Nadhani ifike mahali tutafute maana halisi ya kiongozi hasa anayetokana na mfumo wa siasa

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
201
1,534
Nadhani ifike mahali tutafute maana halisi ya kiongozi hasa anayetokana na mfumo wa siasa. Achana na viongozi wa dini, taasisi na mashirika mbalimbali. Tuzungumzie hawa viongozi wa siasa. Unapotafuta nafasi ya uongozi kupitia siasa focus yako ni nini? What is your primary objective?

Viongozi wanapaswa kuumizwa na changamoto za wananchi ili kuwa sehemu ya kutafuta majawabu ya changamoto hizo. A leader must provide alternatives towards socio-economic and political catastrophe in his/her society. Lakini je ni viongozi wangapi wanaopigania nafasi za uongozi kwa sababu ya kuguswa na changamoto za jamii zao?

Lipo kundi linaloibuka kwa kasi ambalo ni viongozi maslahi. Hawa wapo kwenye vyama vyote (tawala na upinzani), rika zote na nchi zote (hasa kwenye nchi zetu za kiafrika).
Hawa wanapotafuta nafasi za uongozi huvaa ngozi bandia. Hujitambulisha kama watetezi wa wananchi lakini moyoni wana malengo yao.

Ndio maana unaweza kukuta mtu anaishi eneo lisilo na maji. Anapotafuta uongozi kilio chake kikubwa ni maji, lakini akipata uongozi anawaacha wananchi wake kwenye changamoto ileile ya maji, yeye anahamia eneo lenye maji. Na nguvu ya kudai maji inapungua kwa sababu yeye sio mhanga tena wa kukosa maji. Maslahi binafsi.

Wapo wabunge ambao walikuwa watumishi. Na walikuwa wakilia sana makato makubwa ya PAYE kwenye mishahara ya watumishi. Lakini walipopata ubunge kelele za PAYE zikakoma, simply kwa sababu mbunge hakatwi PAYE. As long as yeye sio victim tena wa PAYE basi kelele zinaisha. Hii ndio aina ya viongozi tulionao.

Wapo wanaopigania uongozi ili kulinda mali zao, kuongeza network ya biashara, kupata heshima ya madaraka, na wengine hutumia uongozi kama njia ya kutafuta fedha na kujilimbikizia mali. Viongozi wa aina hii wanapoona upande waliopo unawachelewesha kufikia malengo yao ni rahisi sana kuhamia upande mwingine.

Mhe.Lucy Magereli ametuambia kuwa ndugu Mwarwa Ryoba alianzisha kiwanda cha kusaga kokoto. Ni jambo jema. Lakini mradi huo ulikwamishwa na serikali ya CCM. Alifungiwa milango hata akiomba tender hapewi, na hivyo kujikuta anajiendesha kwa hasara.

Lakini sasa amehamia CCM. Ana uhakika kiwanda chake kitaanza kujiendesha kwa faida. Atapewa tender mbalimbali za kusupply kokoto kwenye miradi ya serikali hasa ya majengo na barabara. Hapo lengo lake litakuwa limetimia.

Kwahiyo inawezekana nia yake haikuwa kuhangaikia changamoto za maji, umeme, na barabara kwa watu wa Serengeti, bali kutumia ubunge kama ‘stepping stone’ ya kufanikisha malengo yake kibiashara kama hicho kiwanda cha kokoto na mengineyo.

Baadhi ya watu hawaoni uongozi kama fursa ya kuwatumikia wananchi, bali fursa ya kumaliza changamoto zao kiuchumi. Hapa ndipo unakuta mtu akikosa nafasi ya uongozi anajenga chuki au anahama chama. Hujawahi kuona watu walikuwa active sana kwenye siasa lakini baada ya kukatwa kwenye kura za maoni au kukosa ubunge/udiwani wakapoa kabisa au wakahamia vyama vingine?

Ndio maana napenda zaidi harakati kuliko vyeo vya kisiasa. Harakati ni endless, lakini vyeo vya kisiasa vina-fade pale unapokosa position. Kinachokufanya ufanye harakati ni changamoto za jamii, lakini mara nyingi kinachokufanya ufanye siasa ni kuwinda position.

