NACTE NA NECTA nani mwenye mamlaka ya kucompute/ kupanga GPA ya Walimu wa Diploma ambao vyeti vyao havina GPA hasa 2015?

Tsakhodegha

Member
Mar 16, 2013
27
45
Mke Wangu Amegraduate Chuo Cha Ualimu Tukuyu Diploma Yake Mwaka 2015 na Kupata GPA ya 3.0 kwa Mujibu wa Matokeo ya NECTA.

Mwaka 2017 Akataka Kujiendeleza Kwa Kusoma Digrii Yake OPEN UNIVERSITY Akapewa Sharti Atafute Uthibitisho NACTE Kwa Sababu Cheti Chake Hakikuwa na GPA .

Basi Tukalipia Kupata Hicho Cheti NACTE na Ikaonekana Hana Sifa Kwani NACTE Walipocompute Wakaona Ana GPA ya 2.8.

Tukapata Tabu Sana Ikabidi Asafiri Hadi Ofisi za NACTE Mbeya Ambako Walielekezwa na Kupewa Matokeo ya NECTA Yakionyesha Alikuwa na GPA ya 3.0 Lkn NACTE Walikataa Kataaa Kwa Kusema Wao Ndio Wenye Mamlaka na GPA kwa Level Hiyo.

Basi Ndoto ya Kujiendeleza Kwa Mke Wangu Kielimu Ikabidi Iishie Pale Ili Ajipange Upya.

Lkn Bado Hili Jambo Linatushangaza as a Family Inawezekana Vipi Mtihani wa NECTA GPA Yake Iwe Computed na NACTE?

NI VP NECTA NA NACTE HAWANA MAWASILIANO? WANADHANI NI WATANZANIA WANGAPI WAMESHINDWA KUJIENDELEZA KWA UZEMBE KAMA HUU?

KUNA MAMBO YANASHANGAZA SANA KWA BAADHI YA TAASISI HAPA NCHI.

Tsakhodegha

Kutoka Milima ya Livingstone Makete
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom