Nadhani tulikosea kuwakabidhi Jeshi la Polisi kuchunguza tukio la mauaji ya Hamza

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Hivi karibuni kulitokea tukio la kustua na kutisha Sana, ambapo kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Hamza, alipofika kituo cha Selander Bridge na kuwafyatulia risasi kwa kutumia bastola yake na kuwaua askari 2 na kuchukua "machine gun" yao na kuanza kuwasaka Polisi popote pale walipo na kuwafyatulia risasi huku akiwaacha raia wa kawaida bila kuwadhuru!

Mara moja iliundwa Tume ya kuchunguza mauaji hayo, iliyoundwa na askari watupu, ambapo naweza kuelezea kuwa kilichofanyika ni sawaswa na kesi ya ngedere kula mahindi umpelekee nyani kuchunguza!

Matokeo ya Tume hiyo iyoundwa ndiyo Iliyonishangaza zaidi.

Eti wanadai kuwa Hamza alikuwa gaidi ambaye alishirikiana na vikundi vya kigaidi vya Al- Shabab na ISIS Katika kutekeleza ugaidi wake!

Hata hivyo wanafamilia wake, wameshangazwa na ripoti hiyo iliyotolewa, kwani kwa namna wanavyomfahamu wao, wanaamini kuwa kijana wao hakuwa gaidi hata kidogo.

Kuna maswali ambayo ninataka kuwahoji hao mapolisi waliofanya uchunguzi wao na kuja na matokeo hayo ya upelelezi wao.

Swali la kwanza, ni kwanini Hamza aliwa-target maaskari pekee, na kuwaacha raia bila kuwadhuru?

Swali la pili, kumkabidhi raia yeyote silaha ya kujilinda, inafuatia "process" ndefu ambapo wao Polisi hadi wajiridhishe kuwa raia wanayempa silaha ya kujihami, hataleta madhara kwa raia wengine, je hiyo "process" ilifanyika Katika kumkabidhi silaha hiyo Hamza?

Swali la tatu, kama kweli Hamza alikuwa gaidi, ni kwanini intelejensia yao mapolisi hsikufanya kazi, hadi wakampa pistol "gaidi" huyo ili awadhuru watu wengine?

Swali la nne, huyo "gaidi" Hamza alifikia hatua ya kuwa mjumbe wa mikutano mkuu wa CCM wa Jimbo la Ilala, ni kwanini chama hicho cha CCM kisifutwe kwenye orodha ya vyama vya siasa nchini, kutokana na kuwalea magaidi?

Swali la tano, kwa kawaida Tume za aina hiyo ni lazima zieleze historia ya mtu huyo waliyemchunguza, ni kwanini Tume hii iliyoundwa haikutueleza historia ya ugaidi wake huyo kijana Hamza?

Kulifanyia "mzaha" suala zito kama hilo la ugaidi, ambalo linawatesa Sana nchi nyinginezo ni hatari Sana kwa mustakabari wa Taifa hili.

Nitoe wito wa kuundwa kwa Tume mpya itakayokuwa huru, itakayohusisha makundi mbalimbali Katika jamii yetu, kama vile majaji wastaafu na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa, ili tuweze kupata ripoti huru ya uchunguzi bila kuegemea upande wowote.
 
"Sirro unaua waislam,lakini sisi vijana tunaomtetea Allah bado tupo(huku akijipiga piga kifua)" Aliskika Hamza!!
Ndipo hapo Tume hiyo ilitakiwa kuchunguza, ni kwa nini kijana huyo Hamza, awa-target maaskari na kuwaacha raia wa kawaida bila kuwadhuru??

That is the main question, which needs to be answered
 
Hakuna aliyewakabidhi polisi hilo jukumu, walikabidhi wenyewe kwasababu wao ndio wenye mamlaka ya kufanya hivyo, inahitajika professionalism ya hali ya juu toka kwa jeshi letu la polisi, waamue kuwaridhisha wananchi kwa kuwapa kile wanachotaka ( Tume huru ya uchunguzi) ili kuondoa dhana ya conflict of interest inayoonekana kuwaondolea polisi credibility ya kujifanyia uchunguzi.
 
