Nadhamiria Kuishitaki Serikali ya Tanzania Mahakama ya Haki za Binadamu

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,832
2,790
Haki ya Mungu sasa ninapenda kufanya hivyo. Kauli za viongozi wetu pindi yanapotokea mauaji yanayofanywa na Polisi kwa raia yananisukuma kufanya hivyo. Siyo hivyo tu bali pia matumizi ya kidhalimu ya vyombo vya usalama kwa raia, vinanisukuma kufanya hivyo.

Usalama wa Taifa:
Hapo awali hawa watu walikuwa waadilifu sana leo hii utadhani hawapo, mauaji kila mara, ugaidi utadhani Tanzania ni uwanja wao wa mazoezi. Hapo awali hatukuwafahamu usalama wa Taifa leo wanajitambulisha utadhani ni mesenjas katika makampuni. Ndiyo hao hao wanatumika kuficha maovu ya watendaji waandamizi. Kama wasingekuwa ni sehemu ya ubadhirifu huo EPA isingeibuka na kashfa ya wizi wa pesa zake.

Jeshi la Polisi:
Ninyi kila kukicha mnaibuka na kila aina ya kashfa, dhuluma, mauaji ya raia wasio na hatia na wenye hatia, matumizi ya nguvu dhidi ya raia kama vile Mauaji ya waandishi wa habari, mauaji ya raia kama vile wale wafanyabiashara wanne wa Mahenge, mauaji ya watoto sehemu mbali mbali za nchi, ubakaji huko Mtwara wakati wa kutuliza vurugu za gesi, uporaji, ujambazi na mengine mengi.

Ningeweka data hapa naona nitawachosha wasomaji wangu kwa mada ndefu.

Hakika tumechoka na hali hii, natamani kuishitaki Serikali katika Mahakama ya Haki za Binadamu.
 
Mimi nashindwa kuelewa hivi serikali mpaka iue watu wangapi ndo inapelekwa ICC?maana nijuavyo na nionavyo kama serikali hii ya Ccm haipo ICC mpaka sasa manaake haina makosa!na kama kwa haya yanayoendelea inaonekana kwamba haina makosa hao waliopo huko walikosa nini kikubwa kuliko kinachofanywa na hawa Ccm na Polisi?Nionavyo mimi Rais aende akajibu mashtaka The Hague,Mwema akajibu Mashtaka The Hague,Chagonja akajibu mashtaka the Hague,Kamuhanda akajibu mashtaka The Hague,Mwigulu akafungwe The Hague,Nape akafungwe The Hague Ccm ipigwe marufuku ulimwenguni ili viongozi wake wakajibu tuhuma za mauaji mbele ya mahakama za Kimataifa..
 
kwa taarifa yako huyu mtu unayesema au ambao chadema wanadai ameua arusha inasemekana chadema wanamfaha vema.

taarifa zaidi zinasema kuwa huyo jamaa alivalishwa nguo ya polisi ili kulichafua jeshi la polisi.
 
Kwa nini Polisi walimbeba kwenye gari lao na kumtorosha? Hata kama ni kweli ulinz na usalama wa nch uko wapi mpaka watu binafsi wanafanya hivyo? Unadhan we uko salama?
 
kwa taarifa yako huyu mtu unayesema au ambao chadema wanadai ameua arusha inasemekana chadema wanamfaha vema.

taarifa zaidi zinasema kuwa huyo jamaa alivalishwa nguo ya polisi ili kulichafua jeshi la polisi.
Sikiliza NP, njia ya mwongo daima ni fupi sana.
Sawa tufanye CHADEMA wanamfahamu.....
1) Je ndio waliompa mrushaji bomu husika?
2) Je ndio walioandaa mtumia SMG na Sniper man?
3) Je ndio waliomsadia kumtorosha/kumnusuru kutumia L/Cruiser ya rangi buluu?
4) Kwa nini wafanye hayo? Why?
 
