NACTE, Vigezo vya kujiunga na Uuguzi ngazi ya cheti(Certificate in nursing) muliangaliwe upya

MRI

JF-Expert Member
Nov 25, 2016
334
428
Hapo awali vigezo vya kujiunga na uuguzi ngazi ya cheti lilikuwa linafanana na kozi nyingine za afya kama maabara,Utabibu,ufamasia,Miozi,n.k ni vigezo ilikuwa ni ufaulu wa alama D katika masomo ya Physics,chemistry na Biology kwa kidato cha nne!.Sasa hivi kujiunga na certificate in nursing lazima uwe na DCC kwenye Physics,chemistry na Biology,vigezo hivi ni sawa na vigezo vya kujiunga diploma in nursing ambavyo navyo DCC (PCB) .Lakini pia vigezo hivi nitofauti kabisa na certifacates za kozi nyingine ambazo zenyewe zimebaki kuwa ni ufaulu wa DDD kwenye PCB

-Swali,NACTE mnamanisha nini vigezo vya ngazi ya cheti kufanana na vigezo vya diploma in nursing,.

-Kuna kitu gani cha ziada vigezo vya kujiunga uuguzi ngazi ya cheti kutofautina na cheti katika utabibu(Certificate in clinical Assistance),Maabara(Certificate in Medical laboratory technician,) Ufamasia(Cerficate in pharmacetical technician)
 
Mkuu hata mimi nimeshangaa kuona vigezo vya cheti na diploma ya nursing vinafanana!!!! Hapa kuna kitu hakijaenda sawa
 
Nacte kuna kitu hakiko sawa,kama wangeongeza vigezo walau wangesema C na DD mbili kwenye PCB
 
Hawajielewi ndo maana mkulu ameanza kuwaondoa taratibu mwisho wa siku wataunganishwa na kitu kingine kama ilivyotokea kwa CDA
 
Kwenye sekta ya Afya tunadeal Na maisha ya watu inahitajika watu bright Uuguzi ni dhamana ya maisha ya watu

Haijalishi kwamba wewe Ni muuguzi wa certificate Au diploma wote mnahudumia Wagonjwa Hivo ufaulu Lazima uwe wa juu

Fani zingine ni rahisi kutofautisha majukumu ya certificate Au diploma holder ila kwa wauguzi Ni vigumu
In fact elimu yao ni MOJA utofauti mdogo sana

Likewise madaktari clinical officers assistant medical officers Na medical officers Lazima ufaulu uwe Mzuri utofauti Wetu ni mdogo Wagonjwa ni walewale
 
Hata waliomba mwaka huu intake ya mwezi March na April ilikuwa vigezo hivyo hivyo
 
mlipokuwa shule mkishauriwa kusoma kwa bidii mnakuwa wajuaji na kutaka kujilinganisha na walimu wenu.

naomba nacte muongeze iwe CCC na lazima wawe na pass za math na English. chagua wenye division three pekee.

hatutaki four kabisa zikidahiliwa kwenye ualimu, unesi na uganga.

four pelekeni kuristi
 
Kwenye sekta ya Afya tunadeal Na maisha ya watu inahitajika watu bright Uuguzi ni dhamana ya maisha ya watu

Haijalishi kwamba wewe Ni muuguzi wa certificate Au diploma wote mnahudumia Wagonjwa Hivo ufaulu Lazima uwe wa juu

Fani zingine ni rahisi kutofautisha majukumu ya certificate Au diploma holder ila kwa wauguzi Ni vigumu
In fact elimu yao ni MOJA utofauti mdogo sana

Likewise madaktari clinical officers assistant medical officers Na medical officers Lazima ufaulu uwe Mzuri utofauti Wetu ni mdogo Wagonjwa ni walewale
Safi nmeipenda sana hii,,, atlist itapandsha hadhi ya uuguzi…!!
 
hii ni zaidi hata ya Clinic afficer, wadogo zetu sijui wataenda wapi.
Mkuu hapo ndiyo huwa tunakosea kufananisha Nursing na medicine including clinical officers,, kifupi ni kuwa wote hawa wanahudumia wagonjwa ili wapate kupona so kikubwa wote inabdi wawe na value moja na sio mmoja kuonkan bora halafu mwingine anaonkana ni mfata maelekezo kutoka kwa mwingine ilihali wote wana level moja ya elimu,,,,

Kwa maono yangu,, nadhani NACTE wameliona hilo,, so ili kuipandsha hadhi ya nursing na ili izidi kuheshimika ni bora waongeze vigezo.

kwann nasema hadhi ya nursing ilikua imeshuka, hii ni kutokana na waliokua wanaingia nursing enzi hizo ni wale waliokua wamekosa vigezo vya kusoma kitu chchote so wakaona ni bora tu waende nursing coz yenyew haina vigezo vingi.

Hii unaweza hata kuiona kupitia vyeti feki pale muhimbili, wengi waliokutwa na vyeti feki ni manesi,, so utaona ni kiasi gani nursing ilionkana kama ni chimbo la,wasiojua…!

So mim nachokiona hapo tuwasapoti tu NACTE kwa maamuzi hayo,, ila pia tuwajengee watoto wetu Moyo wa kuipenda nursing tangu wako shuleni, hivo wasome kwa bidii ili kupata ufaulu mzuri, kama ilivo kwa walio na ndoto za kuwa madaktari siku za usoni…!!
 
Hivi Kwa vigezo hivi PCB=DDD na Eng-D,Kiswahili-D na F-Maths napata Technician certificate clinical medicine (2yrs)?
 
Wenye vyetii vya wasiwasi waliounga unga utawajua tuu mh raisi alisema kama hufai sehemu husika nenda unapofiti nendeni community health mbona watawachukua kwa DDD zenu hizoo weak.?.
 
mlipokuwa shule mkishauriwa kusoma kwa bidii mnakuwa wajuaji na kutaka kujilinganisha na walimu wenu.

naomba nacte muongeze iwe CCC na lazima wawe na pass za math na English. chagua wenye division three pekee.

hatutaki four kabisa zikidahiliwa kwenye ualimu, unesi na uganga.

four pelekeni kuristi
Hahahaha ikiwezekana wawekee BBB mwisho hahah we jamaa sio mtu mzuri wakiambiwa wasomee....?
 
Back
Top Bottom