Watanzania bhana!Wewe unahaha na matokeo ya tatizo badala ya kudeal na tatizo lenyewe.

Tatizo hapa ni Tanzania kukosa uongozi.Unahitaji kuwa na PhD ili kujua mambo madogo kama haya?

Wewe unapaswa kuhangaika na tatizo la nchi yako kukosa uongozi na siyo kuhangaika sijui na Polisi sijui na tume gani ya mavi.

Na Tanzania imekosa uongozi baada ya wananchi kuruhusu kudhulumiwa demokrasia yao na chama cha CCM.Kwa hiyo wananchi kwenye hili suala bado wao ndiyo tatizo.
 
Hakuna aliyewakabidhi polisi hilo jukumu, walikabidhi wenyewe kwasababu wao ndio wenye mamlaka ya kufanya hivyo, inahitajika professionalism ya hali ya juu toka kwa jeshi letu la polisi, waamue kuwaridhisha wananchi kwa kuwapa kile wanachotaka ( Tume hutu ya uchunguzi) ili kuondoa dhana ya conflict of interest inayoonekana kuwaondolea polisi credibility ya kujifanyia uchunguzi.
Kama wao wenyewe wanajua kuwa kuna conflict of interest, iweje wajikabidhi jukumu la kujichunguza??
 
Kwani tuna maamuzi, kila kitu wanaamua wakoloni CCM. Kuanzia nani awe mwenyekiti wa serikali za mitaa, kijiji, wabunge mpaka Rais. Na madaraka ya Rais ni makubwa sana.
IMG_20210707_085335_184.jpg

Hayo ndiyo yaliyotokea DRC
 
Hivi karibuni kulitokea tukio la kustua na kutisha Sana, ambapo kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Hamza, alipofika kituo cha Selander Bridge na kuwafyatulia risasi kwa kutumia bastola yake na kuwaua askari 2 na kuchukua "machine gun" yao na kuanza kuwasaka Polisi popote pale walipo na kuwafyatulia risasi huku akiwaacha raia wa kawaida bila kuwadhuru...
Yaani wamejua ni gaidi baada ya kufa. Lakini intelijensia yao haikujua wakati yu hai, akawa na bunduki binafsi, na akawa mfuasi mzuri wa chama tawala.

Kama haya yote hawakuyajua kabla kuwa ni gaidi, wanatia mashaka sn juu ya usalama wet kama nchi kung'amua wahalifu kabla ya kufanya madhara. Intelijensia huwa inakuwa vzr kwenye mikutano ya vyama vya upinzani tu lakini sio kwenye watu wengine hasa wenye unasaba na ccm. Ni aibu kubwa sn
 
"Sirro unaua waislam,lakini sisi vijana tunaomtetea Allah bado tupo(huku akijipiga piga kifua)" Aliskika Hamza!!
Kama naye Mkuu ametajwa na huyo Muuaji (ina maana amekuwa ni sehemu ya sababu ya Hamza kufanya yale aliyoyafanya) sasa hapo Polisi wanapataje Uhalali wa Kumchunguza mtu anayewatuhumu?
 
Yaani wamejua ni gaidi baada ya kufa. Lakini intelijensia yao haikujua wakati yu hai, akawa na bunduki binafsi, na akawa mfuasi mzuri wa chama tawala. Kama haya yote hawakuyajua kabla kuwa ni gaidi, wanatia mashaka sn juu ya usalama wet kama nchi kung'amua wahalifu kabla ya kufanya madhara. Intelijensia huwa inakuwa vzr kwenye mikutano ya vyama vya upinzani tu lakini sio kwenye watu wengine hasa wenye unasaba na ccm. Ni aibu kubwa sn
Tatizo kubwa ni pale polisi wanapofanya kazi kama genge la wahalifu.