Haki ya Mungu sasa ninapenda kufanya hivyo. Kauli za viongozi wetu pindi yanapotokea mauaji yanayofanywa na Polisi kwa raia yananisukuma kufanya hivyo. Siyo hivyo tu bali pia matumizi ya kidhalimu ya vyombo vya usalama kwa raia, vinanisukuma kufanya hivyo.

Usalama wa Taifa:
Hapo awali hawa watu walikuwa waadilifu sana leo hii utadhani hawapo, mauaji kila mara, ugaidi utadhani Tanzania ni uwanja wao wa mazoezi. Hapo awali hatukuwafahamu usalama wa Taifa leo wanajitambulisha utadhani ni mesenjas katika makampuni. Ndiyo hao hao wanatumika kuficha maovu ya watendaji waandamizi. Kama wasingekuwa ni sehemu ya ubadhirifu huo EPA isingeibuka na kashfa ya wizi wa pesa zake.

Jeshi la Polisi:
Ninyi kila kukicha mnaibuka na kila aina ya kashfa, dhuluma, mauaji ya raia wasio na hatia na wenye hatia, matumizi ya nguvu dhidi ya raia kama vile Mauaji ya waandishi wa habari, mauaji ya raia kama vile wale wafanyabiashara wanne wa Mahenge, mauaji ya watoto sehemu mbali mbali za nchi, ubakaji huko Mtwara wakati wa kutuliza vurugu za gesi, uporaji, ujambazi na mengine mengi.

Ningeweka data hapa naona nitawachosha wasomaji wangu kwa mada ndefu.

Hakika tumechoka na hali hii, natamani kuishitaki Serikali katika Mahakama ya Haki za Binadamu.
Mkuu, hiyo mahakama iko wapi? Mie najitolea kuwa wakili wa kuitetea serikali.mna hukumu ikotolewa ambapo nina hakika serikali itashinda, nitaiamuru mahakama hiyo iiamuru serikali kukaza uzi dhidi ya wale wote wanaocuruga amani ya nchi hii
 
kwa taarifa yako huyu mtu unayesema au ambao chadema wanadai ameua arusha inasemekana chadema wanamfaha vema.

taarifa zaidi zinasema kuwa huyo jamaa alivalishwa nguo ya polisi ili kulichafua jeshi la polisi.

Hiyo taarifa ya kulichafua jeshi la polisi ambalo tunajua ni chafu kwa siku sasa inatoka wapi. Mtu mwenye akili timamu hawezi kuhangaika na jeshi la polisi la hapa Tanzania ambalo viongozi wake wamebaki kuvimbiana matumbo na kusubiri maagizo na maelekezo kutoka kwa watawala na ccm badala ya kutimiza wajibu wake kama inavyotakiwa.

Kimsingi jeshi la polisi limegeuzwa kuwa idara ya ccm na kikundi cha kulinda masilahi ya watawala na sio kwa ajili ya ulinzi wa raia kama wanavyodai.
 
kwa taarifa yako huyu mtu unayesema au ambao chadema wanadai ameua arusha inasemekana chadema wanamfaha vema.

taarifa zaidi zinasema kuwa huyo jamaa alivalishwa nguo ya polisi ili kulichafua jeshi la polisi.

Hivi nguruwe anayetoka kwenye tope la kinyesi ukimwagia kinyesi unamchafua???
 
kwa taarifa yako huyu mtu unayesema au ambao chadema wanadai ameua arusha inasemekana chadema wanamfaha vema.

taarifa zaidi zinasema kuwa huyo jamaa alivalishwa nguo ya polisi ili kulichafua jeshi la polisi.

mmeanza kubabaika,kwani polisi imekuwa ccm chadema wapambane nao.Inaonesha wazi kuwa mmewekeza ktk kichaka cha polisi ndo maana unaongea as if polisi ni chama cha Siasa.safari hizi magamba hamna pa kutokea.
 
Haki ya Mungu sasa ninapenda kufanya hivyo. Kauli za viongozi wetu pindi yanapotokea mauaji yanayofanywa na Polisi kwa raia yananisukuma kufanya hivyo. Siyo hivyo tu bali pia matumizi ya kidhalimu ya vyombo vya usalama kwa raia, vinanisukuma kufanya hivyo.

