mtundu27
Member
- Jul 17, 2018
- 78
- 123
Habarini wadau. Natumai mmeamka salama na mmeanza shughuli za kujiongezea mapato.
Nadhani hii nchi ilipofika kuna uhitaji mkubwa wa katiba mpya itakayopunguza nguvu za urais pamoja na kumfanya kila mtanzania kujihisi yuko huru kwenye nchi yake.
Nasema haya sababu mambo yanayoendelea yanaumiza pamoja na kufedhehesha. Tumemsikia juzi juzi mwenyekiti wa uvccm akitoa kauli za ajabu kabisa, zenye kuleta ubaguzi wa wazi lakini si polisi wala msajili aliyekemea.
Juzi kajiuzulu waitara jana ndugai kwa haraka kashapokea barua kama ile ya lipumba kuhusu wabunge, hivi haki iko wapi? Majibu kuhusu kushambuliwa kwa lissu hadi leo hatujasikia aliyekamatwa.
Jana tena mbunge wa monduli kajiuzulu kisa kuunga mkono juhudi za rais, mimi nadhani mtu akijiuzulu kwasababu hiyo, kwanza hilo jimbo ateuliwe tu mtu wa chama alichotoka mpaka uchaguzi mkuu maana haya mambo si sawa, waitara kajiuzulu akisema alihoji matumizi ya ruzuku ya 237milioni kwa mwezi akatishwa, huku akisahau kujiuzulu kwake na kuitisha uchaguzi mpya ni zaidi ya bilioni 2.
Rais anasema anapigania watanzania wa hali ya chini na maendeleo hayana vyama, hizi kauli zinafika mahali zinakwaza tu. Matumizi ya trilioni na nusu hayajulikani, matumizi ya chato hamna anayehoji, kila mtu kimya maana ukiongee wata 'ku pyu pyu' ila wao ni ruksa kufanya chochote. Ifike mahali tuheshimu utu pamoja na kudai katiba mpya.
Karibuni tujadiliane

Last edited by a moderator: