko haya hayaweki uhuru wa wagombea kuwa na ilani zao ambazo zitashindanishwa mbele ya wanachama ili aliye na ilani bora na anayekubalika ndiye anaweza kushinda. Na badala yake bado Ilani ya chama itachorwa kwa ujumla wake na wagombea watatakiwa kuitekeleza.


  Kwa hiyo, binafsi naamini ni mabadiliko ya kutuliza siasa za ndani za CCM na ni jaribio la kuwahi kile ambacho wanakihofia - mgongano mkubwa wa wagombea. Hata hivyo, utakapokuja wakati wa utekelezaji nina uhakika kutakuwa na mgongano mkubwa wa ndani kwa sababu ya kile ambacho umekidokeza yaani kuibuka majina mapya ambayo hata sasa hayajaanza kufanya kampeni. Wale ambao wanatajwa sasa wanaweza kujiona kuwa wananyang'anywa kile ambacho ni haki yao.
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  Feb 15, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,545
  Likes Received: 18,194
  Trophy Points: 280
  Nadhani ujumbe wa nec utakuwa sio dili tena!. Na kwenye katiba mpya tutapendekeza mawaziri wasiwe wabunge ili tuweke professionals na wabunge wabaki ni watumishi wa watu only!. Rushwa ya uongozi itapungua"
   
 15. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Well Said. Kwa maelezo haya, kama CCM ina nia ya dhati ya kubadilika kama inavyohubiri chini ya falsafa yake ya kujivua gamba, kwa mapungufu uliyoainisha, CCM haina jinsi bali kurudi tena kwenye 'drawing table'. Vinginevyo haya mabadiliko hayataleta mabadiliko. Sana sana yatafungua mlango mpya wa makundi, migonano, kama ulivyoelezea, na pengine kupelekea kwa CCM kugawanyika katika vyama viwili vikubwa, na kwa bahati mbaya, tofauti ya vyama hivi haitakuwa itikadi bali personalities and politics za wale ni wasafi, hawa ni wachafu.
   
 16. mchongameno

  mchongameno Member

  #16
  Feb 15, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana nawe Mwanakijiji kwa 100% kwa sababu mimi naamini mabadiliko yamelenga si tu kwa kuleta tija ndani ya Chama yaani si ya mfumo wa kuendesha Chama bali ni kuwabana watu fulani wasiwe na nafasi ya uongozi. Kwa sababu kama ni suala la utekelezaji suala la kujivua Gamba, kwa nini kusifanyike maamuzi ya kuwachukulia hatua wahusika kabla ya Mabadiliko haya ya Katiba ya CCM? Nini kimekuwa kikwazo? Na kama kuna kikwazo basi inaonyesha hakuna aliye safi. Wote ni Magamba.
   
 17. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #17
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Kwa mtazamo wako, wanaposema kwamba moja ya sifa za mtu kuteuliwa kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM ni uzoefu ndani ya chama, uzoefu huo utatokana na nafasi zipi miongoni mwa wagombea? Kuhusu suala la uwaziri kutenganishwa na ubunge upo sahihi. Lakini ni muhimu sana pia tukaamua tunataka kufanikisha nini chini ya mfumo huo: Je, tunalenga more accountability ya serikali au tunalenga stability ya serikali? Na je, bunge lipewe mamlaka ya kubariki teuzi za rais kwa nafasi kama za mawaziri? Kuhusu rushwa kupungua iwapo uwaziri na ubunge vitatenganishwa, sina uhakika sana juu ya hilo, vinginevyo ufafanue zaidi una maana gani.

  Ila all in all, iwapo tutakuwa na mawaziri wasiotokana na wabunge, na pia wabunge wapewe mamlaka ya kubariki au kukataa teuzi za Rais, mawaziri watajituma zaidi kwani tofauti na sasa ambapo wabunge na mawaziri lao ni moja kwa maana kwamba they sympathize each other kutokana na commonality yao, mawaziri wasiotokana na wabunge hawatakuwa na mahusiano haya na wabunge, hivyo kuongeza uwajibikaji miongoni mwa mawaziri.
   
 18. T

  Topical JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Yanapatikana wapi in full hayo mabadiliko??
   
