Nadhani ni muda mwafaka sasa JF Founder Maxence Melo akapewa Tuzo kubwa kwa juhudi zake

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,546
108,874
Nikianza kumuelezea nadhani sitomaliza hapa ila niseme tu kwamba nahisi kama Member pamoja na Members wengine wa huu Mtandao wetu pendwa na hata Watanzania wengine wenye Kupenda uhuru wa mawazo na habari hatujamtendea haki ' stahili ' Mwanzishaji wa Mtandao huu wa JamiiForums Ndugu Maxence Melo.

Naomba Kuundwe na Kamati ' Maalum ' itakayoratibu zoezi zima na kumuandalia ' Tuzo ' ya Kutukuka kabisa huyu Mpendwa wetu na Ndugu yetu ili mwishowe tuje ' Kumtunuku ' Heshima kubwa ambayo kila akiwa anakaa na akiitizama basi ataona jinsi tunavyomthamini kama ambavyo Yeye anatuthamini, anatupenda na anatulinda sana.

Ni wakati mwafaka sasa wa kumuenzi bila kuchelewa na hiyo ' Tuzo ' isiwe ni ilimradi tu ' Tuzo ' bali iwe kweli ni ' Tuzo ' ambayo pengine hakuna Mtu mwingine yoyote aliyewahi kubahatika kupewa hata nchini Tanzania.

Ombi langu hili likipokelewa na kufanyiwa Kazi nitafarijika mno. Akhsanteni

Nawasilisha.
 
Kabisa mkuu.. Itakuwa sio sawa tukinyamazia Juhudi za Melo.
> naunga mkono hoja
 
Mnatest serikali eeeh?

Maxence Melo kupewa ' Tuzo ' yake na Sisi Wadau na Kauli yako ya kwamba tunaijaribu Serikali vinahusiana vipi? Tafadhali kama Wewe ni mmoja wa wale ambao hamuupendi kabisa huu Mtandao wa JamiiForums na mnautaka ' Ufe ' ondoka tu mapema katika huu ' Uzi ' usije ukaiamsha sasa hivi ' Mizimu ' yangu ya Kizanaki, Kitutsi, Kimakuwa na Kiyao kisha yakawa mengine hapa.

Na aliyekuambia kuwa Watu wa Serikalini siyo Members wa JF ni nani? Kwa kukusaidia tu sasa ni kwamba 75% ya Watumiaji na ' Wakodoleaji ' wakubwa wa huu Mtandao ni Watu hao hao kutoka huko Serikalini na si hivyo tu bali 95% ya ' Ufanisi ' mkubwa wa Watendaji wa Serikalini unatokana na mawazo bora yenye ' madini ' ya kutosha kutoka hapa hapa kwa Members wa JamiiForums.

Hata kama siyo leo au kesho au keshokutwa ila JF Founder Maxence Melo ipo siku tutampa ' Tuzo ' yake ya uhakika.
 
Ni kweli kabisa kwa juhudi alizofanya kwa kushirikiana na wenzake bila shaka anastaili,maana jamii forum ni kama sokoni kila bidhaa unayoitaka ipo iwe biashara,Michezo,mahusiano na bidhaa zote .heshima kwako Melo.
 
Mungu Ni Mwema Wakati Wote
Hadi Sasa Juhudi Zake Zinaonekana
Akimaliza Kazi Atavalishwa Taji
 
Naunga mkono, pendekeza pia modality ya utekelezaji wa pendekezo lenyewe. Pendekezo langu tuzo iambatane na pesa taslim. Members tuchangie kwa hiari kiwango cha chini sh 10,000/=
 
Tatizo la jamii forums siku ya tuzo members hawataonekana kwa kudhani kwamba watajulikana. Humu kuna watu wengi wa kila kaliba ila sasa hata mtu unaemjua kabisa ni member humu hadi id yake unaifahamu ukimuuliza wewe ni member active wa jf huwa anaishia kujibu ndio ila huwa nasoma tuu post za watu except wale verified users only.
Yaani huu mtandao umekuwa kama freemasons especially kipindi hiki cha mtapata tabu sana
 
Back
Top Bottom