Mwanasiasa bora ni yule ambaye ni mwanaharakati pia. Ambaye changamoto za jamii ndizo zinazompa msukumo wa kusonga mbele. Mtu wa aina hii awe na nafasi ya uongozi au asiwe nayo hawezi kuacha kupigania wengine. Political activists are the leaders without titles.

Mwaka 2014 nilishauriwa sana kugombea uongozi BAVICHA. Sikuwa tayari, lakini siakuacha harakati. Sikuwahi kupoa, sikuwahi kurudi nyuma kwa sababu sikutegemea title ili kufanya kazi. Kuna waliopewa "titles" lakini wakashindwa kuzitumia wakassurender.

Mwaka 2015 tuliji-organize vijana watatu kufanya ziara ya kuzunguka nchi nzima kuwanadi baadhi ya wagombea ubunge. Mimi, Dr.Chriss Cyrilo na Engineer Pamela Maassay. Hatukuwa na nafasi zozote za uongozi ndani ya chama. Tulitimiza wajibu wetu kama wanachama wa kawaida.

Kwa kutumia rasilimali zetu wenyewe tulizunguka mikoa 20 kwa muda wa zaidi ya miezi miwili kuwanadi wagombea ubunge, udiwani na mgombea Urais Mhe.Lowassa. Tulinunua bendera 200, tukaenda Ngome kuu ya chama wakatuongezea bendera 500, na mabango kadhaa. Tukaweka kwenye buti. Tukaanza safari.

Tulisafiri usiku na mchana kuvuka mabonde na milima. Kuanzia Ilala kwa Muslim Hassanali hadi Moshi Vijijini kwa Anthony Komu. Kuanzia Rombo kwa Joseph Selasini hadi Shinyanga kwa Patrobas Katambi. Kuanzia Bunda kwa Ester Matiko hadi Bahi kwa Mathias Lyamunda. Kuanzia Nyamagana kwa Ezekiah Wenje hadi Vwawa kwa Fanuel Mkisi.

Kuanzia Tarime Vijijini kule Sirari kwa John Heche hadi Kilolo kwa Brian Kikoti. Kuanzia Tarime mjini kwa Ester Matiko hadi Isimani kwa Patrick Sosopi. Kuanzia Siha kwa Godwin Molel hadi Urambo kwa Sam Ntakamulenga. Na mikoa mingine kama Njombe, Ruvuma, Tabora, Singida, Morogoro, Arusha etc.

Haikuwa kazi rahisi. Tulifanya kazi mchana na kusafiri usiku, kila siku kwa siku 60. Tulipokezana kuendesha gari. Ukichoka unampa mwingine wewe unapumzika. Ukiamka unanawa uso unarudi kwenye usukani. Mchana tupo jukwaani, usiku tupo barabarani. Hii 'spirit' sielewi ilitoka(ga) wapi. Nawauliza(ga) Cyrilo na Pamela tuliwezaje, hata wao hawajui. It was only by GOD.

Tulijikimu kwa kila kitu. Tulijua wagombea wetu wengi walikuwa na mahitaji mengi kuliko hali zao za kiuchumi. Kwahiyo hatukutaka kuwaongezea mzigo. Tulipofika tulihakikisha kuanzia malazi, chakula, service ya gari na mafuta ya gari ni jukumu letu.

Tuligawa bendera kila tulipopita, na baadhi ya majimbo tuliwassupport wagombea hela ya mafuta kwenye gari zao. Kazi ya mgombea ilikuwa ni moja tu. Kutukabidhi microphone na kutuonesha jukwaa lilipo. Ni jimbo moja tu ambako mgombea alikuwa ametufanyia booking hotelini na amelipia. Tulipofika akatuhamisha tuliposhuklia na kutupeleka alipokuwa amepaandaa.

Tuliyafanya yote hayo kwa moyo mweupe. Bila kulipwa, bila kutumwa wala kusukumwa. Nakumbuka tulipofika Mwanza rafiki yetu mmoja alikuja kutufuata pale Lakairo. Baada ya kubadilishana mawazo akatutania ‘tugawane basi hizo pesa za kampeni’. Tukamuuliza zipi? Akajibu 'hizo mlizopewa kuzunguka nchi nzima kumnadi Lowassa". Tukageukiana tukacheka. Hatukutaka kumwambia kwamba tumeji-finance wenyewe kwa sababu 'obvious' asingeamini.

Ni watu wachache sana wanaoweza kujitoa bila kutegemea ubunge, udiwani au nafasi yoyote ya uongozi. Sisi tulitimiza wajibu wetu kama wanachama wa kawaida wa Chadema na tulifurahia kufanya hivyo. Hatukuwa na fedha kuliko wengine, ni moyo tu wa kujitoa kwa ajili ya chama. Kuna wenye fedha nyingi lakini hawawezi kufanya tuliyofanya, kwa sababu hawana moyo huo.

Dada yangu Ester Bulaya aliniambia "Malisa nilikua sikufahamu, lakini kazi mliyoifanya Bunda siwezi kuisahau. Mmesafiri maelfu ya kilomita kuja kuniombea kura. Siku tatu mlizokaa Bunda ni za thamani sana. Mmenyeshewa hadi mvua mkiwa jukwaani kwa ajili yangu"

Mwaka 2015 niligombea Moshi vijijini kupitia kura za maoni. Lakini kura hazikutosha. Sikuvunjika moyo, sikurudi nyuma, sikuacha siasa. Nilienda Moshi kumnadi kaka yangu Anthony Komu aliyepewa ridhaa na chama. Nilizunguka nae maeneo mbalimbali kumuombea kura, akashinda.

Lakini leo utakuta mtu anapambana kumbe lengo lake ni kutaka ubunge, udiwani au nafasi fulani ya uongozi. Na akikosa anakuwa disappointed na huo ndio unakuwa mwisho wake katika siasa. Unajiuliza huyu mtu ni kweli alitaka changes, au alitaka kutimiza tu maslahi yake binafsi kupitia siasa? Jiulize wale "wanaharakati" wote waliokuwepo 2014/15 leo wako wapi? Watu wa aina hii hata wakipewa nafasi, ni rahisi kusaliti wananchi endapo wakiahidiwa maslahi makubwa zaidi.

Nadhani Upinzani tunahitaji kufanya vetting makini zaidi ya kuwapata viongozi wetu. Wapo wengi wanatumia upinzani kama kichaka cha kutimiza malengo yao binafsi. 2020 tutawaona watakavyopukutika.

Tunahitaji viongozi ambao Upinzani kwao ni falsafa, ni itikadi ni Imani. Wasioshawishika, wasiopoa, wasioyumba bila kujali changamoto wanazopitia.!

Malisa GJ
 
Unahangaika sana kujipigia debe ili uonekane mbele ya macho ya Mbowe lakini wapiiiiiiiiiii.

Kwa taarifa yako Chadema ni saccos ya Mbowe anachagua mtu wa kufanya nae kazi ,si kwa sababu anaandika sana mtandaoni . Kinachokufanya Mbowe akuteue ni mpaka ukubali kulamba miguu na kufua mikoti yake kwa miaka kadhaa ,au kwa upande wa viti maalumu ukubali kumzalia.
 
Wewe mbowe amekuzalisha watoto wangapi?
 
Unahangaika sana kujipigia debe ili uonekane mbele ya macho ya Mbowe lakini wapiiiiiiiiiii.

Kwa taarifa yako Chadema ni saccos ya Mbowe anachagua mtu wa kufanya nae kazi ,si kwa sababu anaandika sana mtandaoni . Kinachokufanya Mbowe akuteue ni mpaka ukubali kulamba miguu na kufua mikoti yake kwa miaka kadhaa ,au kwa upande wa viti maalumu ukubali kumzalia.
Utasema kwamba yeye ndio kapost hapa... mtafute ukamchambe huko kwenye page zake.
 
Malisa , umeandika vizuri. Umeandika kwa uchungu naisoma mood yako kupitia haya maandishi. Hili ni tatizo kubwa tulilonalo wachache sana wenye dhamila ya kweli kuhusu ukombozi. Katika nyakati ngumu kama hizi ambazo watu wengi wamebanwa katika kila kona ni rahisi sana kwa wenye mioyo laini kuzikimbia harakati.