 19. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #19
  Feb 15, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Wakuu mpaka sasa kuna vigezo vya kimaandishi vya nani anayetakiwa kuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali za Chama na kuwa kiongozi wa ngazi mbalimbali za seriklai kwa tiketi ya chama. Na kuna vision na manifesto ya chama ambayo wanaogombea nafasi yoyote ile wanatakiwa kuwa na jukumu la kuitekeleza. Lakini kuna vigezo vingine ambavyo havipo kiimaandishi ndio vinaangaliwa na kuzingatiwa kabla ya kuruhusu mtu kupewa nafasi ya kuwa mgombea wa nafasi uongozi, inawezekana hivyo ndio vina nguvu zaidi kuliko vile vilivyoandikwa. It is a matter of having those unwritten qualities and mimick the written ones. So we have official criteria and real criteria, the official one ni ya kuwadanganya watu, na real one is the one which actually work .

  Inasikitisha sana kuona kuwa kiongozi anasema wazi kuwa ana msimamo huu kuhusu jambo hili na ana mtazamo ule kuhusu jambo lile, lakini ukiangalia utendaji wake na vitendo vyake huwezi kuamini kinachofanyika. So the idea that we should judge them on their statements and views on policies, budget and how they will work around them is questionable. There is plenty of evidence that what they say and what they actually do, are two different things. Umetoa mfano mzuri sana wa "maisha bora kwa kila mtanzania", angalia nani alileta maisha bora kwa mtanzania, at least aliyejaribu. JK au BM?

  Ni vizuri ku-strengthen institutions na kuwapima watu kwa walichofanya kutekeleza kile kilichoandikwa kwenye katiba ya chama, manifesto ya chama na katiba ya serikali na malengo ya kuiboresha Tanzania. Nadhani kuna haja ya kuwa na uniformity kwenye katioba za vyama vyote inapokuja kwenye mambo ya kugombea nafasi za urais. Sasa hivi techinically kuna uwezekano wa any party to win presidency, kwa hiyo ni vizuri kuwe na utaratibu wa kitaifa wa kuscreen wanaotaka kwenda kugombea urais.

  NEC yenyewe (hata ya Chadema na vyama vingine) ukiangaza ndani yake unaweza kuona ni chombo chenye jina kubwa lakini kuna members ndani yake ambao are worse than you and me who are not in there. Pamoja na kuwa kweli katiba haisemi mgombea Urais awe mjumbe wa NEC, lakini huo ndio ukweli. Na kama ukiweza kurally support ndani ya NEC kwanza (kwa ulaghai au ukweli) unakuwa na nafasi nzuri kuteuliwa kuwa mgombea urais. Hiyo ni weakness kubwa sana ya real unwritten Constitution of CCM.

  Naona kizuri ni kuimarisha miondo na taasisi iliziwe na nguvu zaidi ya kuwabana wanaogombea nafasi waweze kudeliver baada ya kuchaguliwa. sasa hakuna.
   
 20. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #20
  Feb 15, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  a. ukiangalia mfumo wetu wa vyama vya siasa, si rahisi kwa wanachama kumchagua mgombea urais directly. Kwa mfano, ni rahisi mno kwa mwanachama wa CCM mkoa wa Dar es salaam, kwenda kupiga kura morogoro au Pwani. Hata kama watapiga kura siku moja, itakuwa vigumu sana kuitambua "franchise" ya CCM na kuicontrol (ni rahisi kuhujumu). Pia, pamoja na gharama kuwa kubwa, visiwani hawatawakilishwa proportionally.... au mikoa migine ambayo haina wanachama wengi wa CCM. Kwa hiyo NEC itafaa kwa sababu itakuwa inawakilisha chama proportionally based on the citizenry and not party affilliation.

  b.Kwa Tanzania, chama cha siasa kinasimamia hoja. Unlike US, wagombea wa republicans wanaweza kuwa na hoja inayokinzana na chama chao na bado wakashinda uchaguzi. Kwa Tanzania hiyo haiwezekani. Kama unataka serikali tatu..... unaenda CDM etc.. Kama kuna chama kinataka kufanya huu mtindo kifanye,ila nadhani kutakuwa na ngonjera nyingi tu, na wagombea wataonekana kuwa tofauti na imani za vyama vyao.

  c. a na b nadhani zinaelezea c kwa sababu vyama ndio vinavyoongoza nchi ndiyo maana hakuna mgombea binafsi.

  Kuchagua wajumbe wa NEC kutoka wilayani ni jambo la busara, kwa sababu matawi na kata ndiyo zitakazoshindanisha ujumbe wa NEC... if you can penetrate that deep, then you definately deserve to be a presidential candidate. Mabo ya kuhonga wajumbe wa mkutano mkuu yatakuwa yamekatiliwa mbali. This is the best way kama CCM inataka kuwashirikisha wanachama wake kwenye maamuzi.
   
Loading...