Usalama wa Taifa:
Hapo awali hawa watu walikuwa waadilifu sana leo hii utadhani hawapo, mauaji kila mara, ugaidi utadhani Tanzania ni uwanja wao wa mazoezi. Hapo awali hatukuwafahamu usalama wa Taifa leo wanajitambulisha utadhani ni mesenjas katika makampuni. Ndiyo hao hao wanatumika kuficha maovu ya watendaji waandamizi.
Kama wasingekuwa ni sehemu ya ubadhirifu huo EPA isingeibuka na kashfa ya wizi wa pesa zake.

Jeshi la Polisi:
Ninyi kila kukicha mnaibuka na kila aina ya kashfa, dhuluma, mauaji ya raia wasio na hatia na wenye hatia, matumizi ya nguvu dhidi ya raia kama vile Mauaji ya waandishi wa habari, mauaji ya raia kama vile wale wafanyabiashara wanne wa Mahenge, mauaji ya watoto sehemu mbali mbali za nchi, ubakaji huko Mtwara wakati wa kutuliza vurugu za gesi, uporaji, ujambazi na mengine mengi.

Ningeweka data hapa naona nitawachosha wasomaji wangu kwa mada ndefu.

Hakika tumechoka na hali hii, natamani kuishitaki Serikali katika Mahakama ya Haki za Binadamu.

hapo kwenye nyeusi hivi kumbe hujui kuwa miongoni mwa suspect ni kigogo wa maspy tz kwamba naye alikuwa na fungu lake mambo yanavyoenda nchi hii , uonevu , ukosefu wa ajira , ufisadi na wizi mi nakwambia sasa hakuna anayejari ....inafika mahari sitaki hata kuwa na mtoto manake naogopa kwa maisha gani nizae mtoto tz...huku nikumtafutia matatizo ila madam tegemeo la wengi (CDM) wapo basi tunamshukuru mungu na ndio maana ktk kila sala yangu naimbea cdm
 
kwa taarifa yako huyu mtu unayesema au ambao chadema wanadai ameua arusha inasemekana chadema wanamfaha vema.

taarifa zaidi zinasema kuwa huyo jamaa alivalishwa nguo ya polisi ili kulichafua jeshi la polisi.

Huna akili kweli!

Na kama kazi ya Polisi ni kulinda Usalama wa Raia, na wanafahamiana kikazi na kitaaluma, inakuwaje mtu mwingine avalishwe sare zao na kufanya mauaji mchana kweupe na wasione? Basi waache kazi maana wameshindwa! tutumie mgambo wanaotumia Virungu na Si wao wanaolipua raia wasio na hatia na kuacha wenye hatia!

Kwanza kisheria hauruhusiwi kutumia silaha za kivita kuwatawanyisha wananchi wasio na hatia! Nashangaa polisi wanatumia,na bado wale wasio na hatia ndo wanapelekwa Mahakamani?
Hizi Mahakama zinalinda haki ya watu au zinatupilia mbali?
GOD FORBID!
 
kwa taarifa yako huyu
mtu unayesema au ambao chadema wanadai ameua arusha inasemekana chadema
wanamfaha vema.

taarifa zaidi zinasema kuwa huyo jamaa alivalishwa nguo ya polisi ili
kulichafua jeshi la polisi.

Peleka uliberali wako kwa mumeo mwigulu.
 
Sielewe kwa nini hadi sasa Serikali hii dhalimu ya ccm na mawakala wao bado hawajafikishwa mahakamani THE HAGUE??? Au UN iko kwa ajili ya wazungu tu, au hadi maslahi ya nchi za magharibi yavurugwe ndio THE HAGUE inaoneka??
 
kwa taarifa yako huyu mtu unayesema au ambao chadema wanadai ameua arusha inasemekana chadema wanamfaha vema.

taarifa zaidi zinasema kuwa huyo jamaa alivalishwa nguo ya polisi ili kulichafua jeshi la polisi.

Karibu jamvini kamanda wa operesheni,bila shaka umejiunga kwa ajili ya propaganda!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom