Nadharia tata ya matukio ya mauaji na utekwaji (Mawazo, Ben, Azory, Lissu, Kanguye na Mo)

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Leo nataka nikufundishe dhana moja ngumu kidogo hasa kama ni mgeni katika ulimwengu wa kijasusi, Nilipoanza chuo katika masomo ya Forensic Psychology niliona ni masomo mepesi nikahisi huenda nimechagua mchepuo wakitoto, lakini kadili ninavyopanda na kuingia katika uwanda uliopevuka, najifunza kitu kikubwa ambacho huenda sisi huku Afrika tunajipunja kwakuwa hatuyatafuti maarifa haya na kufunza vizazi chetu.

Kwa hakika hili ni pigo kwetu, Naaam, ukisoma kitabu cha Ujasusi wa kidola na Kiuchumi Sura ya 2, Ukurasa wa 306 nimeeleza juu ya Kinga za Kijasusi, nimeeleza kuwa, Kwenye nchi yoyote ile duniani katika mambo ya utawala na uongozi, kuna kitu kinaitwa National Intelligence na kingine kinaitwa State Intelligence.

National Intelligence huwa ipo kisheria (Legal), na State Intelligence huwa haipo kisheria (illegal au unauthorised). Wanaweza kufanya kazi moja, mahali pamoja, nk. Tofauti yao nikuwa kimoja Natinal Intelligence kinafanya kazi chini ya miiko na taratibu za kisheria kwa nchi husika, na State Intelligence hakitambuliwi na sheria yoyote zaidi ya (decree) na mara nyingi huwa hakifahamiki na wengi katika serikali, huenda katika nchi kikafahamika na watu watano au sita tu. Baadhi ya nchi, kila rais au Waziri Mkuu wa nchi huiingia madarakani na watu wake wa State Intel, Katika nchi za kiafrika si lazima wote wawe wamepata mafunzo ya kijasusi, wanaweza kuwa ndugu zaidi, wafanyabiashara, marafiki zaidi nk, ilimradi wanakuwa wapambe wa kiongozi husika. Kazi za kikosi hiki huwa ni hujuma kwamaana ya kuua, kuteka, kuiba katika mabenki ya ndani au ya nje, kupindua serikali yoyote au kumweka madarakani rais/waziri mkuu yoyote katika nchi yoyote, inategemeana na matakwa ya mmiliki wa kikosi husika.

Nchini Marekani ndani ya shirika la ujasusi la CIA, kuna kikosi kinaitwa Special Activites Division (SAD), Hiki huendesha shughuli zenye maslahi ya rais, chafu, mbaya na pia dhalili zenye maslahi kwa nchi na muda mwingine kwa maslahi ya wakuu katika nchi au katika vikosi husika. Uwepo wacho hautambuliwi na katiba wala sheria yoyote.

Nchini Israel, serikali ya Tel Aviv chini ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu ina kikosi cha siri kiitwacho Kidon, au kwa lugha ya kiswahili kinaitwa ncha ya mkuki, hiki ni kikosi kisichotambuliwa na sheria yoyote ndani ya Israel, na hata utambulisho wa maafisa wake hakuna aujuae. Sehemu kubwa ya shughuli zake ni mauaji na hujuma kwa yeyote anayepinga au kuukosoa utawala wa Tel Aviv, awe wa ndani au wa nje ya Israel. Kikosi hiki kimefanikiwa kuzima harakati zote za kiarabu na makundi yote ya kiislamu yenye msimamo mkali kwakuua mmoja baada ya mwingine.

Nchini Urusi nako ikulu ya Kremlin chini ya Vladimir Vladimirovich Putin ina kikosi ndani ya jeshi kitwacho Spetsnaz ambacho ni cha makomandoo walioiva zaidi kabisa katika ardhi ya Urusi, na kazi yake kubwa ni hujuma za kinchi, oparesheni maalumu za kinchi na kudhibiti wapinzani wa kisiasa na wanaharakati nchini Urusi, kikosi hiki kipo ndani ya jeshi la Urusi lifahamikalo kama Red Army japo kinaundwa zaidi na maafisa wengi kutoka shirika la Ujasusi la nchi hiyo la FSB, sehemu ya shughuli zake (activities) hazitambuliwi kwa sheria yoyote ndani na nje ya Urusi. Alipoingia madarakani Putin alikitumia kikamilifu kikosi hiki kuwadhibiti kwakuwapoteza wapinzania wake nchini pia alifuta matajiri wote aliowakuta na kisha kutengeneza matajiri wengine wanaokuwa royal kwake. Kuwafungulia kesi na kuwaua kwa sumu ni moja ya mbinu inayoaminiwa kwa kiwango kikubwa na mamlaka za Kremlin. Rejea mauaji ya 23 Novemba 2006 ya Alexander Valterovich Litvinenko, na jaribio la mauaji ya 04 Machi 2018 ya jasusi kicheche (double agent) wa Urusi na Uingereza bwana Sergei Viktorovich Skripal na bintie Yuri.

Nchini Zanzibar kuanzia baada ya mapinduzi mpaka miaka ya 1980+, kulikuwa na kikosi kilichoitwa "viwavi jeshi" hiki kilikuwa ndani ya Idara ya Usalama Zanzibar (ZIS) kilichokuwa chini ya Kanali Seif Bakar, kazi kubwa ya kikosi hiki ilikuwa ni kuwashughulikia wale wote waliopinga ama kukosoa utawala wa Mzee Karume, kikosi hiki kilikuwa kimepata mafunzo ya hali ya juu toka Ujerumani Magharibi.