Kupigania haki hapa kwetu ni kijikana nafsi yako. Kupigania haki hapa kwetu kuna ghalama kubwa sana . Utanyimwa tenda kila mahali .Utanyimwa ajira ,utadhalilishwa, utapigwa na kutukanwa. Swali wangapi wanaweza kuvumilia haya?

Hizi ni nyakati ngumu sana. Ni katika nyakati hizi wapigania haki wa kweli ndipo watakapopatikana. Kitaibuka kizazi kipya kabisa kitakacholeta mabadiliko ya kweli.Tuombe uzima ,wakati ni msema kweli.
 
Wapo wabunge ambao walikuwa watumishi. Na walikuwa wakilia sana makato makubwa ya PAYE kwenye mishahara ya watumishi. Lakini walipopata ubunge kelele za PAYE zikakoma, simply kwa sababu mbunge hakatwi PAYE. As long as yeye sio victim tena wa PAYE basi kelele zinaisha. Hii ndio aina ya viongozi tulionao.

Na hili la PAYE nilitegemea Mhe. Raisi alione kwa kuleta sheria ambayo itahakikisha kila mtumishi Nchi hii analipa PAYE hii ni pamoja na Yeye . Raisi wa wanyonge lazima aondoe ubaguzi btwn waheshimiwa na walala hoi.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Mwanasiasa bora ni yule ambaye ni mwanaharakati pia. Ambaye changamoto za jamii ndizo zinazompa msukumo wa kusonga mbele. Mtu wa aina hii awe na nafasi ya uongozi au asiwe nayo hawezi kuacha kupigania wengine. Political activists are the leaders without titles.

Big Up Malisa.
Na hili wapiga kura wengi huwa hawalioni.
 
Unahangaika sana kujipigia debe ili uonekane mbele ya macho ya Mbowe lakini wapiiiiiiiiiii.

Kwa taarifa yako Chadema ni saccos ya Mbowe anachagua mtu wa kufanya nae kazi ,si kwa sababu anaandika sana mtandaoni . Kinachokufanya Mbowe akuteue ni mpaka ukubali kulamba miguu na kufua mikoti yake kwa miaka kadhaa ,au kwa upande wa viti maalumu ukubali kumzalia.
Duh aisee rudi shule tuu kwa kweli hakuna namna hii itapunguza kamasi humo kichwani mwako na itakuwa faida kwako na kwajamii inayokuzunguka kwa kweli
 
Nadhani Upinzani tunahitaji kufanya vetting makini zaidi ya kuwapata viongozi wetu. Wapo wengi wanatumia upinzani kama kichaka cha kutimiza malengo yao binafsi. 2020 tutawaona watakavyopukutika.

Tunahitaji viongozi ambao Upinzani kwao ni falsafa, ni itikadi ni Imani. Wasioshawishika, wasiopoa, wasioyumba bila kujali changamoto wanazopitia.!

Malisa GJ

Nadhani hata hatufai kuwaita wapinzani. Tuwaite Raia Wema/Wazalendo. Rejea Mwalimu Julius Kambarage Nyerere;

uongozi wetu na hatima ya tanzania - JamiiForums
1538313440936.png

Tatu, matukio mawili yenye kuhusiana yalitishia moja kwa moja Muungano wa Tanzania kama ulivyo sasa yaani wenye muundo wa serikali mbili. Suala la Zanzibar kujiunga kwenye Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (Organisation of Islamic Countries/Conferences -OIC) mwaka 1992 kulihusiana moja kwa moja na baadhi ya wabunge wa kutoka bara (waliojulikana kama G55) kutaka kudai kurudishwa kwa Serikali ya Tanganyika. Haya mawili (la OIC na hoja ya Tanganyika) bila ya shaka yalikuwa ndiyo sababu kubwa ya Mwalimu kuvunja ukimya na kuandika kijitabu hiki kuelezea kilichotokea miezi michache nyuma yake akijaribu kujenga hoja ya kuokoa mfumo wa muungano ambao yeye aliuasisi. Kwa kupitia kijitabu hiki Watanzania wanapatiwa nafasi ya kuyaelewa mambo yanayofanywa nyuma ya pazia jeusi la serikali na Chama tawala.

