Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 3,832
- 2,790
Haki ya Mungu sasa ninapenda kufanya hivyo. Kauli za viongozi wetu pindi yanapotokea mauaji yanayofanywa na Polisi kwa raia yananisukuma kufanya hivyo. Siyo hivyo tu bali pia matumizi ya kidhalimu ya vyombo vya usalama kwa raia, vinanisukuma kufanya hivyo.
Usalama wa Taifa:
Hapo awali hawa watu walikuwa waadilifu sana leo hii utadhani hawapo, mauaji kila mara, ugaidi utadhani Tanzania ni uwanja wao wa mazoezi. Hapo awali hatukuwafahamu usalama wa Taifa leo wanajitambulisha utadhani ni mesenjas katika makampuni. Ndiyo hao hao wanatumika kuficha maovu ya watendaji waandamizi. Kama wasingekuwa ni sehemu ya ubadhirifu huo EPA isingeibuka na kashfa ya wizi wa pesa zake.
Jeshi la Polisi:
Ninyi kila kukicha mnaibuka na kila aina ya kashfa, dhuluma, mauaji ya raia wasio na hatia na wenye hatia, matumizi ya nguvu dhidi ya raia kama vile Mauaji ya waandishi wa habari, mauaji ya raia kama vile wale wafanyabiashara wanne wa Mahenge, mauaji ya watoto sehemu mbali mbali za nchi, ubakaji huko Mtwara wakati wa kutuliza vurugu za gesi, uporaji, ujambazi na mengine mengi.
Ningeweka data hapa naona nitawachosha wasomaji wangu kwa mada ndefu.
Hakika tumechoka na hali hii, natamani kuishitaki Serikali katika Mahakama ya Haki za Binadamu.