Nadhani tulikosea kuwakabidhi Jeshi la Polisi kuchunguza tukio la mauaji ya Hamza

Hivi karibuni kulitokea tukio la kustua na kutisha Sana, ambapo kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Hamza, alipofika kituo cha Selander Bridge na kuwafyatulia risasi kwa kutumia bastola yake na kuwaua askari 2 na kuchukua "machine gun" yao na kuanza kuwasaka Polisi popote pale walipo na kuwafyatulia risasi huku akiwaacha raia wa kawaida bila kuwadhuru!

Mara moja iliundwa Tume ya kuchunguza mauaji hayo, iliyoundwa na askari watupu, ambapo naweza kuelezea kuwa kilichofanyika ni sawaswa na kesi ya ngedere kula mahindi umpelekee nyani kuchunguza!

Matokeo ya Tume hiyo iyoundwa ndiyo Iliyonishangaza zaidi.

Eti wanadai kuwa Hamza alikuwa gaidi ambaye alishirikiana na vikundi vya kigaidi vya Al- Shabab na ISIS Katika kutekeleza ugaidi wake!

Hata hivyo wanafamilia wake, wameshangazwa na ripoti hiyo iliyotolewa, kwani kwa namna wanavyomfahamu wao, wanaamini kuwa kijana wao hakuwa gaidi hata kidogo.

Kuna maswali ambayo ninataka kuwahoji hao mapolisi waliofanya uchunguzi wao na kuja na matokeo hayo ya upelelezi wao.

Swali la kwanza, ni kwanini Hamza aliwa-target maaskari pekee, na kuwaacha raia bila kuwadhuru?

Swali la pili, kumkabidhi raia yeyote silaha ya kujilinda, inafuatia "process" ndefu ambapo wao Polisi hadi wajiridhishe kuwa raia wanayempa silaha ya kujihami, hataleta madhara kwa raia wengine, je hiyo "process" ilifanyika Katika kumkabidhi silaha hiyo Hamza?

Swali la tatu, kama kweli Hamza alikuwa gaidi, ni kwanini intelejensia yao mapolisi hsikufanya kazi, hadi wakampa pistol "gaidi" huyo ili awadhuru watu wengine?

Swali la nne, huyo "gaidi" Hamza alifikia hatua ya kuwa mjumbe wa mikutano mkuu wa CCM wa Jimbo la Ilala, ni kwanini chama hicho cha CCM kisifutwe kwenye orodha ya vyama vya siasa nchini, kutokana na kuwalea magaidi?

Swali la tano, kwa kawaida Tume za aina hiyo ni lazima zieleze historia ya mtu huyo waliyemchunguza, ni kwanini Tume hii iliyoundwa haikutueleza historia ya ugaidi wake huyo kijana Hamza?

Kulifanyia "mzaha" suala zito kama hilo la ugaidi, ambalo linawatesa Sana nchi nyinginezo ni hatari Sana kwa mustakabari wa Taifa hili.

Nitoe wito wa kuundwa kwa Tume mpya itakayokuwa huru, itakayohusisha makundi mbalimbali Katika jamii yetu, kama vile majaji wastaafu na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa, ili tuweze kupata ripoti huru ya uchunguzi bila kuegemea upande wowote.
Umeandika mautopolo mareefu pumba tupu. Tukio limerekodiwa mwanzo mwisho live anaonekana anavyoshambulia na kujihami na.anasikika.akiongea wazi wazi.dhamira yake.kuwa.anafanya hivyo kwa ajili.ya.dini yake hao wachunguzi ulitaka waje na jibu gani. nadhani wewe mtoa mada una imani sawa na huyo gaidi na unaona alichokifanya kuua watu wasio na hatia waziwazi kwako ni sawa?
 
Hili Jambo Ni Kama Lile La Abdallah Zombe
Yaani Wajichunguze Wenyewe Halafu Wajikaange
Subiri Labda Sakata La Handeni La Police Kushika Nyeti Za Watu Nalo Ujanjaujanja Mwingi
Watasema Hakuna Lolote
 
Back
Top Bottom