NACTE, TCU, Waziri wa elimu tupeni ufafanuzi uhuni na ulaghai unaofanywa na chuo cha Ustawi wa Jamii

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
11,321
17,817
Habari wana JF,

Niende moja kwa moja kwenye mada husika.

Kuna taarifa za ajabu na kusikitisha kuwahusu vijana wetu waliomba na kuchaguliwa kusoma kozi ya CERTIFICATE IN SOCIAL WORK.

Wanafunzi walipoenda kuomba kujiunga na chuo na hata walipofanikiwa kupata udahili barua ilionesha kozi yao ni ya mwaka mmoja iliambatanishwa na gharama zote za kozi husika kwa mwaka mmoja.

Katika hali ya kushangaza ijumaa ya tarehe 11 mwezi wa Novemba (11/11/2017) vijana wetu wamepewa taarifa kozi yao itakuwa ya miaka miwili tofauti na barua yao ya udahili ilivyoeleza na pia tofauti na taarifa tulizopewa wazazi/walezi/wadhamini wa wanafunzi wakati wanaomba kupata taarifa za kujiunga na chuo. TAARIFA HII IMEKUJA ZAIDI YA MAJUMA MAWILI BAADA YA KUANZA MASOMO!

Jambo hili limeleta taharuki kubwa sababu taarifa imetolewa tayari tukiwa tumeshalipia karo/ada ya masomo na gharama zingine.

Pia muda wa kukamilisha usajiri/udahili wa vyuo vingine ukiwa umepita hivyo kusababisha vijana wakose nafasi ya kujiunga vyuo vingine. Jambo hili ni kinyume kabisa na haki za msingi za mlaji au consumer(kwa hapa ni mwanafunzi)

Sasa tunauliza huu sio utapeli unaofanywa na taasisi kubwa kabisa ya umma? Kwanini tusirudishiwe fedha zetu na fidia juu ya kupotezewa muda tupate hiyo fedha watoto wetu wakasome hata nje ya nchi?

Kwanini NACTE na chuo husika hamkutoa taarifa mapema ili mwanafunzi afanye chaguo akasome kozi gani nyingine ambayo ataziweza gharama zake na muda utakuwa mwaka mmoja? Taasisi kubwa ya umma kama hiki chuo kinakosaje utaratibu wa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati?

Tatizo kubwa zaidi ni ongezeko la gharama kwa huo mwaka mmoja ulio ongezwa. Kumbukeni sio wanafunzi wote wana uwezo wa kumudu hizo gharama.
Kuna wengine wamepewa msaada na watu au taasisi tofauti ambao sio wazazi wao hivyo waliojitolea kuwasaidia waliomba kujua gharama husika kabla na huu ndio msingi wa zile prospectus, brochure, na baraua wakati wa kupewa taarifa za udahili aliopewa mwanafunzi. Kwanini hizi taratibu zimepuuzwa?

Tunachotaka kujua kwa wale wasiokuwa tayari kuendelea na kozi hii ya miaka miwili watarudishiwa fedha zao wakasomee hata kozi ya kazi za hoteli na utalii muda mfupi wakajiajiri. Au turudishiwe haraka pesa tukajaribu vyuo vingine kozi zingine hata nchi jirani. Je serikali itaingilia kati na kuwapa nafasi wakafanye usajili vyuo vingine ambavyo pia walipata udahili?

Wataalamu wa sheria tunaomba msaada wenu wa ushauri juu ya jambo hili la kihuni.

Mimi nimeguswa na hili jambo kwa sababu ni kati ya watu ninafadhili mwanafunzi mmoja ambae mimi sitakuwa na uwezo wa kumlipia huo mwaka wa ziada, na wazazi wa mwanafunzi wana hali mbaya sana kiasi cha kukosa hata pesa ya matibabu na chakula.

Uzembe mkubwa zaidi tunaambiwa taarifa hizi wanafunzi wamepewa na uongozi wa wanafunzi na wahanga walikaa kikao na hao wanafunzi wenzao waitwao rais wa ungozi wa wanafunzi wa chuo, taarifa kama hizi ilibidi wapewe na uongozi wa chuo sio wa wanafunzi pamoja na idara husika. Cha kushangaza zaidi wameambiwa wamsubiri mkuu wa idara kujua hatima yao, hivi hawa watu wapo makini na kazi yao?

