Nadhani wanawake wengi wangependa kuolewa na mwanaume wa hivi

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,571
35,472
KE: Baby nitachelewa kurudi,kuna rafiki yangu mmoja kaja leo toka UK tulisoma nae sekondari,tuko hapa wambea bar tunapiga stori za zamani.(hiyo ni saa tano usiku)
ME: Aaah na wewe nae hadi saa hizi,basi usichelewe kurudi,nafunga mlango lakini,ukifika gonga.
wegine
KE: Baba VV mie sa ivi naelekea Arusha kuna send off ya mfanyakazi mwezetu,mie ndo matron wake ntarudi baada ya siku tatu.(hiyo ni simu,yuko safarini tayari)
ME: Aaah sasa mbona hukuniambia kabla, sasa hiyo ndo tabia gani umeanzisha? Unaondoka kwenda mbali hivyo bila kuniomba ruhusa wala kunifahamisha?
KE: Unasemaje wewe? ruhusa?
ME:Aaa basi bana we nenda tu.
Wengine
KE:Mzee naenda kidogo pale tabu bar kuna kaka mmoja wa kazini kaniletea mzigo wangu,ntarudi sasa hivi.(saa nne usiku)
ME: Poa,mie ngoja nicheki Man U wanavyoadhibiwa leo.
RAFIKI: Mme wako kakuruhusu kutoka saa hizi kweli peke yako?
KE: Mie mume wangu mzungu ,hanaga shobo.
Wengine
KE:Baba Tii nasema hivi,hii gari mie siitaki tena,kwa sababu nimemwona dada mmoja hivi,anaendesha gari kama hii,nasema hivi,nataka gari mpya,ambayo hana mtu yeyeote hapa mjini.
ME: Wewe! gari hii si ina miezi sita tu?,na ulisema hii ndo toleo jipya,bana mie sina hela.
KE: Shika ufunguo wako,ntatembea kwa mguu,hata ile Prado siendeshi.
ME: Haya bana ntakununulia,
KE: Lini sasa
ME: Baada ya mwezi mmoja na nusu
KE:Mwezi na nusu kabisa?ntatembea kwa miguu tu
ME: Basi wiki mbili,mama
Wengine
ME:Mama K shilingi milioni mbili za nini tena wakati hata wiki mbili hazijaisha nilikupa milioni moja na nusu?
KE: Babu wee kama umenichoka nijue kabisaaa,mana naona siku hizi maswali yamekua mengi vile kama nipo kituo cha polisi,ukinipa hela usinipangie matumizi mie sio mtoto mdogo,kama hivyo basi kaa na hela yako.
ME:Mama K yaani kukuuliza hivyo tu ndo umenikasirikia namna hiyo mke wangu?,haya lete kitabu changu cha hundi,maana we huna dogo.

Na mengi mengineyo.
 
Mwanamke anaejitambua hakubali kufanya ujinga huo hata siku moja,sababu kumbuka kama wewe umefanya hivyo leo na yeye atakulipa jee utaweza kumeza?
 
Ni Dar peke yake ndo watapatikana/wanapatikana wanaume wa sampuli hiyo , maana hao huwa wanajinadi kuwa wana pesa
 
mmhh !! haya yote huwa yanawezekana tuu kwenye bongo movie lakini si huku kwetu uswahili tunakoishi
 
Mwanamke anaejitambua hakubali kufanya ujinga huo hata siku moja,sababu kumbuka kama wewe umefanya hivyo leo na yeye atakulipa jee utaweza kumeza?
Mkuu hujawahi kusikia hata aina fulani ya wanawake ambao wametajwa hapo juu,hata kama ni wachache lakini wanafanya vitu vya namna hiyo,najua sio wote.
 
mmhh !! haya yote huwa yanawezekana tuu kwenye bongo movie lakini si huku kwetu uswahili tunakoishi
Kuna mwanamke mmoja,tena ni mke wa mtu mkubwa tu anafanya mambo kama baadhi ya niliyoaniasha hapo juu.Na wengine wengi uswazi.
 
hayo ni matatizo ya kumdekeza sana mwanamke, lamba makofi tu...Unaleta mbishe za kipuuzi hapa!
Yani maishani usije ukaruhusu mwanamke akumudu maana hayo ndio madhara yake
 
Genero ukikamatwa na mwanamke utakua mpole tu.Chezea vitu vyote lakini suio papuchi.Wamenasa makasisi na mashehe,Majenero ndo usiseme kbs.
Hiyo kitu huwa haitokei kabisa kwa super general Galadudu, mi ndo huwa nawaendesha nitakavyo hawa viumbe kwa kutumia kanuni kali tu kama vle CHIZI ZOBA,NG'OMBE MAKENGEZA, NYEGELE,MKAMATE UMTULIZE na nyinginezo nyingi tu huwa hawapindui
 
Back
Top Bottom