Nadhani tunahitaji kura ya kutokuwa na imani na rais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nadhani tunahitaji kura ya kutokuwa na imani na rais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Haki Yetu, Aug 19, 2011.

 1. H

  Haki Yetu Senior Member

  #1
  Aug 19, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF

  Nimekuwa nikisoma mawazo ya watu hapa jamvini, nikisikiliza maoni ya watu mtaani, ofisini, kwenye vijiwe, kwenye vyombo vya habari na hata kwenye vyombo vya usafiri. Kwenye maoni na mawazo haya ni kwamba kila mtu analalamika juu ya kuongezeka shida hapa nchini kwetu. Umeme, mafuta, bei za vyakula, kushuka kwa elimu, mishahara ya watumishi, mikataba mibovu na utoroshwaji wa maliasili hayo ni machache tu.

  Maisha yamekuwa magumu sana, kashfa kila kona na nchi imepoteza uelekeo kabisa. Hakuna mwananchi wa kawaida hivi sasa mwenye matumaini na Serikali iliyoko madarakani. Wachache wanaoitetea ni wale kwa namna moja au nyingine wamepenyeza mirija yao ya kinyonyaji. Watu ambao wamenunuliwa kwa vibaba vya unga na mchele.

  Sasa tumekuwa tukilalamika sana, tumehoji uwezo wa Rais kiasi cha kutosha. Mimi napendekeza kwa wabunge hasa wale ambao ni wana jamvi wenzetu wapeleke hoja ya kutokuwa na imani na Rais.

  Najua itakua ni ngumu na inaweza kuletwa mizengwe hasa na Spika. Lakini haiwezekani kuendelea na malalamishi wakati hali inazidi kuwa mbaya. Kuvumilia miaka minne ijayo kwa mwendo huu tunaweza kutumbukia kwenye janga kubwa zaidi.

  Sijui wana jamvi wenzangu mnaona vipi kuhusiana na hili.

  Nawasilisha
   
 2. s

  smz JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wazo lako ni zuri, lakini najua itakuwa ngumu hata kupokelewa tu. Kumbuka juzi Mnyika alitaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Pinda. Kama unakumbuka uliona mwenyewe NS alivyoipangua.

  Najua itakuwa ngumu, kwa sababu hata ikikubaliwa mwisho wa siku zitapigwa kura, haya piga picha hapo, jamaa wako wengi. Ni wazi kwamba watashinda na jamaa ataendelea kupeta.

  Ila kama ikipelekwa itamshtua Mkulu kuona kwamba watu wameshapoteza imani na yeye. Ni wazo zuri watafute jinsi ya kupenyeza hoja hiyo.

  Naunga mkono mia kwa mia.
   
 3. m

  mtoto wa mama Senior Member

  #3
  Aug 19, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 186
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kama hauna imani nae si uandamane mwenyewe.. mnalaumu hata vtu ambavyo vpo nje ya uwezo wa mtanzania yoyote yule..sasa bei ya mafuta kwenye soko la dunia imepanda unataka kikwete afanye nn...
   
 4. o

  oldonyo JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mawazo yako ni mazuri hivyo yanaitajika kuwekwa katika katiba mpya na si raisi tu ata wabunge wanaodai posho kuongezwa kila dakika wakati watanzania hatuna maji,umeme na kukosekana kwa uduma nyingine za muhimu.
   
 5. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja.
  Hata kama magamba wataikwepesha itawaamsha kutoka usingizini.
   
 6. K

  Kiluvya2011 JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 215
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  <br />

  Hahaha...kweli ww mtoto wa mama, unaongea upupu tuu koz bado unanyonyeshwa na kufuliwa mpaka chupi kama inavyosema jina lako...

  Wapishe wenye kujitegemea kimaisha wanao jua ugumu wa maisha upoje ndo wajadili huu uzi
  <br />
   
 7. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  akuchumbie
   
 8. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2011
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Well said brother, bahati mbaya ni kwamba wanaofaidika na huu mfumo mbovu ni pamoja na hao waliopo humo humo bungeni hasa ukizingatia kwamba kila kitu kilishapangwa kitaalamu kiasi kwamba hakuna uadui kati ya serikali na wabunge ukizingatia kwamba wao walishaanza kulipwa posho ya mafuta ya shilingi 2,500 tangu mwaka 2000 hivyo kwa vyovyote vile hawawezi kuwa upande wetu.
   
 9. t

  takeurabu JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2011
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hata kama hiyo hoja ikitinga bungeni jee magwanda mnawabunge wa kutosha wa kui-support? je utamaduni huo upo nchini mwetu? kuna historia yoyote? navyofahamu mimi kura ya kutokuwa imani na JK imeshapigwa wakati wa uchaguzi octoba 2010 pale 61% walipoonyesha imani yao kwake ambapo nyie 39% (magwanda, mapanga shaa, na wengineo) hamkuwa na imani nae; ni vyema sasa mkajipanga na 2015 achaneni na mabo ya kufikirika
   
 10. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,826
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Ebu jaribu kuangalia mambo ki utu uzima kidogo,weka ushabiki na ujuha pembeni....Pia usitutukane watanzania wote kwa udhaifu wa M.kwere,kuna watu wana uwezo mkubwa wa kututoa hapa tulipokwama na kufanya hayo unayohisi kuwa hayawezekani.Kupanda kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia isiwe sababu ya kuhalalisha upuuzi wenu...ulishajiuliza ikiwa serikali na mamlaka zake wakipunguza tozo walau kwa 50% bei itabaki hii hii?
   
 11. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Tupo Pamoja Tuivimushe hii Hoja Hadi Mkwe''ere Aisikie nilishawahi toa Hii Hoja wengi waliikubali naona muamko huu umekaa sawia kwani ugumu wa maisha unasambaa kwa kasi kwa watu wengi wale ambao bado watafikiwa tu..

  TANGANYIKA BILA KIKWETE NDIO ITAENDELEA!
   
 12. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Kwa mwendo huu tanzania haihitaji Rais kwani hana kazi. kwa kifupi nchi hii ni yatima
   
 13. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Naunga hoja mkono asilimia mia moja! Na mimi nimeshaanza maandamano kutoka Rorya kuelekea ikulu ila sijajua nitafika lini manake ni safari ndefu kwa miguu!
   
 14. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2011
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,211
  Likes Received: 312
  Trophy Points: 180
  Katiba iliyopo sasa hairuhusu kuweko kwa kura ya kutokuwa na imani na Rais. Inaruhusu kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, lakini na Rais HAPANA.

  Kwa hivyo basi, cha kupigania ni kuwekwa kwa kipengele kama hicho kwenye katiba mpya.

   
 15. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,160
  Likes Received: 1,162
  Trophy Points: 280
  Ondoa neno "Nadhani" weka lazima, "tz inajiendesha bila rais tangu 2006!"
   
Loading...