Consigliere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 12,037
- 24,626
Wote nadhani mngali mnakumbuka ile kauli ya kuwa iwapo bunge litapiga kura ya kutokua na imani na waziri mkuu basi yeye, rais atamrudisha tena na kama bunge litamkataa basi yupo tayari kulivunja bunge na ili turudi kwenye uchaguzi mkuu.
Kwanini rais alipata hisia ya kwamba bunge linaweza likapiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu? Inasemekana mkuu huyo wa mkoa aliitwa ili kuhojiwa na bunge lakini akakataa, na sababu ya kukataa kwake ingawa si aliyoitoa kwa bunge, ni kwamba mkuu wake alimkataza kutoenda, ila baada ya kutoa vitisha hivyo kwa wabunge wa chama chake, ikawa dhahiri kwamba yeye ndiye aliyemzuia kwenda kuhojiwa.
Ni kipi ambacho hakikueleweka? Hapa ni dhahiri kuwa rais aliwatisha wabunge ambao walikua wanamnyooshea vidole mkuu huyo wa mkoa. Kwake ni heri nchi irudi kwenye uchaguzi mkuu kuliko kumuwajibisha mtu huyu, kwake mtu huyu ni zaidi ya thamani yoyote ile ipatikanayo duniani... kama msimamo wake ni huo, je kuna yeyote anashangazwa na yaliyomkuta Nnape? Mnadhani Nnape au Chombo cha habari ni zaidi ya bunge?
Nape ni shujaa 'aliyefia' vitani, binafsi nilishaujua mrejesho utakaokuja kutokana na kamati ile ni lazima umpige usoni Nnape, lakini pamoja na hayo kamwe simlaumu Nape,kwani amefanya jambo sahihi. Ni heri ukawajibishwa ukitimiza wajibu wako, Nnape aliamua bora apigwa risasi akiwa amesimama kuliko kuchagua kuishi akiwa amepiga magoti.
Kuna mengi alifanya Nnape ambayo yalikera sana watu, tangu akiwa katibu wa siasa na uenezi, na hata kipindi cha kupitishwa kwa sheria ya habari na majibu aliyokuwa akiyatoa. Lakini kwa siku za karibuni, nimemuona Nnape yule ambaye nilimfahamu miaka ya kabla ya 2008. Kwa hili la Nnape kufukuzwa uwaziri linamuonodoa from SHAME and moved him to FAME.
Kiuhalisia CCM ipo katika wakati mgumu sana kwa sasa, na yeyote abishaye kuhusu hili ni punguani ambaye wakti huu kwake una faidi zaidi kwa maslahi yake. CCM ndiyo dominant katika nchi hii, mara chache wanazosinzia na kupuuzia mambo nchi huyumba na kutikisika sana, lakini mara hii walichokifanya kinaobomoa nchi. CCM ina karata moja tu mkononi, nayo ni kutumia wingi wa wabunge wake bungeni kuirudisha nchi kwenye mstari. Cha kufanya warudi kwenye katiba tu, maana sababu ni nyingi kuliko zinazohitajika.
Nchi ni yetu sote, si ya mtu au kikundi cha watu fulani.