Hivyo, wakati Mwalimu anaandika kijitabu hiki alikuwa na lengo la kutupa mwanga wa kile ambacho kwa namna nyingine yoyote ile tusingeweza kukijua. Taifa letu linamuwia Mwalimu deni kubwa na la kihistoria. Kueweza kuelewa uzito wa hili ni muhimu kukumbushia jinsi ambavyo taifa la Marekani liliposimamia Muungano wake siyo kwa uzuri wa hoja bali kwa nguvu ya mtutu pale wanasiasa wa majimbo ya Kusini walipotaka kujitenga na ndugu zao wa Kaskazini na kumlazimisha Rais Abraham Lincoln kwenda vitani na ndugu zao. Kwa Tanzania, Muungano wetu umetetewa kwa nguvu ya hoja na taifa letu bado liko moja. Hatuna budi kujivunia tunu hii, kuilinda na kuendeleza utetezi usio na utata wa taifa letu; hata pale walioko madarakani wanaposhindwa kufanya hivyo.
 
Makala nzuri sana. Ila kos kubwa walilofanya upinzani ni kuua imani ya wanachama wao baada ya kumkubali lowasa ambaye ndio alioeonekana kamaadui no 1 enz hizo. mfano uislam hauwezi back salama kama pengo awe muislam na kuw shekh mkuu lazima iman za watu zitattreka kama ulivyosasa upinzan
 
"Mwanasiasa mzuri ni yule ambaye pia ni Mwanaharakati"

Kuna mjadala katika hili kwa siku za mbeleni sio leo kwa homa hii ya Yanga itakapoifunga Simba leo!

Otherwise kama kawaida yako, umeandika kisomi na kwa lugha nyepesi kueleweka pasipo kuumiza hisia za wale wanaopingana na mtizamo wako!
 
Nadhani ifike mahali tutafute maana halisi ya kiongozi hasa anayetokana na mfumo wa siasa. Achana na viongozi wa dini, taasisi na mashirika mbalimbali. Tuzungumzie hawa viongozi wa siasa. Unapotafuta nafasi ya uongozi kupitia siasa focus yako ni nini? What is your primary objective?

Viongozi wanapaswa kuumizwa na changamoto za wananchi ili kuwa sehemu ya kutafuta majawabu ya changamoto hizo. A leader must provide alternatives towards socio-economic and political catastrophe in his/her society. Lakini je ni viongozi wangapi wanaopigania nafasi za uongozi kwa sababu ya kuguswa na changamoto za jamii zao?

Lipo kundi linaloibuka kwa kasi ambalo ni viongozi maslahi. Hawa wapo kwenye vyama vyote (tawala na upinzani), rika zote na nchi zote (hasa kwenye nchi zetu za kiafrika).
Hawa wanapotafuta nafasi za uongozi huvaa ngozi bandia. Hujitambulisha kama watetezi wa wananchi lakini moyoni wana malengo yao.

Ndio maana unaweza kukuta mtu anaishi eneo lisilo na maji. Anapotafuta uongozi kilio chake kikubwa ni maji, lakini akipata uongozi anawaacha wananchi wake kwenye changamoto ileile ya maji, yeye anahamia eneo lenye maji. Na nguvu ya kudai maji inapungua kwa sababu yeye sio mhanga tena wa kukosa maji. Maslahi binafsi.

Wapo wabunge ambao walikuwa watumishi. Na walikuwa wakilia sana makato makubwa ya PAYE kwenye mishahara ya watumishi. Lakini walipopata ubunge kelele za PAYE zikakoma, simply kwa sababu mbunge hakatwi PAYE. As long as yeye sio victim tena wa PAYE basi kelele zinaisha. Hii ndio aina ya viongozi tulionao.

Wapo wanaopigania uongozi ili kulinda mali zao, kuongeza network ya biashara, kupata heshima ya madaraka, na wengine hutumia uongozi kama njia ya kutafuta fedha na kujilimbikizia mali. Viongozi wa aina hii wanapoona upande waliopo unawachelewesha kufikia malengo yao ni rahisi sana kuhamia upande mwingine.

Mhe.Lucy Magereli ametuambia kuwa ndugu Mwarwa Ryoba alianzisha kiwanda cha kusaga kokoto. Ni jambo jema. Lakini mradi huo ulikwamishwa na serikali ya CCM. Alifungiwa milango hata akiomba tender hapewi, na hivyo kujikuta anajiendesha kwa hasara.

