Nadhani Tundu Lissu anamsaidia Rais Magufuli. Anasema ukweli ambao wana-CCM, wasaidizi, na washauri, wanaogopa kumwambia Magufuli

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,442
55,017
Vitisho anavyopokea Tundu Lissu vinatoka kwa wasaidizi wa Rais Magufuli ambao wameshindwa kumwambia bosi wao ukweli.

Wanamdanganya Rais Magufuli kuwa anatukanwa, lakini ukweli ni kwamba Tundu Lissu anasema mambo ambayo yalitakiwa yasemwe na washauri na wasaidizi wa Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameponzwa na watu wanaomshangilia kwa kila analofanya hata pale "anapochemka" waziwazi.
 
Watanzania tumeshuhudia maiti za watanzania wenzetu zikiokotwa kwenye fukwe zikiwa zimefungwa mawe na vyuma na nyingine zikiwa kwenye viroba.

Watanzania, tumeshuhudia wenzetu wakitekwa na kupotezwa, wafanyabiashra wakifilisiwa.

Tumeona ndugu na jamaa zetu wakifunguliwa makesi makubwa na yasiyo na dhamana.

Huyu mtu hatufai kabisa.
 
1597801576273.png
 
CCM imekuwa na makandokando mengi yaliyofanyika ndani ya miaka mitano iliyopita ya serikali ya awamu hii. Lakini njia nyingi zilitumika ili wananchi wasiweze kuyajua.

Mbali ya kutunga sheria na kanuni mbalimbali zenye kuminya uhuru wa kupashana habari, lkn walikwenda mbali na kuwaminya wapinzani ili wao pekee tu ndio waweze kufanya siasa za kitaifa. Badala ya kujenga taasisi imara ya ofisi ya Rais wao waligeuka na kumsifu mtu mwenye kuiongoza ndiye kila kitu ijapokuwa alikuwa na mapungufu mengi ya kiuongozi.

Sasa umotokea upenyo wa wapinzani kufanya siasa za kitaifa, na kutimiza wajibu wao wa kuikosoa serikali na yule mwenye kuiongoza. Kwa kuwa ilishazoeleka kwa miaka hii mitano ya kuwa Mkuu huwa hakosolewi, kwa hiyo pale mapungufu yake yanapowekwa wazi na Tundu Lissu inaonekana kama ni jambo geni nchini.

Uraisi ni cheo çha kikatiba kinachogombewa kupitia siasa, na mwenye kukistahili hukipata kupitia mchakato wa upigaji wa kura, na kuungwa mkono na wapiga kura wengi. Ni wakati wa CCM kujibu hoja zinazotolewa dhidi yao. Wasikimbilie visingizio vya uchochezi ama kutukanwa pale maovu yao waliyoyafanya yanapowekwa hadharani.
 
Vitisho anavyopokea Tundu Lissu vinatoka kwa wasaidizi wa JPM ambao wameshindwa kumwambia bosi wao ukweli.

Wanamdanganya JPM kuwa anatukanwa, lakini ukweli ni kwamba Tundu Lissu anasema mambo ambayo yalitakiwa yasemwe na washauri na wasaidizi wa JPM.

JPM ameponzwa na watu wanaomshangilia kwa kila analofanya hata pale "anapochemka" waziwazi.
Hao wasaidizi wake mnawaonea sana
 
Vitisho anavyopokea Tundu Lissu vinatoka kwa wasaidizi wa JPM ambao wameshindwa kumwambia bosi wao ukweli...
JPM anafanya mambo ya kweli na maendeleo. Wasaidizi wake wanakosea pale anapokengeuka na kutukana wananchi au wasaidizi wake hadharani.

Tumesikia
”wapumbavu” hata kwa wakurugenzi
”niawapiga mashangazi”
”unawashwa washwa”
n.k.......n.k.....!
 
JPM anafanya mambo ya kweli na maendeleo.Wasaidizi wake wanakosea pale anapokengeuka na kutukana wananchi au wasaidizi wake hadharani.

Tumesikia
”wapumbavu” hata kwa wakurugenzi
”niawapiga mashangazi”
”unawashwa washwa”
n.k.......n.k.....!
Kwa hiyo !
 
Kama watanzania watampa kura MEMBE sina tatizo.

Lakini kama watampa kula Lissu basi sitakuwa na tatizo na Magufuli.
 
Ukweli wa kusema rais hatakiwi kujisifu kujenga kinu cha umeme maana mtera ipo.

halafu viazi mbatata(sio makutano) waliopo naye jukwaani pale wanapiga kelele wakisema "mwambie baba mwambieeee".
 
upinzani ni sawa na simba na yanga , sasa kushindwa kulezena vizuri hakusababishi yanga au simba kutofaa . ili simba au yanga imara iwepo ni lazima mmoja wapo awepo n andiyo utamu wa mpira huo wa kishabiki .

napata shida sina kusikia wapinzani wanakufa , wanapigwa wanatekwa wananyimwa airtime radioni , katika tv . Maana yake huyo anayetaka iwe hivyo , ni Rahisi kuanguka . Time will tell .

kama tundu lissu asipozuiliwa na watawala . Anguko la ccm ni kubwa . Naomba tu chadema wakubaliane na kachero mmbobezi bernard membe waungane . Kuna kitu kitatokea .
 
Back
Top Bottom