Nadhani kama hutojiuliza maswali then huna haki ya kuilaumu serikali ya Magufuli

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Kwa tathmini ya mwenendo wa uchaguzi kwa awamu hii naona vyama vyetu vikuu vya siasa nchini na wanachama wake hawana haki katika kudai maendeleo!
Wanaruhusiwa kutamani maendeleo, lakini hawana haki ya kudai maendeleo katika serikali ya Magufuli!Ukifanyia analysis kampeni zilivyokuwa lengo kuu la vyama na watu wao lilikuwa ni kundi lipi litawale bila ya kuzingatia tunawahitaji wakafanye nini!

Makundi yalitawaliwa zaidi na utashi wa vyama vya siasa na priority ilikuwa vyama hivyo vishinde tu! Lakini pia kulikuwa na kuyakubali au kuyakataa baadhi ya makundi kama dini zetu, kabila zetu, kanda zetu etc! Sasa nafasi ya kufanya uchaguzi umepita, tumeshachagua watu wa vyama vyetu bila ya kujali uwezo, dini, kabila au kanda zetu lakini suddenly tumebadilika na kuanza kudai maendeleo!

Maswali haya ni ya msingi kabla ya kuanza kulaumu:-
  1. Je kiongozi uliyemchagua aliahidi hayo maendeleo.
  2. Je alielezea process za kuyafikia hayo maendeleo?
  3. Je yupo katika hatua zipi za maendeleo alizoahidi?
  4. Je unapimaje kama ameyafikia malengo?
    1. Ni indicators zipi unazitumia kupima hayo malengo?
    2. Zina match na za mgombea wako?
    3. Kuna time frame?
    4. Zipo specific?
  5. Je chaguo lako lilizingatia maendeleo au zile factors zingine kama dini, kabila, chama etc?
    1. Je haitoshi kuwa kiongozi wa chama, kabila au dini yako ameshinda kama ulivyotarajia?
    2. Je uliyemchagua anajua matarajio yako?
    3. Je unamsaidia huyo kiongozi wa dini/kabila/chama chako kufikia malengo mliyojipangia?
    4. Je kweli huyo mtu wako ana uwezo wa kuyafanya hayo mnayoyatarajia!
 
Back
Top Bottom