Uchaguzi 2020 Nadhani ni wakati muafaka kwa red brigade, kitengo cha kumlinda Lissu kuanza kupewa posho

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,482
20,426
Jana maeneo ya Mabatini jijini Mwanza nilishtuka baada ya kuona wale walinzi maalum walipoanza kugombea maji ya chupa ambayo yalikuja katoni moja na hivyo kutokutosha wote.

Hali ile ilinishtua hasa ikizingatia kuwa mgombea urais alikuwa amefika tayari na hiyo ingetoa upenyo kwa MTU yoyote kumdhuru Lissu. Ni wakati mzuri kuanza kuwapa chochote hawa makamanda waweze kujikimu hata na vitu vidogovidogo kama maji, vocha nk sio tu ruzuku kuishia huko juu.

Pamoja na mambo mengine nilishtushwa na uhafifu wa vyombo vya muziki ambapo yalikuwa yakisikika maneno 3 kati ya 5.
Pia ni wakati muafaka wa Chadema kutafuta vyanzo vya uhakika vya mapato kuliko hiyo hali ya kupitisha kikapu kwenye kila mkutano
 
Back
Top Bottom