Lakini sasa amehamia CCM. Ana uhakika kiwanda chake kitaanza kujiendesha kwa faida. Atapewa tender mbalimbali za kusupply kokoto kwenye miradi ya serikali hasa ya majengo na barabara. Hapo lengo lake litakuwa limetimia.

Kwahiyo inawezekana nia yake haikuwa kuhangaikia changamoto za maji, umeme, na barabara kwa watu wa Serengeti, bali kutumia ubunge kama ‘stepping stone’ ya kufanikisha malengo yake kibiashara kama hicho kiwanda cha kokoto na mengineyo.

Baadhi ya watu hawaoni uongozi kama fursa ya kuwatumikia wananchi, bali fursa ya kumaliza changamoto zao kiuchumi. Hapa ndipo unakuta mtu akikosa nafasi ya uongozi anajenga chuki au anahama chama. Hujawahi kuona watu walikuwa active sana kwenye siasa lakini baada ya kukatwa kwenye kura za maoni au kukosa ubunge/udiwani wakapoa kabisa au wakahamia vyama vingine?

Ndio maana napenda zaidi harakati kuliko vyeo vya kisiasa. Harakati ni endless, lakini vyeo vya kisiasa vina-fade pale unapokosa position. Kinachokufanya ufanye harakati ni changamoto za jamii, lakini mara nyingi kinachokufanya ufanye siasa ni kuwinda position.

Mwanasiasa bora ni yule ambaye ni mwanaharakati pia. Ambaye changamoto za jamii ndizo zinazompa msukumo wa kusonga mbele. Mtu wa aina hii awe na nafasi ya uongozi au asiwe nayo hawezi kuacha kupigania wengine. Political activists are the leaders without titles.

Mwaka 2014 nilishauriwa sana kugombea uongozi BAVICHA. Sikuwa tayari, lakini siakuacha harakati. Sikuwahi kupoa, sikuwahi kurudi nyuma kwa sababu sikutegemea title ili kufanya kazi. Kuna waliopewa "titles" lakini wakashindwa kuzitumia wakassurender.

Mwaka 2015 tuliji-organize vijana watatu kufanya ziara ya kuzunguka nchi nzima kuwanadi baadhi ya wagombea ubunge. Mimi, Dr.Chriss Cyrilo na Engineer Pamela Maassay. Hatukuwa na nafasi zozote za uongozi ndani ya chama. Tulitimiza wajibu wetu kama wanachama wa kawaida.

Kwa kutumia rasilimali zetu wenyewe tulizunguka mikoa 20 kwa muda wa zaidi ya miezi miwili kuwanadi wagombea ubunge, udiwani na mgombea Urais Mhe.Lowassa. Tulinunua bendera 200, tukaenda Ngome kuu ya chama wakatuongezea bendera 500, na mabango kadhaa. Tukaweka kwenye buti. Tukaanza safari.

Tulisafiri usiku na mchana kuvuka mabonde na milima. Kuanzia Ilala kwa Muslim Hassanali hadi Moshi Vijijini kwa Anthony Komu. Kuanzia Rombo kwa Joseph Selasini hadi Shinyanga kwa Patrobas Katambi. Kuanzia Bunda kwa Ester Matiko hadi Bahi kwa Mathias Lyamunda. Kuanzia Nyamagana kwa Ezekiah Wenje hadi Vwawa kwa Fanuel Mkisi.

Kuanzia Tarime Vijijini kule Sirari kwa John Heche hadi Kilolo kwa Brian Kikoti. Kuanzia Tarime mjini kwa Ester Matiko hadi Isimani kwa Patrick Sosopi. Kuanzia Siha kwa Godwin Molel hadi Urambo kwa Sam Ntakamulenga. Na mikoa mingine kama Njombe, Ruvuma, Tabora, Singida, Morogoro, Arusha etc.