Kuhusiana na kuzuia mikutano ya wapinzani kwa sababu za kipumb.avu kabisa na kubambikia watu kesi, hakuhitaji akili wala werevu, ni moyo wa kishetani tu unatosha.
 
Hivi karibuni kulitokea tukio la kustua na kutisha Sana, ambapo kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Hamza, alipofika kituo cha Selander Bridge na kuwafyatulia risasi kwa kutumia bastola yake na kuwaua askari 2 na kuchukua "machine gun" yao na kuanza kuwasaka Polisi popote pale walipo na kuwafyatulia risasi huku akiwaacha raia wa kawaida bila kuwadhuru!

Mara moja iliundwa Tume ya kuchunguza mauaji hayo, iliyoundwa na askari watupu, ambapo naweza kuelezea kuwa kilichofanyika ni sawaswa na kesi ya ngedere kula mahindi umpelekee nyani kuchunguza!

Matokeo ya Tume hiyo iyoundwa ndiyo Iliyonishangaza zaidi.

Eti wanadai kuwa Hamza alikuwa gaidi ambaye alishirikiana na vikundi vya kigaidi vya Al- Shabab na ISIS Katika kutekeleza ugaidi wake!

Hata hivyo wanafamilia wake, wameshangazwa na ripoti hiyo iliyotolewa, kwani kwa namna wanavyomfahamu wao, wanaamini kuwa kijana wao hakuwa gaidi hata kidogo.

Kuna maswali ambayo ninataka kuwahoji hao mapolisi waliofanya uchunguzi wao na kuja na matokeo hayo ya upelelezi wao.

Swali la kwanza, ni kwanini Hamza aliwa-target maaskari pekee, na kuwaacha raia bila kuwadhuru?

Swali la pili, kumkabidhi raia yeyote silaha ya kujilinda, inafuatia "process" ndefu ambapo wao Polisi hadi wajiridhishe kuwa raia wanayempa silaha ya kujihami, hataleta madhara kwa raia wengine, je hiyo "process" ilifanyika Katika kumkabidhi silaha hiyo Hamza?

Swali la tatu, kama kweli Hamza alikuwa gaidi, ni kwanini intelejensia yao mapolisi hsikufanya kazi, hadi wakampa pistol "gaidi" huyo ili awadhuru watu wengine?

Swali la nne, huyo "gaidi" Hamza alifikia hatua ya kuwa mjumbe wa mikutano mkuu wa CCM wa Jimbo la Ilala, ni kwanini chama hicho cha CCM kisifutwe kwenye orodha ya vyama vya siasa nchini, kutokana na kuwalea magaidi?

Swali la tano, kwa kawaida Tume za aina hiyo ni lazima zieleze historia ya mtu huyo waliyemchunguza, ni kwanini Tume hii iliyoundwa haikutueleza historia ya ugaidi wake huyo kijana Hamza?

Kulifanyia "mzaha" suala zito kama hilo la ugaidi, ambalo linawatesa Sana nchi nyinginezo ni hatari Sana kwa mustakabari wa Taifa hili.

Nitoe wito wa kuundwa kwa Tume mpya itakayokuwa huru, itakayohusisha makundi mbalimbali Katika jamii yetu, kama vile majaji wastaafu na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa, ili tuweze kupata ripoti huru ya uchunguzi bila kuegemea upande wowote.
Kwanini polisi walijichunguza wenyewe? Nani anaweza kujichunguza mwenyewe kama mtuhumiwa halafu akaleta ripoti ya kujimaliza mwenyewe?
 
Ogopa sana mtu anayefanya jambo na haraka haraka anakimbilia kum-ambuse mwingine. Polisi walijipa kazi ili kujiondoa kwenye hatia ya kuwa chanzo cha tukio.
 
Kama POLISI Walikuwa WANATUHUMIWA na HAMZA Je ulitarajia POLISI waseme HAMZA ni RAIA MWEMA?

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom