Nadhani hatuna shida kubwa kwa kiwango cha kutangazwa kuwa Tanzania ina maambukizi makubwa sana ya corona

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,387
2,000
Hoja yangu ni hii kweli corona ipo na Rais amesema na amekiri.

Lakini kusema sisi ni nchi hatari si kweli maana hakuna anaweza kuficha vifo vya watu wote, tupo hapa tunatembea na tuna ndugu zetu na marafiki zetu lakini tatizo siyo kubwa kiasi hicho.

Pili gonjwa hili ni hatari kweli lakini kwa wenzetu wazungu ina maslahi mapana sana nyuma yake anayepambana kivyake anashambuliwa sana kuwa hafuati ushauri wa madaktari wa dunia. badala ya kushukuru huenda dawa itapatikana wanafanya mashambulizi kukatisha tamaa. Hapo ndipo mashaka yanapoanza

Tatu chanjo hii inalazimishwa sana kwa watu kwa sababu gani hasa afrika tangu wanzo lakini afrika kutumika kama gunia la mazoezi inajulikana kwa nini hatushtuki? Magu kwa hili nampongeza sana ingawa kuna baadhi ya move zake siikubali.

Nne baada ya kupewa chanjo unapewa elecronic certificate kwa sababu gani? Lazima mtu mwenye akili timamu ujiulize maswali mengi sana.

Mwisho ushauri wangu ni huu, tatizo hili kwa Tanzania siyo kubwa kwa kiwango cha kutangazwa kuwa nchi hatari kwa kuwa vifo havifichiki ndugu zangu kila moja angekiri kweli kuna tatizo.

Lakini mimi nataka kusema hivi tunatakiwa kukataa chanjo zote na wala siyo ya corona tu maana huwezzi kusema ndizi ya huyu bwana huyu sili kwa sababu ina sumu lakini akakupa wali wa mtu yule yule ukala umeepuka nini hapo? Hakuna.

Chanjo ya surua, pepopunda, nakadhalika ipigwe marufuku pia mimi naweza sema hizo chanjo ni moja ya watoto wetu kuwa na uwezo mdogo sana katika sayansi na hesabu huku ashuleni hali ni mbaya sana

Ni maoni yangu ruksa kukosolewa kwa lugha zote
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
21,941
2,000
Tunatakiwa tuchukue TAHADHARI dhidi ya ugonjwa wa CORONA.

Na viongozi wetu wasimung'unye maneno ktk kuwahimiza wananchi kuchukua tahadhari.

Rais, mawaziri na viongozi wengine wasisitize wananchi kuvaa barakoa, kunawa mikono, kujifukiza, na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.
 

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,387
2,000
Tunatakiwa tuchukue TAHADHARI dhidi ya ugonjwa wa CORONA.

Na viongozi wetu wasimung'unye maneno ktk kuwahimiza wananchi kuchukua tahadhari.

Raisi, mawaziri, na viongozi wengine wasisitize wananchi kuvaa barakoa, kunawa mikono, kujifukiza, na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.
Corona ina uhusiano mkubwa sana na hofu, ukiwa na hofu hata mafua ya kawaida inakufanya usononeke mpaka kukosa nguvu.

Nadhani mnajua mfadhaiko au msongo wa mawazo unavyokuwa na athari this thing is well studied and experimented make my words ukiweza kuondoa hofu tu ndo ushindi kwa taarifa yako
 

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
2,444
2,000
Hoja yangu ni hii kweli corona ipo na rais amesema na amekiri...
Hivi mna hata teknolojia ya juuda wembe?

Nchi kama China au Japan au India wale wana uwezo wa kupinga Chanjo za Wazungu make kwa sayansi wako mbele sana, India inazalisha madawa kibao ya binadamu.

Nyie ni kipi mnazalisha? Madawa yote ni ya nje,

Hao wazungu wanashindwa kudili na sisi kupitia vyakula? Ngano asilimia 90 tunaagiza kwao,

Tuanze hata kuunda wembe then tupate nguvu ya kuhoji
 

Immanuel Simon Mathew

JF-Expert Member
Apr 2, 2020
380
1,000
Wakati mwingine unakuta matatizo tuliyonayo ni madogo in such a way yanaweza kutatuliwa haraka na kirahisi kabisa yakatoweka. Lakini kwakuwa tupo chini ya miliki ya Malaika tunaanza kujiaminisha kuwa changamoto zetu hazipo na kuanza kushi maisha ya assumption matokeo yake shida ikishakuwa kubwa ndiyo tunazinduka usingizini very late
 

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,387
2,000
Hivi mna hata techinolojia ya juuda wembe?

