Nadhan hili la korosho limetupa funzo kubwa mno sidhan kama litajirudia tena

Hili zao lishatiwa gundu, itachukua miaka mingi mpaka lirudi kwenye hali ya kawaida. Pesa za kugharamia process yote ya kuhudumia zao, pembejeo, uvunaji, usafiri nk zote zimekwenda na maji.
 
ingependeza kauli hiyo aitoe rais mwenyeweeeeeeeee na si waziri
Awamu hii kazi ya Rais ni .........na ya waziri ni......... 👇👇👇
tapatalk_1543132807768.jpeg
 
Kwa mkulima asiye na dhamana...... Kangomba hakwepek. Na kangomba ni risk takers wanaweza kutoa hela yao kununa hata korosho kabla haijawa hata kwenye mti!, Ila wana matumaini.
 
Ukweli inasikitisha na haswa nawaonea huruma sana wakulima na wafanya biashara ndio walioumia sana katika siasa hizi. Serikali wala sio aibu kusema katika sera hizi wamekosea na waombe msamaha ili yasijirudie tena. kazi kubwa ya serikali kuwatafutia soko wakulima wake wa mazao yote ili hawa wakulima na wafanya biashara wa katikati wafaidike maana hakuna biashara duniani mkulima akafanya direct na mnunuzi wa nje siku zote wako wafanya biashara wa ndani wananunua wanauza wote wanapata faida. Mimi naweza kusema Rais alikosea ila kama kuna watu walimshauri awafukuze haraka hao sio watu wakweli njaa tu. Rafiki wa kweli anakwambia kweli maoni yake na waziri au mwana siasa wa kweli ana maoni yake na akiona serikali inafanya sivyo anavyoamini yeye anakaa pembeni lakini hawa wanasiasa wetu ni kama simu za kichina sim card 4 hujui yuko mtandao gani.
 
Back
Top Bottom