Hii ndio Tanzania anayoitaka Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli?

NB: KAMA TAARIFA HIZI NILIZOPEWA MLEZI AU MDHAMINI SIO SAHIHI TUNAOMBA TAARIFA SAHIHI TOKA UONGOZI WA CHUO, WIZARA NA NACTE.
 
certificate unaisoma 2 years.. je diploma utaisoma miaka mingapi?? na je degree??
 
certificate unaisoma 2 years.. je diploma utaisoma miaka mingapi?? na je degree??
Wanasema diploma watasoma mwaka mmoja. Hii kitu ni vurugu sana. Baadae kuna baadhi ya taasisi watazikataa hizo diploma za mwaka mmoja. Hasa ukijaribu kuomba kufanya kazi au kusoma nje ya nchi.
 
Wamezingua kinoma yaani, halafu sio social work peke yake ila certificate kozi zote pale ustawi ni miaka miwili
 
Kozi waliyo omba kusoma na kuchaguliwa sio kozi wanayolazimishwa kusoma sasa kwa maana ya kuna tofauti ya muda na gharama, tofauti na barua na maelezo ya chuo kabla ya usajili na wakati wanasajili hawakupewa taarifa hizi tata.
 
Wamezingua kinoma yaani, halafu sio social work peke yake ila certificate kozi zote pale ustawi ni miaka miwili
Wangetoa taarifa mapema kabla watu hawajafanya usajili na kulipa pesa. Vijana wengine walipata kozi zingine vyuo vingine wangeenda huko lakini sasa udahili na usajili umeshapita na fedha zao zimeshachukuliwa huu ni utapeli na wizi waziwazi. Wadau wakijiunga pammoja watashinda kesi mahakamni kudai fidia au kurejeshewa fedha zao au kurudisha muda walioambiwa wakati wanaomba na kusajiliwa.
 
Wangetoa taarifa mapema kabla watu hawajafanya usajili na kulipa pesa. Vijana wengine walipata kozi zingine vyuo vingine wangeenda huko lakini sasa udahili na usajili umeshapita na fedha zao zimeshachukuliwa huu ni utapeli na wizi waziwazi. Wadau wakijiunga pammoja watashinda kesi mahakamni kudai fidia au kurejeshewa fedha zao au kurudisha muda walioambiwa wakati wanaomba na kusajiliwa.
Yaani kama watu wakienda mahakamani mie nitaungana nao
 
Fikiria kama mwanafunzi ni mwajiriwa wa taasisi fulani ambae aliomba ruhusa ya masomo mwaka mmoja.
sasa atamweleza nini mwajiri wake huo mwaka wa ziada wakati tayari alishaomba ruhusa ya mwaka mmoja kwa maandishi?
Au aliomba likizo bila malipo ya mwaka mmoja sasa inabidi aache kazi au afanyeje? Au ataishije huo mwaka wa ziada bila malipo kama mwanzo alitafuta pesa ya kujikimu kimaisha na kulipia masomo kwa mwaka mmoja tu?
 
Yaani kama watu wakienda mahakamani mie nitaungana nao
Jikusanyeni vijana muombe ushauri hapa na wazazi na walezi mfungue hili shauri la madai mahakamani haraka sana kama hamtasikilizwa.
 
Jikusanyeni vijana muombe ushauri hapa na wazazi na walezi mfungue hili shauri la madai mahakamani haraka sana kama hamtasikilizwa.
Watanzania wengi waoga mkuu naweza nikawa nipo peke yangu kwa hili jambo maana wengine naona kama wameridhika vile
 
Watanzania wengi waoga mkuu naweza nikawa nipo peke yangu kwa hili jambo maana wengine naona kama wameridhika vile
Je mmefanya mawasiliano na ofisi ya taaluma au mkuu wa chuo kuhusu hili jamabo?
 
Back
Top Bottom