Kwa namna yoyote, hujuma, uhalifu dhidi ya ubinadamu na ama mauaji ya wanaharakati au wanasiasa ndani ya taifa lolote hayafanywi na mashirika au idara kama taasisi zilizopo kisheria, bali hufanywa na vikosi vya namna hiyo vinavyofanya kazi chini ya amri za kirais (presidential decrees). Nchi zinapofilisika katika hazina yake, vikosi kama hivi hugeuzwa kuwa makundi ya ujambazi na kuvamia mabenki ya nje au ya ndani, kuwatapeli matajiri, kuwaibia matajiri, kuwateka nakupora (uharamia), kuvamia hasa migodi na viwanda vya vito vya thamani, na uchafu mwingine mwingi ambao kimsingi unatafsiriwa na umma kwamba hutendwa na makundi tu ya ujambazi na sio serikali.

Wakati huo katika nchi za Magharibi kama Nchini Marekani, Rais amepewa kinga yakutoshitakiwa kufuatia shughuli za oparesheni za kijasusi zinazofanywa na CIA kwa manufaa ya taifa la Marekani na hata zisizo na manufaa kwa taifa. Kinga hiyo huitwa, AMRI No 12333 (Executive Order No 12333) ya mwaka 1947 ambapo mwaka 2008, ilifanyiwa marekebisho.

Mwaka 1974 hadi 1976, kwenye mapendekezo ya taarifu huru ya tume ya Agranat , ambapo aliyekuwa Waziri Mkuu Israel Bwana Yitzhak Rabin alimteua Jenerali Rehavam Zeevi kuwa mshauri wake, katika mambo ya usalama na ujasusi. Vile vile, Zeevi akawa mshauri wa Waziri Mkuu katika masuala ya vita dhidi ya ugaidi ndani na nje ya Israeli, na akawa pia mwambata wa Mkurugenzi wa Usalama Jeshini, na vile vile, akawa afisa maalumu wa kumtaarifu Waziri Mkuu, juu ya tofauti za kimawazo, zilizokuwa zikijitokeza katika idara na vitengo vya usalama na ujasusi.

Katika maoni yake ya jumla, Jenerali Rehavam alisema, ni udhihirisho uliowazi kuwa uamuzi na matakwa ya vitengo vya siri vya ofisi ya Waziri Mkuu visivyotambuliwa na katiba wala sheria, vina nguvu kuliko mamlaka zilizopo kisheria (akimaanisha mkurugenzi wa Kidon ananguvu kuliko wa Mossad). Hii ilikuwa ni katika kuonya utendaji kazi wa chombo hicho ambapo wakurugenzi wote huripoti kwa bosi mmoja ambaye ni Waziri Mkuu.

Sikufundishi kuelewa, nakufundisha kufikiri maili milioni...

Unataka kujua undani wa kisa hiki cha kijasusi?
Soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.

OFA YA NYERERE DAY inaendelea..... Ni 56,000/= tu.. Kitabu cha Taifa na Afrika cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi kinauzwa kwa ofa ya punguzo la 30% sawa na 56,000/=

Ofa inaisha Jumatatu 22/10/2018.....

Piga simu na lipia 56,000/= tu, M Pesa na Tigo Pesa.

0755865544
0715865544

IMG_20181019_013125_805.jpg
 
View attachment 903850
Vipi kamati kuu chadema imesemaje kuhusu komu na kuvenea?
 
Law is mind without a reason, time always speak the truth. (Nchi za Africa tupo nyuma sana kwenye maswala hayo, tuangalie kwa watendaji hasa wa kazi hizo, kuanzia uaminifu, mafunzo, na utendaji ni dhaifu. Na ndio maana viongozi wengi wetu hufeli kutokana na maamuzi yao na strategic tacles wanazo zichukua :- Kifupi Plan na Excecution hua haziendani. Kwa mfano mzuri Mheshimiwa Jacob Zuma, stratetgy zake ndio zilimuangusha urais hapo South Africa)

Halafu turudi kuangalia mfano wa Jasusi alieiamua vita ya pili ya dunia (Second World War). Mr Juan Pujol Garcia, aliejulikana kwa jina almaaruf Agent Garbo. Na mwingine jasusi wa kiongozi Joseph Stallin kipindi hicho akitawala Soviet, wakati Hitler (German) na Hirohito (Japan) wakijiandaa kuipiga Soviet Union. Mr. Richard Sorge. *Hivi vilikua ni vimelea hatari sana ambavyo sasa nchi nyingi zinajaribu kuzalisha majasusi kama hawa ila wanafeli*

Ni kitabu kizuri sana, na umeandika jambo geni katika akili za watu wengi.

Hongera sana mkuu, Salut
 
Rejea mauaji ya 23 Novemba 2006 ya Alexander Valterovich Litvinenko, na jaribio la mauaji ya 04 Machi 2018 ya jasusi kicheche (double agent) wa Urusi na Uingereza bwana Sergei Viktorovich Skripal na bintie Yuri.
Mkuu Yericko Jina ni Yulia siyo Yuri.
Nchini Zanzibar kuanzia baada ya mapinduzi mpaka miaka ya 1980+, kulikuwa na kikosi kilichoitwa "viwavi jeshi" hiki kilikuwa ndani ya Idara ya Usalama Zanzibar (ZIS) kilichokuwa chini ya Kanali Seif Bakar, kazi kubwa ya kikosi hiki ilikuwa ni kuwashughulikia wale wote waliopinga ama kukosoa utawala wa Mzee Karume, kikosi hiki kilikuwa kimepata mafunzo ya hali ya juu toka Ujerumani Magharibi.
Viwavi Jeshi walifundishwa Ujerumani Mashariki ile ya Kikomunisti au Ujerumani Magharibi ?
 
Back
Top Bottom