Haikuwa kazi rahisi. Tulifanya kazi mchana na kusafiri usiku, kila siku kwa siku 60. Tulipokezana kuendesha gari. Ukichoka unampa mwingine wewe unapumzika. Ukiamka unanawa uso unarudi kwenye usukani. Mchana tupo jukwaani, usiku tupo barabarani. Hii 'spirit' sielewi ilitoka(ga) wapi. Nawauliza(ga) Cyrilo na Pamela tuliwezaje, hata wao hawajui. It was only by GOD.

Tulijikimu kwa kila kitu. Tulijua wagombea wetu wengi walikuwa na mahitaji mengi kuliko hali zao za kiuchumi. Kwahiyo hatukutaka kuwaongezea mzigo. Tulipofika tulihakikisha kuanzia malazi, chakula, service ya gari na mafuta ya gari ni jukumu letu.

Tuligawa bendera kila tulipopita, na baadhi ya majimbo tuliwassupport wagombea hela ya mafuta kwenye gari zao. Kazi ya mgombea ilikuwa ni moja tu. Kutukabidhi microphone na kutuonesha jukwaa lilipo. Ni jimbo moja tu ambako mgombea alikuwa ametufanyia booking hotelini na amelipia. Tulipofika akatuhamisha tuliposhuklia na kutupeleka alipokuwa amepaandaa.

Tuliyafanya yote hayo kwa moyo mweupe. Bila kulipwa, bila kutumwa wala kusukumwa. Nakumbuka tulipofika Mwanza rafiki yetu mmoja alikuja kutufuata pale Lakairo. Baada ya kubadilishana mawazo akatutania ‘tugawane basi hizo pesa za kampeni’. Tukamuuliza zipi? Akajibu 'hizo mlizopewa kuzunguka nchi nzima kumnadi Lowassa". Tukageukiana tukacheka. Hatukutaka kumwambia kwamba tumeji-finance wenyewe kwa sababu 'obvious' asingeamini.

Ni watu wachache sana wanaoweza kujitoa bila kutegemea ubunge, udiwani au nafasi yoyote ya uongozi. Sisi tulitimiza wajibu wetu kama wanachama wa kawaida wa Chadema na tulifurahia kufanya hivyo. Hatukuwa na fedha kuliko wengine, ni moyo tu wa kujitoa kwa ajili ya chama. Kuna wenye fedha nyingi lakini hawawezi kufanya tuliyofanya, kwa sababu hawana moyo huo.

Dada yangu Ester Bulaya aliniambia "Malisa nilikua sikufahamu, lakini kazi mliyoifanya Bunda siwezi kuisahau. Mmesafiri maelfu ya kilomita kuja kuniombea kura. Siku tatu mlizokaa Bunda ni za thamani sana. Mmenyeshewa hadi mvua mkiwa jukwaani kwa ajili yangu"

Mwaka 2015 niligombea Moshi vijijini kupitia kura za maoni. Lakini kura hazikutosha. Sikuvunjika moyo, sikurudi nyuma, sikuacha siasa. Nilienda Moshi kumnadi kaka yangu Anthony Komu aliyepewa ridhaa na chama. Nilizunguka nae maeneo mbalimbali kumuombea kura, akashinda.

Lakini leo utakuta mtu anapambana kumbe lengo lake ni kutaka ubunge, udiwani au nafasi fulani ya uongozi. Na akikosa anakuwa disappointed na huo ndio unakuwa mwisho wake katika siasa. Unajiuliza huyu mtu ni kweli alitaka changes, au alitaka kutimiza tu maslahi yake binafsi kupitia siasa? Jiulize wale "wanaharakati" wote waliokuwepo 2014/15 leo wako wapi? Watu wa aina hii hata wakipewa nafasi, ni rahisi kusaliti wananchi endapo wakiahidiwa maslahi makubwa zaidi.

Nadhani Upinzani tunahitaji kufanya vetting makini zaidi ya kuwapata viongozi wetu. Wapo wengi wanatumia upinzani kama kichaka cha kutimiza malengo yao binafsi. 2020 tutawaona watakavyopukutika.

Tunahitaji viongozi ambao Upinzani kwao ni falsafa, ni itikadi ni Imani. Wasioshawishika, wasiopoa, wasioyumba bila kujali changamoto wanazopitia.!

Malisa GJ
Hata upande mwingine, kwa nini tumbua tumbua sana?
 
Back
Top Bottom