Nchi kama China au Japan au India wale wana uwezo wa kupinga Chanjo za Wazungu make kwa sayansi wako mbele sana, India inazalisha madawa kibao ya binadamu...
Tunaweza kuwa maskini lakini siyo umaskini wa kufikiri kwa kuwa hatuna uwezo wa kutengeneza wembe ukubali tu kila kitu hata kama umeona ina matatizo?

Kutengeneza ni uamuzi tu hatukutaka kama nchi
 

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
3,665
2,000
Hoja yangu ni hii kweli corona ipo na rais amesema na amekiri...
Si rahisi kujua ukubwa wa tatizo mpaka uwe karibu na watu wa hospitali.

La pili mwaka jana serikali ilkuwa ikizika wanaokufa na ukubwa ulikuwa unaonekana, kwa sasa kila mtu anazika mtu wake kwao au popote,si rahisi ukubwa wa tatizo kuonekana.
 

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,387
2,000
Mimi nadhani maamuzi yetu kama nchi na vipaumbele vyetu ndio yanayoturudisha nyuma
 

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,387
2,000
Si rahisi kujua ukubwa wa tatizo mpaka uwe karibu na watu wa hospitali.
La pili mwaka jana serikali ilkuwa ikizika wanaokufa na ukubwa ulikuwa unaonekana,kwa sasa kila mtu anazika mtu wake kwao au popote,si rahisi ukubwa wa tatizo kuonekana.
Hivi hili la sisi kutangazwa dunia nzima kuwa Tanzania ni nchi hatari ni kweli kwa maoni yako mkuu?
 

Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
2,371
2,000
Hoja yangu ni hii kweli corona ipo na rais amesema na amekiri...
Naikataa hoja yako, kwanini tulikataa tatizo hili halipo, hatutaki hata kuwaelimisha watu wachukue tahadhari. Tumekataa kutoa takwimu muda mrefu, kinyume na mikataba ya kimataifa tuliyoingia. Lete hoja kinzani tusonge mbele.
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
21,941
2,000
corona ina uhusiano mkubwa sana na hofu ukiwa na hofu hata mafua ya kawaida inakufanya usononeke mpaka kukosa nguvu

nadhani mnajua mfadhaiko au msongo wa mawazo unavyokuwa na athari this thing is well studied and epxerimented make my words ukiweza kuondoa hofu tu ndo ushindi kwa taarifa yako

Miimi sisemi tuwe na hofu.

Nasema tuwe waangalifu; tuchukue tahadhari.

Uzembe, kubweteka, na kutokuchukua tahadhari ya magonjwa, ni chanzo cha vifo na majanga.

Viongozi wetu wasiwadanganye wananchi na kusababisha wasichukue tahadhari dhidi ya covid-19.
 

ofisa

JF-Expert Member
May 15, 2011
2,779
2,000
Wale wa jicho la tatu wanaona ni maandalizi matumizi ya namba.

Ulimwengu wote lazima ukubali sasa wazungu lazima watumie nguvu kubwa kulazimisha hili.

Na JPM anaelewa kuwa unavyokuwa mgumu ndivyo dau lako linavyopanda so wazungu watakuja na dau la kumshawishi JPM akubali.
 

john issa

JF-Expert Member
Mar 21, 2017
275
250
Binafsi nahisi issue ya COVID-19 kuna watu wanataka kugeuza opportunity kiuchumi
 

Mvumbo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
2,052
2,000
'
JamiiForums329407765.jpg
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
4,375
2,000
Ni pale mtakapogundua when it comes to binadamu na mazingira (death and survival) hakuna sisi na wao... , tunahangaika kutafuta mchawi badala ya kupambana na kusaidiana kutatua matatizo

Binadamu na Magonjwa ni vita ambavyo havitakwisha kila siku vijidudu vina-adapt na sisi inabidi kupambana, Corona sio mwisho yatakuja na mengine (swali ni je tumejitayarisha)? Pamoja na kuambukiza sana Corona Mortarity rate yake ni ndogo, pale ambapo litakuja gonjwa la kuambukiza na kuua kwa kasi huenda binadamu as a specie akatoweka iwapo tutaendelea na huu ulimbukeni
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom